One Six 'mcharo' wa vibwagizo, ni nguvu ya soda?

Ncha Kali

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2019
Posts
15,335
Reaction score
29,114
Ndugu zangu!

Ni nyimbo mbili tu alizozifanya kwa umahiri na njonjo zilitosha kumleta mjini. Nazo ni 'Anaitwa Roma' na 'Mkombozi' acha ule mwingine. Zote akishirikishwa na Roma Mkatoliki na alifanya poa sana.

Tukasema tumepata mkali wa vibwagizo, japo historia ishajiandika kuwa wengi wa wakali wa viitikio huwa hawasimami kwa miguu yao. Na akisimama basi ni nchecheme kwa muda mfupi tu.

Tuendelee kuiheshimu historia?

One Six, kama u-hai bado basi ujue tunakudai. Ladha uliyotuonjesha tunaitaka tena na tena.

Kama ilikuwa nje ya uwezo wako basi toa japo kawimbo kabovu tu ili tukuchoke tujue MOJA.[emoji16]

Je, ndo inaanza au imeisha?

Kama unamkubali, hebu mpe neno pengine kumtia moyo ikiwa amejikatia tamaa.

Ncha Kali.
 
Huyu one six mimi nilianza kumsikia miaka 9 iliyopita pale Dodoma area A kuna studio ilikuwa Long Miles Records ilikuwa chini ya bwana mmoja anaitwa Msafiri na producer wake alikuwa ni Double Y.

Kwa ufupi nilizisikia nyimbo kama 4, 5 za one six. Jamaa ni fundi na anaujua muziki. Ni suala la muda tu watu watamuelewa. Nikipomsikia mara ya kwanza miaka hiyo niliamini atafika mbali na bado naona atafika mbali.
 
Au niyule wakwene ngoma ya Stamina ile aliyomuimbia cjui mkewe
 
Huyu one six mimi nilianza kumsikia miaka 9 iliyopita pale Dodoma area A kuna studio ilikuwa Long Miles Records ilikuwa chini ya bwana mmoja anaitwa Msafiri na producer wake alikuwa ni Double Y.

Kwa ufupi nilizisikia nyimbo kama 4, 5 za one six. Jamaa ni fundi na anaujua muziki. Ni suala la muda tu watu watamuelewa. Nikipomsikia mara ya kwanza miaka hiyo niliamini atafika mbali na bado naona atafika mbali.

Unaona sasa, miaka 9 mingi sana ila huenda ipo siku yake tu... ingekuwa inatosha kuimba viitikio tu ningeshauri ajikite huko zaidi.
 
Nimekuja upande huu ndugu yangu NCHA KALI

Huyu jamaa one six ni mkali pia siyo kwenye chorus Tu pia ana Ngoma nzuri Tu Ila haizkupewa sikio..mfano ana Ngoma Kali Sana aliiyoa mwaka juzi inaitwa MAYA,hii nyimbo ukiisikililiza Hadi leo ni bonge la hit song

Inasemekana aliimba kuhusu maisha ya kakaake Mez B(walimwengu walivyoconnect dot lakn)
Ni vile Tu media zinawapa nafasi wasanii wabovu wenye kiki na kuwapa kisogo wanaojua
 
Nadhani pia anahitaji kushikwa mkono na watu ambao wanaujua vizuri mziki
 
Ndugu zangu!

Ni nyimbo mbili tu alizozifanya kwa umahiri na njonjo zilitosha kumleta mjini. Nazo ni 'Anaitwa Roma' na 'Mkombozi' acha ule mwingine. Zote akishirikishwa na Roma Mkatoliki na alifanya poa sana.

Tukasema tumepata mkali wa vibwagizo, japo historia ishajiandika kuwa wengi wa wakali wa viitikio huwa hawasimami kwa miguu yao. Na akisimama basi ni nchecheme kwa muda mfupi tu.

Tuendelee kuiheshimu historia?

One Six, kama u-hai bado basi ujue tunakudai. Ladha uliyotuonjesha tunaitaka tena na tena.

Kama ilikuwa nje ya uwezo wako basi toa japo kawimbo kabovu tu ili tukuchoke tujue MOJA.[emoji16]

Je, ndo inaanza au imeisha?

Kama unamkubali, hebu mpe neno pengine kumtia moyo ikiwa amejikatia tamaa.

Ncha Kali.
Nimekesha kwa waganga nimevunja nazi njia panda nimeshikishwa tunguli mkata kabeba majangaaaa huyu jamaa ni hatari
 
Ndugu zangu!

Ni nyimbo mbili tu alizozifanya kwa umahiri na njonjo zilitosha kumleta mjini. Nazo ni 'Anaitwa Roma' na 'Mkombozi' acha ule mwingine. Zote akishirikishwa na Roma Mkatoliki na alifanya poa sana.

Tukasema tumepata mkali wa vibwagizo, japo historia ishajiandika kuwa wengi wa wakali wa viitikio huwa hawasimami kwa miguu yao. Na akisimama basi ni nchecheme kwa muda mfupi tu.

Tuendelee kuiheshimu historia?

One Six, kama u-hai bado basi ujue tunakudai. Ladha uliyotuonjesha tunaitaka tena na tena.

Kama ilikuwa nje ya uwezo wako basi toa japo kawimbo kabovu tu ili tukuchoke tujue MOJA.[emoji16]

Je, ndo inaanza au imeisha?

Kama unamkubali, hebu mpe neno pengine kumtia moyo ikiwa amejikatia tamaa.

Ncha Kali.
Kwakweli kwenye hizo ngoma aliua sana hasa kwenye mkombozi.
 
Back
Top Bottom