One stop business center ya Ubungo ikijengwa itaua Kariakoo na kubadilisha mfumo mzima wa biashara Kwa Tanzania na nchi jirani

One stop business center ya Ubungo ikijengwa itaua Kariakoo na kubadilisha mfumo mzima wa biashara Kwa Tanzania na nchi jirani

Ni kweli serikali wapo serous na hili au stori, ikiwa ni kweli Tanzania itakuwa nusu ya Dubai wachina wanajua sana biashara,tuombe serikali iwe serious
Kariakoo itaimarika zaidi maana china inahamia Ubungo.badala ya kuhangaika na mavisa na mandege mameli ,unasafirisha mzigo wa kutoka china kwa mwendo kasi au guta hadi kariakoo Dar es Salaam
 
Trading is an ignition for main industries!, so trading ina tabia ya ku forecast juu ya biashara inakuwaje? Endapo kitajengwa kiwanda!, GET KNOW THAT!
Kwani Dubai Pana viwanda kama chi
Kuruhusu ule ujenzi maana yake tumeruhusu Tanzania kuwa dampo la bidhaa za China.

Wachinà walipaswa anzisha viwanda ili kukabiriana na upungufu wa ajira.
Kwani Dubai ni mji wa viwanda au ni hub ya viwanda duniani, wanazalisha huko Wana warehouse nyingi na kubwa sana matokeo yake ndipo sokoni kwa sisi wote
 
Ni wachache wana-risk. Wafanyabiashara wakubwa wa electronics Kariakoo kina Mashariki Power, Zabb, wale suppliers wa brands za hadhi ya wabongo kina iAccess, Aldeppo, Oraimo, Rising, Boss, Aborder, etc wengi wao wakiwa Wachina, Wahindi na Waarabu na mixer ya Wachaga na Wakinga wanaitegemea ecosystem ya Kariakoo.

Kariakoo imeishajijenga kiasi kwamba ukibeba milioni 200 yako ukapata flemu mtaa na jengo sahihi, unaanza kuuza on spot bila kuwa na wateja wa kudumu. Unauzia mawinga na wanunuaji wa jumla. Sasa Ubungo haina hiyo ecosystem, anayeenda ajue anaenda kupambana kutafuta wateja uko.

Ikiwa Wachina watapanga pale sawa, which i believe itatokea baada ya majengo kukosa wapangaji wabongo Mchina aliyejenga atafanya lobbying Wachina wapange pale badala ya Kariakoo. Sitegemei wabongo tu ndio waiinue Ubungo nq kuiua Kariakoo.

Na suala la wateja wa rejareja halipo pale. Wakienda Wachina ujue wanalenga jumla, wakienda wabongo rejareja itasumbua. Hakuna route za daladala kama ilivyo Kariakoo. Raia wakilazimisha kwenda pale wataleta foleni kubwa kuliko iliyo Kariakoo. Na Kkoo ina barabara nyingi njia mbili, chocho za kutosha, mwendokasi inazidi kujengwa nyingine na masoko ya bidhaa zote. Pale Ubungo soko la vyakula sidhani kama litakuwepo. Kariakoo ni dude kubwa
Na kama wachina ndo watakao hudumia watu hapo ubungo, patakufa haraka maana ninavowajua wabongo hawapendi sana ku-interract na ngozi nyeupe wasiojua kiswahili vizur na mambo ya kuliakulia kupunguziwa bei, bora waajiri wabongo wakae madukani hapo itakuwa rahisi kwa mbongo kuingia hilo duka, mbongo akiona duka limejaa ngozi nyeupe tuu analipita kama halioni.
 
Itatusaidia kupunguza foleni kwa sehemu na sio kuua kariakoo.
 
Ni kweli serikali wapo serous na hili au stori, ikiwa ni kweli Tanzania itakuwa nusu ya Dubai wachina wanajua sana biashara,tuombe serikali iwe serious
kwa bei ya zile frame sidhani. Yaani square meter 14 wanauza 16m kwa mwaka? sidhani kwa kweli
 
Na kama wachina ndo watakao hudumia watu hapo ubungo, patakufa haraka maana ninavowajua wabongo hawapendi sana ku-interract na ngozi nyeupe wasiojua kiswahili vizur na mambo ya kuliakulia kupunguziwa bei, bora waajiri wabongo wakae madukani hapo itakuwa rahisi kwa mbongo kuingia hilo duka, mbongo akiona duka limejaa ngozi nyeupe tuu analipita kama halioni.
Ubungo haitakuwa na bei za Kiswahili pale ni mzigo wa jumla hivyo hakuna mamantilie ataenda kujiliza apunguziwe bei ya kiswaswadu. Labda mpango wao ubadilike kutofautiana na matangazo yao.
 
Tunaviongozi vichaaa hasa wa awamu hii.hapo wameruhusu wachina Kuja kuchuma Mali za Tanzania na kupeleka kwao china.yaani bidhaa zinazalishwa china Kwa maana ajira ni za wachina halafu wanazileta hapa kutuzuia takataka.Ilitakiwa wajenge kiwanda hapa ili ajira ziwe za wtz na siyo kuwa dumping place for china products.
Bora waje wachina kuuza bidhaa zao ili hao wabongo wanaaochuuza bidhaa za wachina wakawekeze kwenye biashara zingine za kutuwezesha kuexport.
 
Kuna mchina alikuja kariakoo .ana kiwanda kwao huko alipiga helaaa akawa tajiri Hadi akafilisika .yaani alienda kujinyonga.
Hujui wabongo wewe.wanajua jinsi ya kushindana kibiashara
Acha tuone
 
mpaka lini wabongo tutendelea kutumia mavitu feki ya kichina? hali imekuwa mbaya sana mjini, kila kitu cha kichina.
 
Back
Top Bottom