Ni wachache wana-risk. Wafanyabiashara wakubwa wa electronics Kariakoo kina Mashariki Power, Zabb, wale suppliers wa brands za hadhi ya wabongo kina iAccess, Aldeppo, Oraimo, Rising, Boss, Aborder, etc wengi wao wakiwa Wachina, Wahindi na Waarabu na mixer ya Wachaga na Wakinga wanaitegemea ecosystem ya Kariakoo.
Kariakoo imeishajijenga kiasi kwamba ukibeba milioni 200 yako ukapata flemu mtaa na jengo sahihi, unaanza kuuza on spot bila kuwa na wateja wa kudumu. Unauzia mawinga na wanunuaji wa jumla. Sasa Ubungo haina hiyo ecosystem, anayeenda ajue anaenda kupambana kutafuta wateja uko.
Ikiwa Wachina watapanga pale sawa, which i believe itatokea baada ya majengo kukosa wapangaji wabongo Mchina aliyejenga atafanya lobbying Wachina wapange pale badala ya Kariakoo. Sitegemei wabongo tu ndio waiinue Ubungo nq kuiua Kariakoo.
Na suala la wateja wa rejareja halipo pale. Wakienda Wachina ujue wanalenga jumla, wakienda wabongo rejareja itasumbua. Hakuna route za daladala kama ilivyo Kariakoo. Raia wakilazimisha kwenda pale wataleta foleni kubwa kuliko iliyo Kariakoo. Na Kkoo ina barabara nyingi njia mbili, chocho za kutosha, mwendokasi inazidi kujengwa nyingine na masoko ya bidhaa zote. Pale Ubungo soko la vyakula sidhani kama litakuwepo. Kariakoo ni dude kubwa