Onesimo Ole Ngurumwa: Ni Bora Demokrasia ndani ya Udikiteta kuliko Udikteta ndani ya Demokrasia, Uganda ndio Case Study

Onesimo Ole Ngurumwa: Ni Bora Demokrasia ndani ya Udikiteta kuliko Udikteta ndani ya Demokrasia, Uganda ndio Case Study

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2020
Posts
5,532
Reaction score
14,164
Wakili Onesmo Olengurumwa Onesmo Kasale Olengurumwa ambaye ni mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu na Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), kupitia ukurasa wake wa X ametoa somo kuhusu masuala ya Demokrasia akilinganisha mifumo ya Demokrasia kati ya Tanzania na Uganda, amenukuliwa kama ifuatavyo:

"Wale msioelewa kwanini madai ya reforms kwenye mfumo wa uchaguzi nimuhimu sana ni vyema kujifunza kwa wengine. Bahati mbaya suala la
siasa na uongozi wa nchi tunadhani ni la vyama vya siasa pekee. Hali
hii pia inachangiwa na katiba kulazimisha ili mtu awe kiongozi wa
kuchaguliwa lazima apitie kwa chama. Hili ni tatizo kubwa katika
demokrasia ya kweli.

Sasa mkiangalia bunge la Uganda na Bunge la Tanzania utaelewa kuwa
Museven ana afadhali sana na walau kuna demokrasia shirikishi pamoja
na kwamba anaonekana kuwa na chembe chembe za kukandamiza haki na demokrasia.

Bunge la Uganda kwa mujibu wa Kifungu cha 78(1) cha Katiba ya Uganda Bunge la Uganda litaundwa sio na wanasiasa pekee bali na makundi mengine ya kijamii.

Muundo wake unajumuisha wabunge wa kuchaguliwa
majimboni, Mbunge mwanamke wa kuchaguliwa katika kila Wilaya,
Wawakilishi wa vyombo vya usalama, wawakilishi wa vijana , wawakilishiwa wafanyakazi , wawakilishi wa watu wenye ulemavu, wawakilishi waasasi za kiraia pamoja na makundi mengine.

Katika Bunge la sasa la Uganda, kuna jumla ya wabunge 556 kama ifuatavyo;
a) Wabunge wa majimbo 353
b) Wabunge wa Wilaya wanawake 146
c) Wawakilishi wa vyombo vya usalama 10
d) Wawakilishi wa Vijana 5
e) Wawakilishi watu wenye ulemavu 5
f) Wawakilishi wa Wazee 5
g) Wawakiishi wa wafanyakazi 5
h) Na makundi mengine 27

Na katika hawa 353 wanaotokana na vyama majimboni na wale wanawake wa vyamba kila wilaya 146 ambao jumla ni 499 , wabunge 342 ni wa chama tawala NRM, Chama cha NUP cha Bob Wine ambacho ndicho chama kikuu cha upinzani kina viti 57, FDC viti 30, Jema kiti 1, UPC viti 11, PPkiti kimoja ,DP viti 9. Manake ni kwamba upinzani wana viti 157,
Makundi ya Jamii viti viti 69.


Kwa aina hii ya Muundo , walau ni vigumu kumlaumu Museven kwamba hapendi demokrasia. Jambo zuri zaidi ni kwamba bungeni hawapo wanasiasa pekee
wapo wabunge ambao hawajatokana na vyama vya siasa.

Suala la maboresho ya mfumo wa uongozi na mfumo wa uchaguzi hapa nchini ni muhimu sana umoja na maendeleo ya Taifa, watu wote wenye mapenzi mema na nchi hii sidhani kama wanaona ni vyema kuendelea na mifumo hii kama ilivyo kwa kuwa inawapekea kundi la wachache sana kushiriki uongozi wa nchi.

Tusichoke kuonyesha na kudai Katiba mpya itakayotuletea mageuzi mengi hapa nchini. Viongozi watakaokuja kuomba madaraka tunapaswa kuwaambia kazi ya kwanza baada ya kupata uongozi october iwe ni kuendesha mchakato wa katiba mpya.

Twende kwenye uchaguzi na makubaliano kuwa
baada ya uchaguzi tutakuwa na mchakato wa katiba mpya. Tusisubiri kupata Katiba mpya kwenye vita , tupate katiba mpya tukiwa na amani na utulivu ili tuweze kuja na katiba imara zaidi."

Ameandika Wakili Onesmo Ole Ngurumwa.
 
Subiri vijambio vya CCM vinavyojua kutumia vijambio kuhandika na kuongea kuliko huyu
IMG_1352.jpeg
 
Muundo wake unajumuisha wabunge wa kuchaguliwa
majimboni, Mbunge mwanamke wa kuchaguliwa katika kila Wilaya,
Wawakilishi wa vyombo vya usalama, wawakilishi wa vijana , wawakilishiwa wafanyakazi , wawakilishi wa watu wenye ulemavu, wawakilishi waasasi za kiraia pamoja na makundi mengine.
Hawa wote wakiwa ni Chawa hamna kitu.
 
Chawa wamekata pumzi sasa ati wanasifia Chopa la Mama😆😁

Jana huko Katoro machawa wamechoma nyama za bure na kiwagawia wananchi ili wasiende kwenye mkutano wa CHADEMA lakini watu wakala nyama na wakaenda kwenye NO REFORMS NO ELECTION 🤣🤣
 
Wale msioelewa kwanini madai ya reforms kwenye mfumo wa uchaguzi nimuhimu sana ni vyema kujifunza kwa wengine. Bahati mbaya swala la
siasa na uongozi wa nchi tunadhani ni la vyama vya siasa pekee.

Halihii pia inachangiwa na katiba kulazimisha ili mtu awe kiongozi wa kuchaguliwa lazima apitie kwa chama. Hili ni tatizo kubwa katika
democrasia ya kweli.

Sasa mkiangalia bunge la Uganda na Bunge la Tanzania utalewa kuwa
Museven ana afadhali sana na walau kuna democrasia shirikishi pamoja
na kwamba anaonekana kuwa na chembe chembe za kundamiza haki na democrasia.

Bunge la Uganda kwa mujibu wa Kifungu cha 78(1) cha Katiba ya UgandaBunge la Uganda litaundwa sio na wanasiasa pekee bali na makundi mengine ya kijamii. Muundo wake unajumuisha wabunge wa kuchaguliwa
majimboni, Mbunge mwanamke wa kuchaguliwa katika kila Wilaya,
Wawakilishi wa vyombo vya usalama, wawakilishi wa vijana , wawakilishiwa wafanyakazi , wawakilishi wa watu wenye ulemavu, wawakilishi waasasi za kiraia pamoja na makundi mengine.

Katika Bunge la sasa la Uganda, kuna jumla ya wabunge 556 kama ifuatavyo;
a) Wabunge wa majimbo 353
b) Wabunge wa Wilaya wanawake 146
c) Wawakilishi wa vyombo vya usalama 10
d) Wawakilishi wa Vijana 5
e) Wawakilishi watu wenye ulemavu 5
f) Wawakilishi wa Wazee 5
g) Wawakiishi wa wafanyakazi 5
h) Na makundi mengine 27

Na katika hawa 353 wanaotokana na vyama majimboni na wale wanawake wa vyamba kila wilaya 146 ambao jumla ni 499 , wabunge 342 ni wa chama tawala NRM, Chama cha NUP cha Bob Wine ambacho ndicho chama kikuu cha upinzani kina viti 57, FDC viti 30, Jema kiti 1, UPC viti 11, PPkiti kimoja ,DP viti 9. Manake ni kwamba upinzani wana viti 157,
Makundi ya Jamii viti viti 69.

Kwa aina hii ya Muundo , walau ni vigumu kumlaumu Museven kwamba hapendi democrasia. Jambo zuri zaidi ni kwamba bungeni hawapo wanasiasa pekee
wapo wabunge ambao hawajatokana na vyama vya siasa. Swala la maboresho ya mfumo wa uongozi na mfumo wa uchaguzi hapa nchini ni muhimu sana umoja na maendeleo ya Taifa, watu wote wenye mapenzi mema na nchi hii sidhani kama wanaona ni vyema kuendelea na mifumo hii kama ilivyo kwa kuwa inawapekea kundi la wachache sana kushiriki uongozi wa nchi.

Tusichoke kuonyesha na kudai Katiba mpya itakayotuletea mageuzi mengi hapa nchini. Viongozi watakaokuja kuomba madaraka tunpaswa kuwambia kazi ya kwanza baada ya kupata uongozi october iwe ni kuendesha mchakato wa katiba mpya. Twende kwenye uchaguzi na makubaliano kuwa
baada ya uchaguzi tutakuwa na mchakato wa katiba mpya. Tusisubiri kupata Katiba mpya kwenye vita , tupate katiba mpya tukiwa na amani na utulivu ili tuweze kuja na katiba imara zaidi.

Wikiend Njema , Wakili Olengurumwa 10/5/2025
 

Attachments

  • IMG-20250511-WA0002.jpg
    IMG-20250511-WA0002.jpg
    149.6 KB · Views: 24
Back
Top Bottom