SoC02 Ongeza kipato chako kwa kuzingatia njia hizi 3

SoC02 Ongeza kipato chako kwa kuzingatia njia hizi 3

Stories of Change - 2022 Competition

Sofago

New Member
Joined
Aug 2, 2022
Posts
4
Reaction score
4
Umeshawahi kujiuliza, utaongeza vipi pesa ambayo unaipata katika maisha yako? Watu wengi sana wanatamani kuongeza kipato chao ila mara nyingi wanatumia njia ambazo sio sahihi kujipatia au kujiongezea kipato. Leo ningependa ujifunze njia rahisi na sahihi ambazo unaweza kuzitumia kuanzia sasa na ukajiongezea kipato chako.

Screenshot_20220807-102028_1.jpg


1. Utayari wa kutatua matatizo ya watu.

Jambo la kwanza kabisa unalotakiwa kujiuliza unapotaka kuongeza kipato chako ni kwamba je, upo tayari kutatua matatizo ya watu? Sehemu moja wapo pesa zilipojificha ni kwenye matatizo yanayowakabili watu mbali mbali na leo utajifunza jinsi ya kuchukua pesa zilizojificha kwenye matatizo ya watu.

Tafrisi kubwa ninayopenda kuitumia kuhusu pesa ni ile inayosema 'pesa ni zawadi unayopata baada ya kutatua tatizo la mtu flani', kwani huu ni ukweli usiopingika kabisa. Ukitaka kujua tafsiri hii imebeba uzito mkubwa kwenye maisha yako jiulize siku ya leo umetumia pesa kiasi gani kufanyia mahitaji yako, hapo ndipo utagundua kuwa yupo mtu uliyempatia pesa yako akakutatulia tatizo lako ambalo wewe huna uwezo wa kulitatua au huna muda wakutosha wa kulitekeleza mwenyewe hivyo umemruhusu mtu afanye kwa niaba yako.

Hii ikiwa na maana kwamba njia kubwa ya kupata pesa ni kutatua tatizo au matatizo ya watu wengine. Kadiri utakavyo tatua matatizo mengi na makubwa kwa watu ndivyo kipato chako kitaongezeka kwa wingi. Hii inamaanisha kwamba kama kipato chako ni kidogo kwa sasa basi utambue bado hujafanikiwa kutatua matatizo mengi yanayo wakabili watu.
images - 2022-08-04T171642.761.jpeg

Kila sehemu yapo matatizo yanayowakabili watu na yanahitaji watatuzi hivyo ni wewe mwenyewe kuchagua aina ya tatizo ambalo lipo ndani ya uwezo wako na unaweza kulitatua.

Kabla hujaendelea kusoma makala hii, jiulize katika mazingira yanayokuzunguka ni tatizo gani linawakabili watu ambalo unaweza kulitatua? Haijalishi upo eneo gani hata kama ni shuleni, ofisini, nyumbani kwako au hata popote cha msingi watu wawepo. Pia unaweza hata kupita kwa wahusika na kuwauliza changamoto zinazowakabili ili iwe rahisi kwako hata kama ni kuanzisha biashara basi iwe inatatua changamoto zao kwa kiasi kikubwa.

Baadhi ya watu wamekuwa wakilalamika kuhusiana na mitaji, nakushauri kwamba ukitaka kuanzisha biashara unapaswa kuanza na kile ambacho kipo ndani ya uwezo wako.


2. Ongeza thamani katika kile unachokifanya.

Unachotakiwa kujua ni kwamba watu hukupa fedha zao kulingana na thamani ya kile unachowapa, hii inamaana kwamba kama utashindwa kuboresha thamani ya biashara yako basi itakuwa vigumu sana watu kukuletea pesa zao ili uwahudumie. Kufanya kazi kwa werevu na maarifa makubwa hii inatusaidia sana katika kukuza kipato chetu.

Jaribu kuchunguza, wapo watu wanaofanya kazi kwa bidii sana lakini bado kipato chao hakiridhishi, wanaamka mapema na kuchelewa kulala lakini bado pesa wanayopata hailingani na juhudi zao. Kama wewe ni mmoja wa watu hawa basi fuata njia hizi ili thamani yako katika kazi au biashara yako iongezeke.

3. Hakikisha unajenga sifa ya kuaminika kwa kila jambo.
Unapojenga uaminifu kwa watu, inakuwa rahisi sana kuzipata pesa zao au hata kupata fursa kutoka kwa watu wengine kutokana na uaminifu uliojijengea. Kama wewe ni mfanyabiashara jitahidi sana kutimiza ahadi unazowapa wateja wako, itakusaidia sana katika kuikuza biashara yako kwa kupata wateja wengi zaidi.

images (71).jpeg

Nakushukuru kwa muda wako uliotumia kusoma makala hii. Natumai umevutiwa na ungependa kupata habari zaidi.

Basi bofya neno FOLLOW kulia juu na kutoa maoni yako chini ya habari hii kisha kuSHARE kwa wengine. Ubarikiwe Sana!
 
Upvote 3
Nime kupigia kura

Asante sana kwa ushauri mzuri kwa upande wa vijana kama sisi tunao ingia kwenye kujitegemea kimaisha lakini hapo ongezea kipengele cha nne vijana tusisahau kufanya na ibada ni muhimu sana .
 
Shukrani sana....nimepokea ushauri wako pia

Nime kupigia kura

Asante sana kwa ushauri mzuri kwa upande wa vijana kama sisi tunao ingia kwenye kujitegemea kimaisha lakini hapo ongezea kipengele cha nne vijana tusisahau kufanya na ibada ni muhimu sana .
 
Back
Top Bottom