Elifuraha Longu
Member
- May 8, 2014
- 73
- 10
Kumekuwepo na ongezeko la bei ya vyumba vya kupangisha kila mara, wamiliki wa majumba wamekuwa wakipandisha kodi kila mwaka jinsi wanavyopenda wao maana hakuna sheria yeyote inayowabana. Mfano; Jiji la Arusha kodi ya chumba cha chini ni Tsh20,000-30,000 kwa mwezi (single room) huku duble vinaanzia Tsh40,000-60,000 kwa mwezi.
Na vyumba vyenye hadhi nzuri vinaanzia Tsh40,000-60,000 kwa mwezi (single room) huku duble ni 60,000-150,000 kwa mwezi. Na hizi kodi ni nje na bili ya umeme. Pia bei hizi hutofautiana kutoka eneo moja kwenda eneo jingine. Hali hii huwafanya wapangaji kushindwa kujimudu kimaisha kutokana na kuwa kodi zipo juu na kipato/mishahara wanayopata kwa mwezi ni kidogo sana. Kwa mtazamo wangu naona ni vizuri pawepo na sheria itakayowabana mamiliki wa vyumba.