Tetesi: Ongezeko la masharti ukitaka kufungua akaunti ya Benki lazima kuongezea kiapo cha mahakama licha ya kuwa na vitambulisho husika

Kumbe hakuna aliyejua Magu anatupeleka wapi. Sasa tunaanza kupata mwelekeo, lakini nao bado hatujaufahamu. Tuendelee kusubiri.

Kuna wanaobuni kuwa tunaelekea kwenye Ujamaa. Mi sijui kama ni ujamaa tu au tutapitiliza mpaka UKOMUNIST. Tusubiri!!!!!
 
Nimeenda NBC Leo hii wananiambia niwe na uthibitisho wa mwanasheria ,hii siyo tetesi sema ni habari kamili
Hi ni njia ya kutengenezea watu ulaji. Kuna wanasheria (advocates) wengi hawana ajira na hii itawasaidia kuwapa kipato hivyo kupunguza wasio na kazi mitaani.
 
pole sana chief,.
 

Kitambulisho cha kibongo siyo smart card ( haki hifadhi data zozote) ..Hichi kitambulisho ni cha hovyo kabisa.
United States of America masharti sio kiasi hiki aisee!

Unbankable population itaongezeka!

Tulisema kitambulisho cha taifa kita-solve everything,ila naona it is useless on every step!

Kitambulisho cha taifa ni cha kizamani na kishamba wala hakifai kuaminiwa.Siyo smart ID card (hakihifadhi data zozote za mwenye nacho) .Wakati dunia ya sasa wenzao wanatumia smart ID card
 
Mkuu hawa wehu walituaminisha kua ndio suluhisho la hizi korokoro zote!

Sasa kama ni hovyo namna hiyo nadhani wakubeba lawama ni serikali ya CCM!

Tunateswa tangu mwaka 1961 mpaka leo,na bado shida inakua kubwa zaidi.....I wish wakoloni warudi wawe wanatuchapa viboko kabisa ila uchumi na maendeleo yaje ila sio hizi ngendembwe za CCM na watu wake aisee!

Im tired of this country,Im tired of this life,No hope whatsoever!

Where will we turn to?Life is not fair kabisa!
 
Kila mara wanakuja na project za kupiga hela tu.Hivi viambulisho hawatakaa muda mrefu watakuja na mradi wa kuingia kwenye smart ID card
 
Dr. Bashiru, kuna siku alisema CCM bado inasimamia azimio la Arusha, ambalo kimsingi ni azimio linaolezea mfumo wa kijamaa. Itakuwa ni kosa kubwa sana kuirudisha nchi katika misingi ambayo haikuwa na matokeo chanya kwa taifa.
 
Sijui unaongea nini.

Kuna 'presumtion of regularity of official acts'. Yani shughuli za serikali zinadhaniwa kua zimefuata sheria.

Sasa kitambulisho nitoe Nida kisheria kabisa then niende bank halafu uniambie nirudi Nida wanipe verification ya icho kitambulisho...si utakua wehu huo??

Bank wanatakiwa wapokee kitambulisho kama kilivyo ila kama watakitilia mashaka(reasonable suspicion) ndo wanaweza kuomba further verification from NIDA...

Ndo tatizo la nchi kuongozwa na vilaza...elimu haijawasaidia kuelemika kabisa.

Hasa ilo lenye PhD ya maganda ya Korosho....bora yule wa ngumbaro
 

Sasa hapa ndio umeeleza nini, mbona unachanganyachanganya tu. Kwani uliyoeleza hapa ndio ujamaa ulioutaja kwenye mchango wako huko juu?

'Literacy rate' ya China na hayo yanayofanyika Bank, unayoyaita Ujamaa, yana uhusiano gani?

In short, hakuna lolote uliloeleza hapa kuhusu Ujamaa na hayo mambo yanayofanyika huko benki.

Nimekupa mfano wa China kwa sababu ya wimbo wako huo wa 'Ujamaa', kumbe hata hukuweza kuelewa chochote.

Ukinitajia Kenya 'kutengeneza mazingira mazuri ya biashara' inanipa picha nzuri ya kukuelewa. Nikupe mfano tu wa mazingira mazuri unayoyasema: angalia uagizaji wa sukari uliofanyika mwaka jana na kuingiza tani karibu ya millioni moja na matatizo yaliyotokana na swala hilo.

Huo ni mfano mmoja tu, lakini sidhani kuwa uko 'informed' vya kutosha kuelewa nazungumzia nini.

Labda utaelewa kutengeneza mabilionea wa dola za kimarekani 30 kwa mwaka mmoja, 2017; wakati wananchi milioni mojatu ndio wanavuka toka kwenye rindi la umaskini ndani ya miaka 10! Hayo ndio mazingira mazuri!

Elewa kuwa wewe kuwa mfanya biashara haikupi hati miliki ya kuelewa mambo 'vizuri' kuliko wengine.
 
Vipi kuhusu mama muuza mboga mboga je, ataweza kumudu gharama za kumlipa advocate??
Hi ni njia ya kutengenezea watu ulaji. Kuna wanasheria (advocates) wengi hawana ajira na hii itawasaidia kuwapa kipato hivyo kupunguza wasio na kazi mitaani.
 
Naomba kujua masharti na vigezo vya kufungua account nje ya nchi yangu wakuu[emoji41]
 
Labda umechelewa tu kufahamu, toka muda mrefu sana,ikipita pesa isiyo ya kawaida katika acc yako wanazuia,mpaka maelezo ya kina ilipotoka.

Na mkijifanya mnazichimbia tunachapisha noti mpya pumbaavu.

Hamuwezi kuwa na akili kila wakati,na watu wakawa wanakosea wakati wote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…