Tetesi: Ongezeko la masharti ukitaka kufungua akaunti ya Benki lazima kuongezea kiapo cha mahakama licha ya kuwa na vitambulisho husika

Tetesi: Ongezeko la masharti ukitaka kufungua akaunti ya Benki lazima kuongezea kiapo cha mahakama licha ya kuwa na vitambulisho husika

Mkuu nadhani umekariri tu,kuna mabadiliko sana kwa sasa! Mimi ni muathirika wa hii issue. Niliuza nyumba yangu mkoani zaidi ya 60mil. Me nilikuwa na akaunti yangu kwenye bank ambayo haina branch huko. Nikalazimika kufungua akaunti kwenye moja ya hizi bank zenye nasaba na serikali. Na wakati nafungua nilijieleza km nalipwa pesa za kuuza nyumba yangu. Na mtu aliyekuwa ananilipa ana akaunti hapohapo ktk ile bank. Nilifanya taratibu zote na pesa ikaingizwa. Baada ya siku 2 nilifanikiwa ku-withdraw milioni 3 na nusu. Na nikarudi dar. Nimefika dar nimekaa km wiki moja,nikaenda kumlipa mtu milioni 35 za nyumba ambayo nilitaka kununua hapa mjini. Nikakuta nimepigwa pin. Yaani mpaka hv nnavyoandika nimeshapeleka vielelezo vyote nilivyoombwa lkn bado sijaruhusiwa kutumia pesa zangu mwenyewe. Na ni kesi ya tangu mwaka Jana mwezi wa 9. Yaani hata kuchukua elf 20 siwezi. Hii nchi imeshaharibika. Nyumba sina na hela sina! Usicheze na jiwe mkuu,ndo maana kila siku anasema hela zipo!

Ase Pole. Hii hatari. Huko sikukaa na ugonjwa wa Pressure kama Jiko na sufuria?
 
Awamu ya tano ni awamu ya kuwatia hofu wananchi kwa miaka yote tokea iimgie madarakani, lakini wajanja wachache wakiwemo mameneja wa mabenk wamepiga pesa za wateja kwa visingizio kuwa A/c zao zinachunguzwa na vyombo vya Dola wamekuwa wakila njama kisha kula pesa za watu, wametumia fursa hizo kujinufaisha na sasa Bank zinazidi kuongeza kero kwa wateja wao unategemea nini zaidi ya wananchi kuendelea kuichukia zaidi Serikali ya mtukufu toka chato?


Hilo nalo neno! Usikute kweli wajanja wameona njia ya kutokea ndiyo imeshapatikana.
 
Mkuu umeandika Kwa hisia lakini umeshindwa kupata the big picture na bahati mbaya kabisa wewe ni muumini wa Ujamaa..., Okay IPO hivi....
Kama umeajiriwa serikali I au mahali ambapo unapata kipato cha wastani hutaelewa kinachozungumzwa, Hadi utakapokuwa na biashara yako au upewe usimamizi wa biashara kubwa ndipo utaelewa vizuri...
Issue ya money laundering sio kitu cha kuzuia Kwa kuweka beuracracy zisizo na maana na kuchelewesha biashara bila sababu..."follow the money"
Bado policy nyingine za hovyo kabisa zinaendelea kuwa implemented as if tumetoka kwenye vita....
Government unapotaka Ku control everything na ikibidi kufanya biashara na kuongeza urasimu ni kutengeneza umasikini wa kujitakia kwenye taifa..sijui kwanini hamtaki kuelewa hili...
Lakini mnapojifananisha na Uchina manchekesha Sana.... Unaelewa literacy rate ya mchina wa kawaida compared na hawa waswahili wavaa Madera wa Temeke? Au mna day dream Tu.....
Kwanini msijifananishe na SA? au Botswana au Nigeria au Ghana.....au Kenya katika kutengeneza mazingira Bora ya biashara...? To make few premium who can pay all the taxes? Mnakimbizana na kuporwa Hadi hela za mifuko ya jamii?
Mkuu ,hongera kwa uchambuzi makini,si sahiho hata kidogo kufananisha China na Tanzania kwa kitu chochote kile.
 
Nani kakutukana ? Ukiambiwa kichwa Kama embe ndio tusi ???
Acheni kutafuta sympathy kwa ujinga ujinga wenu.
Narudia tena wewe si tu ni embe Bali ni Una kichwa KAMA EMBE BOLIBO BICHI.
Sasa nakusubiri uje na Huruma zako za Kingazinja nikufumue kisawasawa, Tabulasa wewe.
The best I can do ni kusema tuu asante, na ukiweza kufumua, huna haja ya kusubiria nije, be free kufumua tuu, if kwa kufumua, makes you happy, be happy.
P
 
Tatizo la watanzania tunaongea lugha tofauti,, siku tukikubali kuongea lugha moja haya matatizo yatakwisha.
 
Ujamaa 💯....
Alijaribu Nyerere alikiona kiti kichungu.....
Pengine itauzia money laundering and those stuffs, Ila kiukwel too much beuracracy has never been a a good indicator for economy growth....
Hapa Kenya na Uganda tutwasikia tu kwenye list za middle class economy....
Tutaburuzika for another good100yrs....
Tanzania ni vulnerable hasa kwa vitendo vya kigaid na uvushaji wa pesa sishangai kuchujuliwa hizi hatua kila nchi hasa za ulaya huwezi pitisha hela kinyemela tu hata bank inakukaba koo bika serikali
 
Nimeenda NBC Leo hii wananiambia niwe na uthibitisho wa mwanasheria ,hii siyo tetesi sema ni habari kamili
Huo uthibitisho wa mwanasheria unathibitisha nini?? Mbona tunapangiana sana matumizi siku hizi??
 
Ujamaa huu unaharibu nchii na kuturudisha nyuma kimaendeleo.

Siujui ni wawekezaji gani watakuja kuwekeza kwenye nchi yenye sera mbovu kama hizi za ujamaa uchwara!
Nyie watu hamjasafiri,hebu fanyeni utafiti mjue wenzenu wanafanyaje
Marekani ukitumia tu ATM ukiwa nje ya nchi utapigiwa simu na kadi kufungiwa,lazima uiage benki kua unaenda Tanganyika!
 
Back
Top Bottom