KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Ujamaa 💯....
Alijaribu Nyerere alikiona kiti kichungu.....
Pengine itauzia money laundering and those stuffs, Ila kiukwel too much beuracracy has never been a a good indicator for economy growth....
Hapa Kenya na Uganda tutwasikia tu kwenye list za middle class economy....
Tutaburuzika for another good100yrs....
"Ujamaa upo wapi katika hayo aliyoyaelezea Britannica hapo juu.
Ni jambo la kusikitisha sana kwa baadhi ya watu kudhani kwamba maana ya 'Ujamaa' ni kuzuia watu wasiwe na maisha bora.
Tafsiri hii wanailazimisha kila mahali panapotokea kuwa na matatizo ya uchumi, hata kama matatizo hayo hayana uhusiano wowote na Ujamaa.
Kwa hiyo jambazi akiua na kupata pesa nyingi na kufanikisha maisha yake, tusifu kuwa "Ubepari" ni mzuri?
Unapotoa mfano wa Kenya kufanikiwa kwa ubepari, ina maana Kenya wanaruhusu utakasishaji wa pesa kupitia kwenye mabenki?
Unapoimba,' Ujamaa, Ujamaa', umezuiwa kufanya shughuli zako halali kwa kufuata taratibu ili ujiletee mafanikio, au unataka uachiwe mianya ya kuwaumiza wengine?
China bado ni waCommunist, wameendelea mpaka walipofikia wakiwa ndani ya mfumo wa kiCommunist. Leo wewe bado umelala kwenye nyimbo zilezile walizoachana nazo wengi. Usidhani Ubepari ni kila kitu. Beza 'Ujamaa, lakini elewa kwamba nao una mchango mkubwa katika ufanisi wa taifa lolote, hata huko wanakojitambulisha kuwa Mabepari wa Ulimwengu.
Achana na nyimbo za kutapishwa kama Kasuku. Tumia akili yako uliyojaliwa kupambanua mambo.muhimu kama haya.
Kama utaratibu ni mbaya benki, sio lazima iwe sababu ya 'Ujamaa'.