Tetesi: Ongezeko la masharti ukitaka kufungua akaunti ya Benki lazima kuongezea kiapo cha mahakama licha ya kuwa na vitambulisho husika

Ujamaa 💯....
Alijaribu Nyerere alikiona kiti kichungu.....
Pengine itauzia money laundering and those stuffs, Ila kiukwel too much beuracracy has never been a a good indicator for economy growth....
Hapa Kenya na Uganda tutwasikia tu kwenye list za middle class economy....
Tutaburuzika for another good100yrs....

"Ujamaa upo wapi katika hayo aliyoyaelezea Britannica hapo juu.

Ni jambo la kusikitisha sana kwa baadhi ya watu kudhani kwamba maana ya 'Ujamaa' ni kuzuia watu wasiwe na maisha bora.

Tafsiri hii wanailazimisha kila mahali panapotokea kuwa na matatizo ya uchumi, hata kama matatizo hayo hayana uhusiano wowote na Ujamaa.

Kwa hiyo jambazi akiua na kupata pesa nyingi na kufanikisha maisha yake, tusifu kuwa "Ubepari" ni mzuri?

Unapotoa mfano wa Kenya kufanikiwa kwa ubepari, ina maana Kenya wanaruhusu utakasishaji wa pesa kupitia kwenye mabenki?

Unapoimba,' Ujamaa, Ujamaa', umezuiwa kufanya shughuli zako halali kwa kufuata taratibu ili ujiletee mafanikio, au unataka uachiwe mianya ya kuwaumiza wengine?

China bado ni waCommunist, wameendelea mpaka walipofikia wakiwa ndani ya mfumo wa kiCommunist. Leo wewe bado umelala kwenye nyimbo zilezile walizoachana nazo wengi. Usidhani Ubepari ni kila kitu. Beza 'Ujamaa, lakini elewa kwamba nao una mchango mkubwa katika ufanisi wa taifa lolote, hata huko wanakojitambulisha kuwa Mabepari wa Ulimwengu.

Achana na nyimbo za kutapishwa kama Kasuku. Tumia akili yako uliyojaliwa kupambanua mambo.muhimu kama haya.

Kama utaratibu ni mbaya benki, sio lazima iwe sababu ya 'Ujamaa'.
 
Kuwa na kitambulisho pekee haitoshi kuweza kutambuliwa maana hapa Tanzania hakuna miundo mbinu ya kuweza kuhakikisha vitambulisho vyako.

'Excuse' ya ovyo kabisa.

Kwa hiyo kila anayetaka kusafiri aende mahakamani kujua kuwa Passport' yake ni halali?

Ni kitu gani kinazuia hivyo vitambulisho vilivyopo visilindiwe uhalali wake!

Huko mahakama ndiko kuna malaika?
 
Pamoja na kwamba hata kama utakuwa na vitambulisho vyoote husika lakin muhim kuwa na kiapo cha mahakamani kwa taarifa unazotoa wakati wa ufunguzi wa akaunt,

Wakati huo huo akaunt zote ambazo zitaonekana kupitisha hela kubwa kubwa zitachunguzwa na wakibaini hela inapita tu bila kuwa na uthibitisho wa hela zako, akaunt inazuiliwa, na kiasi chenyewe ni zaid ya milion 50 kwa miezi kadhaa
Kwa wafanyakazi wa ENI EMU BII ninyi ni mashahidi wamepokea waraka toka BII OO TII kwamba hakuna mtu ku deposit zaid ya milion 40 bila maelezo zimetoka wapi

Pia kwamba Huruhusiwi kufungua akaunt mbili za aina moja ndani ya benki moja kama ilivyokuwa zamani,

Stay tuned,

Britannica,
Mkuu britanica tuseme nikiingiziwa bongo kwenye akaunti yangu kama euro laki tano inaruhusiwa? Nauliza tu kwa mfano amani iwepo tu
 
Mkuu Britannica, asante kwa taarifa hii, kwenye ukweli unaleta za kweli kabisa tena za Moto moto kutoka jikoni, ila pia ni mpishi mzuri, ukiamua kupika, na viungo unavyo pikia, pilau na biriani zitasubiri, kama ile ya kisiwa cha Guam.
P
how are you my bro pascal, have missed your contribution here, or were you busy,? now i think this country is headed for the DITCH, next time utasikia ukitaka kuoa na vitambulisho vya bibi na babu, na mashangazi , na report ya mwanasheria kuoyesa ya kuwa wewe si tu hujaoa, lakini hujawai onekana na binti wingine isipokuwa huyu unaoa, i tell you COMMUNISM IS KNOCKING AT US, have a blessed week
 
"Ujamaa upo wapi katika hayo aliyoyaelezea Britannica hapo juu.

Ni jambo la kusikitisha sana kwa baadhi ya watu kudhani kwamba maana ya 'Ujamaa' ni kuzuia watu wasiwe na maisha bora.

Tafsiri hii wanailazimisha kila mahali panapotokea kuwa na matatizo ya uchumi, hata kama matatizo hayo hayana uhusiano wowote na Ujamaa.

Kwa hiyo jambazi akiua na kupata pesa nyingi na kufanikisha maisha yake, tusifu kuwa "Ubepari" ni mzuri?

Unapotoa mfano wa Kenya kufanikiwa kwa ubepari, ina maana Kenya wanaruhusu utakasishaji wa pesa kupitia kwenye mabenki?

Unapoimba,' Ujamaa, Ujamaa', umezuiwa kufanya shughuli zako halali kwa kufuata taratibu ili ujiletee mafanikio, au unataka uachiwe mianya ya kuwaumiza wengine?

China bado ni waCommunist, wameendelea mpaka walipofikia wakiwa ndani ya mfumo wa kiCommunist. Leo wewe bado umelala kwenye nyimbo zilezile walizoachana nazo wengi. Usidhani Ubepari ni kila kitu. Beza 'Ujamaa, lakini elewa kwamba nao una mchango mkubwa katika ufanisi wa taifa lolote, hata huko wanakojitambulisha kuwa Mabepari wa Ulimwengu.

Achana na nyimbo za kutapishwa kama Kasuku. Tumia akili yako uliyojaliwa kupambanua mambo.muhimu kama haya.

Kama utaratibu ni mbaya benki, sio lazima iwe sababu ya 'Ujamaa'.
Mkuu umeandika Kwa hisia lakini umeshindwa kupata the big picture na bahati mbaya kabisa wewe ni muumini wa Ujamaa..., Okay IPO hivi....
Kama umeajiriwa serikali I au mahali ambapo unapata kipato cha wastani hutaelewa kinachozungumzwa, Hadi utakapokuwa na biashara yako au upewe usimamizi wa biashara kubwa ndipo utaelewa vizuri...
Issue ya money laundering sio kitu cha kuzuia Kwa kuweka beuracracy zisizo na maana na kuchelewesha biashara bila sababu..."follow the money"
Bado policy nyingine za hovyo kabisa zinaendelea kuwa implemented as if tumetoka kwenye vita....
Government unapotaka Ku control everything na ikibidi kufanya biashara na kuongeza urasimu ni kutengeneza umasikini wa kujitakia kwenye taifa..sijui kwanini hamtaki kuelewa hili...
Lakini mnapojifananisha na Uchina manchekesha Sana.... Unaelewa literacy rate ya mchina wa kawaida compared na hawa waswahili wavaa Madera wa Temeke? Au mna day dream Tu.....
Kwanini msijifananishe na SA? au Botswana au Nigeria au Ghana.....au Kenya katika kutengeneza mazingira Bora ya biashara...? To make few premium who can pay all the taxes? Mnakimbizana na kuporwa Hadi hela za mifuko ya jamii?
 
Mkuu britanica tuseme nikiingiziwa bongo kwenye akaunti yangu kama euro laki tano inaruhusiwa? Nauliza tu kwa mfano amani iwepo tu
Inaruhusiwa ila uitolee maelezo, ila Euro 500,000 ni parefu utaambiwa fisadi
 
Mkuu Britannica, asante kwa taarifa hii, kwenye ukweli unaleta za kweli kabisa tena za Moto moto kutoka jikoni, ila pia ni mpishi mzuri, ukiamua kupika, na viungo unavyo pikia, pilau na biriani zitasubiri, kama ile ya kisiwa cha Guam.
P
We Pascal kichwa kama embe,
 
Pamoja na kwamba hata kama utakuwa na vitambulisho vyoote husika lakin muhim kuwa na kiapo cha mahakamani kwa taarifa unazotoa wakati wa ufunguzi wa akaunt,

Wakati huo huo akaunt zote ambazo zitaonekana kupitisha hela kubwa kubwa zitachunguzwa na wakibaini hela inapita tu bila kuwa na uthibitisho wa hela zako, akaunt inazuiliwa, na kiasi chenyewe ni zaid ya milion 50 kwa miezi kadhaa
Kwa wafanyakazi wa ENI EMU BII ninyi ni mashahidi wamepokea waraka toka BII OO TII kwamba hakuna mtu ku deposit zaid ya milion 40 bila maelezo zimetoka wapi

Pia kwamba Huruhusiwi kufungua akaunt mbili za aina moja ndani ya benki moja kama ilivyokuwa zamani,

Stay tuned,

Britannica,
Huu ujinga ndiyo unawafanya wananchi wengi kuhifadhi pesa ndani na wengine kuweka kwenye mitandao pasipo kwenda huko Bank, hayo mashariti ya kijinga jinga yatazidhoofisha bank
 
Hii sio salama kwa banking industry,inaongeza usumbufu kwa wateja wapya.
 
KWENYE HUU UZI HUWEZI KUWAONA KINA ISIS, KIPARA KIPYA, RUTASHOBORWA AND CO. SASA NGOJA UJE UZI WA KUMSIFIA CHIEF JANGA AU WA KUMPONDA MBOWE WATAKAVYOUSHAMBULIA KAMA NYUKI MZINGANI.
 
Watu hawataweka weka fedha Bank
Bank wengi sasa wamekuwa wajinga sana wanatoa Siri za wateja, watanzania wenye pesa nyingi wameamua kuweka pesa zao Uganda, Kenya na sehemu zingine Duniani ambapo hakuna Ujinga huo usiokuwa na manufaa kwa wananchi kwani pesa zote wanazokamata na kupora kwenye Acount za watu ni mtukufu na Bashite wanagawana na zingine kujengea Chato Airport isiyo na Tija kwa Taifa
 
Mkuu Britannica, asante kwa taarifa hii, kwenye ukweli unaleta za kweli kabisa tena za Moto moto kutoka jikoni, ila pia ni mpishi mzuri, ukiamua kupika, na viungo unavyo pikia, pilau na biriani zitasubiri, kama ile ya kisiwa cha Guam.
P

Kwa ufahamu wangu naona umehitimisha kuwa hili kapika!
 
Hii sio salama kwa banking industry,inaongeza usumbufu kwa wateja wapya.
Nchi hii sasa imekuwa Nchi ya usumbufu kwa wananchi wake badala ya kuwapenda viongozi wamegeuka kuwa wasumbufu, mara visima vya maji ambavyo wananchi wamejichimbia kwa gharama zao lakini wanataka pesa na sasa wanazidi kuwakera wananchi hawajui kuwa uchaguzi wa 2020 watagoma kujitokeza kupiga kura maana CCM imekuwa Sumu kwao ingawa CCM watafanya uchakachuaji kujipa ushindi kwa njia haramu lakini yafaa watambue kuwa watanzania sasa wanaichukia Serikali ya mtukufu na Naibu Rais ndugu Bashite kwa kiwango cha kutisha.
 
Hizi tetesi zikiendelea kwa staili hii si afya kwa uchumi wetu. BOT wanafaa kuchukua hatua na kulitolea msimamo. Taratibu watu wataanza kuishi na pesa chini ya vitanda na mwisho Benki kukosa uaminifu.
 
KWENYE HUU UZI HUWEZI KUWAONA KINA ISIS, KIPARA KIPYA, RUTASHOBORWA AND CO. SASA NGOJA UJE UZI WA KUMSIFIA CHIEF JANGA AU WA KUMPONDA MBOWE WATAKAVYOUSHAMBULIA KAMA NYUKI MZINGANI.
Tenda ya kuwatetea CCM kwenye mitandao na kwenye magazeti walipewa Le mutuz na Musiba wanalipwa mapesa mengi lakini wanatumia kwenye michepuko ndipo wakaamua kuwaajiri vilaza wajinga wajinga wenzao wenye Akili ndogo kama zao ili wawalipe pesa ndogo wapate kubaki na pesa nyingi waendelee kula bata na michepuko kila kona
 
Hizi tetesi zikiendelea kwa staili hii si afya kwa uchumi wetu. BOT wanafaa kuchukua hatua na kulitolea msimamo. Taratibu watu wataanza kuishi na pesa chini ya vitanda na mwisho Benki kukosa uaminifu.
Naunga hoja yako kwa 100%
 
Back
Top Bottom