SHAIRI KUHUSU USHOGA NA USAGAJI
1. Mikono ninaipunga, salamu nipate jenga
Salamu hiyo yalenga, janga lilotia nanga
Watu wamepigwa changa, wa tayari kuwahonga
Ushoga jamani janga, sasa linaziba mwanga
2. Ushoga jamani janga, sasa linaziba mwanga
Wengi wamepigwa chenga, eti pesa inalonga
Tukatae hu ujinga, kwa Neno pia kupinga
Ushoga jamani janga sasa linaziba mwanga
3.Si ushoga peke yake, Usagaji ni ujinga
Hao watoto wa kike, wanavuliana kanga
Kilio na tupeleke, kwa Mungu alie Mwanga
Ushoga jamani janga sasa linaziba mwanga
4. Tumekemea kudanga, tukikipiga kipyenga
Ushoga sasa mzinga, bora ukapigwa Panga
Hii imekuwa ndinga, tuombe pia kufunga
Ushoga jamani janga, sasa linaziba mwanga
5. Mwanga ukisha kuziba, hakuna ukionacho
Hapo tumepigwa roba, bora hata ya kichocho
Lia mama pia baba, fundisha bila kificho
Ushoga jamani janga sasa linaziba mwanga
6. Mtoto kajaa Pesa, hujui kapata wapi
Kumbe kabeba mkasa, nyuma amebaki kopi
Mnasubilia posa, kumbe ni Mvaa nepi
Ushoga jamani janga sasa linaziba mwanga
7. Tuwafundishe watoto, Tamaa kuziepuka
Wasijepata Majuto, waonekane vibaka
Watendaji beba wito, tutoe hiki kichaka
Ushoga jamani janga sasa linaziba mwanga
8.umewatuma watoto, chuo kuna mawakala
Hata shule za vidato, vibaraka watawala
Kila kona tumbo joto, hata kwenye daladala
Ushoga jamani janga sasa linaziba mwanga
9. Tizedi bila ushoga, hilo linawezekana
Kwa elimu tutaloga, watu wapate kupona
Vita hii tutapiga, bila hata konakona
Ushoga jamani janga sasa linaziba mwanga
10. Waletao dili hili, wameleta mchecheto
Na hiyo ndio dalili, mambo yamepamba moto
Wanaziteka akili, kwa kugawa maokoto
Ushoga jamani janga sasa linaziba mwanga
11. Unataka gari kali, kwa kugawa makalio
Bora ukose ugali, au ishi kwa Limao
Lakini usikubali, kuchukua wazo lao
Ushoga jamani janga sasa linaziba mwanga
12. Eti kuna wachungaji, viongozi na mashehe
Ushoga kwao ulaji, wamependa sitarehe
Wamkana muumbaji, Ee Mungu uwasamehe
Ushoga jamani janga sasa linaziba mwanga
13. Tuwakumbuke Sodoma, Tusisahau Gomora
Ushoga uliwalima, Mungu walipomkera
Hii zaidi ya homa, haiogopi na kora
Ushoga jamani janga sasa linaziba mwanga
14. Tutashinda mambo hayo, Mungu akituwezesha
Tutaokoa Mioyo, tukiomba na kukesha
Wote na tuseme ndiyo, pinga wanaopotosha
Ushoga jamani janga sasa linaziba mwanga
15. Mungu wetu Mungu wetu, twaomba usituache
Hili janga kama chatu, lisituletee cheche
Mwisho mwovu huyu Fyatu, utulinde tusimche
Tamati nimalizie, Mungu atusaidie