Azniv Protingas
JF-Expert Member
- Oct 29, 2020
- 335
- 554
Hivi karibuni katika eneo la Buguruni kumekuwa na unyang'anyi ambao hufanywa kwenye mida ya saa 10 mpaka saa 11 alfajiri. Wezi hao wamegawanyika katika makundi mawili; kuna ambao hutembea kwa vikundi na hubeba silaha kama visu na ambao hutumia bodaboda. Wanawavizia watu ambao wanaenda kazini asubuhi na kuwapora vile walivyokuwa navyo.
Cha ajabu ni kuwa kila nyumba inachangia pesa ya ulinzi shirikishi kwa kila mwezi lakini bado wezi wametawala kwenye maeneo hayo. Jukumu la ulinzi limewekwa juu ya hao ulinzi shirikishi lakini kazi yao hawaifanyi ipasavyo.
Kuna watu watasema kuwa tatizo ni ajira hakuna, lakini wezi wana mpaka pikipiki kwanini wasiitumie hiyo pikipiki kama kitega uchumi. Na kama kusoma mimi nasema hata form four hawajafika au hawajahitimu au wamefeli, sababu mtu aliesoma hawezi kuiba kishamba kwa kutumia visu na bisibisi, akatishia kutoa uhai wa mtu kwa sababu ya simu au pesa ambazo haendi kufanyia jambo la maana, kubwa wataenda kuvutia bangi na kununua pombe Kali, zikiisha pesa wataendelea kufanya tena wizi.
Pia soma Ulinzi shirikishi pia ni chanzo cha kuongezeka kama matukio ya wizi “panya road”