Ongezeko la mshahara kwa watumishi wa umma lisiwafanye muingie mkenge kukopa kwenye taasisi ndogo ndogo za kifedha

Ongezeko la mshahara kwa watumishi wa umma lisiwafanye muingie mkenge kukopa kwenye taasisi ndogo ndogo za kifedha

Joined
Jan 22, 2014
Posts
33
Reaction score
83
Asilimia 23.3 la ongezeko la mshahra kwa kima Cha chini si haba, japo baadhi wanakejeli ongezeko Hilo Ila ukweli ni kwamba kheri ya kitu kidogo kuliko kutokuongezewa kabisa.

Napenda kuwashauri watumishi wa umma ambao hupendelea kukopa katika taasisi za fadha kuwa makini na taasisi ndogo ndogo za kifedha mfano faidika, maboto na nyingine nyingi zenye kufanana na hizo.

Taasisi hizi Kwanza Zina riba kubwa ukilinganisha na kukopa katika bank moja kwa moja, lakini pia Kuna usumbufu mkubwa hasa pale unapohitaji kufanya malipo ya Deni lako kwa mkupuo, taasisi hizi husumbua kutoa salio la mkopo ili walipwe, lakini pia taasisi nyingine hazitoi salio la mkopo wako kabisa, na hubaki kukusumbua kila siku.

Pia taasisi nyingine zitakupa salio la mkopo wako lakini baada ya malipo hawatasitisha makato kwa wakati.

Ushauri wangu ni kwamba Kama utalazimika kukopa fadha Bora uende bank moja kwa moja, hawana usumbufu ambao umekuwa kero kubwa.
 
Huo ni ukatili mkubwa sana kwa wafanyakazi, ni sawa na mauaji ya Kimberly Rwanda.

Ikiwa TZ yenyewe inajiendesha kimikopo, Je Raia/wafanyakazi wake ni akina nani hasa hadi wasikope pesa [emoji848]

NB: Benki zote za TZ na mashirika mbali mbali ya mikopo ya wafanyakazi yanayotambulika kisheria, ni muda sasa kupiga pesa za Wafanyakazi, kazi kwenu [emoji87]
 
Wapi Bayport na Platinum! Salamu nyinhi ziwafikie huko mliko...!
 
Hakika BAYPORT,PLATNUM, ABC BANC ni matapeli narudia ni matapeli kwa msisitizo ni MA TA PE LI Hawa , yaani watumishi hange hange bora nenda bank moja kwa moja hujijuta ,ni matapeli hakuna riba kama hizo ni hatar riba kubwa mno MNO
 
Hakika BAYPORT, PLATNUM, ABC BANC ni matapeli narudia ni matapeli kwa msisitizo ni MA TA PE LI Hawa, yaani watumishi hange hange bora nenda bank moja kwa moja hujijuta ,ni matapeli hakuna riba kama hizo ni hatar riba kubwa mno MNO
Mi Kuna mtu alinifata Ni jirani tunafahamiana kapata kazi hapo platinum, et nikope, nikamwambia sawa, nikamuuliza riba kiasi gani akanitajia, nikamuuliza nikikopa milion 3 nilipe ndani ya miezi 10 kila mwezi ninatakiw kulipa sh ngapi? Akanijib laki 5 kila mwezi, yaani ndani ya miezi kumi nilipe mili 5 kwa kweli? Jamaa nikamwambia t riba yenu kubwa na staki Tena unishawishi kuhusu mikopo yenu, Ni wezi ukiingia kichwa kichwa lazima wakulime.
 
Back
Top Bottom