Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 199
- 322
Wimbi hili la uwekezaji wa Marekani barani Afrika linaongozwa na Shirika la Fedha la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (DFC), ambalo lilianzishwa mwaka 2019. Kwenye tovuti yake, shirika hilo linasema wazi kwamba kuanzishwa kwake ni kwa ajili ya “kuondoa ushawishi wa China katika maeneo ya kimkakati.”
Sababu ya kimsingi zaidi ya uwekezaji wa Marekani barani Afrika ni hitaji la maslahi yake ya kiuchumi. Afrika ina rasilimali nyingi muhimu za madini kama vile lithiamu, elementi adimu, kobalti, na tungsten. Madini haya si kama tu ni malighafi kuu kwa utengezaji wa vifaa vya kielektroniki kama vile simu za mkononi na kompyuta, bali pia ni muhimu kwa magari ya umeme, vituo vya data vya akili bandia, na hata silaha za kijeshi. Katika miaka ya hivi karibuni, Marekani imefanya juhudi kubwa ili kutafuta madini muhimu duniani kote, na Afrika ni moja ya maeneo muhimu.
Nchi za Afrika zinafahamu vizuri jambo hili. Mchumi wa Namibia Sepo Haihambo, ambaye alikuwa mtendaji mkuu wa Benki ya Kwanza ya Kitaifa ya nchi hiyo, alionya kwamba nchi za Afrika lazima zitetee maslahi yao zinapojadiliana na Marekani, na hazipaswi kutarajia faida yoyote. Anaona kuwa Afrika inapaswa kuanzisha utaratibu wenye haki katika kugawana uzalishaji na ubia, na kuzingatia kukusanya fedha ili kuanzisha mfuko huru wa kusaidia maendeleo ya jamii haswa elimu na afya. Pia alitoa wito wa usindikaji zaidi wa madini barani Afrika, badala ya kusafirisha malighafi nje ya nchi, ili Afrika iweze kudhibiti mnyororo wenye thamani zaidi.
Je, Marekani imerejesha ushawishi wake barani Afrika kutokana na kufufuka kwa uwekezaji? Uchambuzi uliochapishwa mwezi uliopita na Shirika la Mafunzo ya Mikakati na Kimataifa la Marekani (CSIS) unaonyesha kwamba, sera nyingi za Marekani zimechochea hisia za chuki kwa Waafrika dhidi ya Marekani. Wakati wa awamu ya kwanza ya rais wa Marekani Donald Trump, nafasi za ubalozi katika nchi kadhaa za Afrika zilibaki wazi kwa muda mrefu, na kuiacha Marekani bila uwakilishi wowote wa kidiplomasia katika eneo hilo. Wakati huo huo, marufuku ya usafiri iliwazuia raia wa nchi kadhaa za Afrika kwenda Marekani. Hali hii ilizidi kuwa mbaya katika awamu hii ya pili ya urais wa Trump. Kwanza “Ushuru Sawa” umekasirisha nchi nyingi za Afrika. Mwezi Juni, Marekani ilianzisha mafuruku makali zaidi ya kusafiri dhidi ya nchi za Afrika. Mwezi Agosti, Marekani ilitangaza amana za usalama wa visa za dola 15,000 za kimarekani kwa watalii na wasafiri wa biashara kutoka nchi kadhaa za Afrika. Mbali na hayo, ingawa viongozi wa nchi nyingi za Afrika wametoa ombi, lakini Marekani bado haijaongeza muda wa Sheria ya Ukuaji na Fursa ya Afrika (AGOA), ambayo imeisha tarehe 30 Septemba mwaka huu.
Ongezeko la uwekezaji kwa muda halimaanishi ongezeko la ushawishi. Afrika haitaki kubadilisha madini kuwa pesa taslimu. Wale wanaoheshimu uhuru wa Afrika na kushirikisha Afrika fursa za maendeleo ndio washirika wake wa kwel