Ongezeko la watoto wanaouza mifuko Sokoni ikiwamo Kariakoo linazidi kutia hofu

Duu
 
Alafu wote wanatoka kigoma sijui kuna shida gani?
 
Kinachofanya familia zao ziwaeuhusu watumikishwe, na kinachofanya wao wakubali kutumika ni hicho alichoandika mkuu hapo juu, yaani kukosekana kwa uhakika wa chakula.
 
Kuna watu wanawatumia hao watoto km miradi yao ya kujipatia kipato.!!
Waulize hiyo mifuko nani anawapa awauzie?
Wale ombaomba wanafanya km kazi usiku wanapeleka kipande kwa boss.!!

Yote hii inasababishwa na serikali ajira hakuna, hawawasaidii wananchi wao kujikomboa na umaskini.!! Maisha yamekuwa magumu.
 
Asa kama watoto ndio taifa la kesho huoni wako sahihi kufanya kazi saiv ili kesho ikifika wawe wametoboa
 
Kabla ya kuilaumu serikali kila mwananchi ajiulize anahusika vipi na ongezeko la watoto mitaani. Mitaa haizai watoto. Ni sisi tunawaleta duniani kwa starehe zetu. Asilimia kubwa ni watoto waliokosa malezi sahihi ya wazazi. Mtu anazaa watoto na kukimbia majukumu ya kuwalea.
 
Kwani Kuna shida watu kuuza mifuko sasa si bora hao kuliko wale wapuuzi wanaowaza waende kuiba wapi
Kinachoelezwa na mleta mada na kusikitisha wengi ni kwamba, watoto wengi wenye umri wa kwenda shule wameonekana wakiuza mifuko, tofauti na matarajio ya wengi kwamba walipaswa wawe shule, mkuu..
Asa kama watoto ndio taifa la kesho huoni wako sahihi kufanya kazi saiv ili kesho ikifika wawe wametoboa
Kwa bahati mbaya, kazi wanazofanya , wakuu wengi humu wamesema watoto wanatumikoshwa, yaani mwenye nafasi kubwa ya kutoboa ni hiyo anaewatumikisha. Wachache sana watatoboa Kwa kudra za mwenyezi Mungu huku wengi wao wakiendelea kuteseka na kuwa mzigo Kwa taifa.
 
Uko sahihi
 
Serikali tunailaumu Kwa kusababisha maisha magumu Kwa wazazi. Hakuna mzazi anaependa mtoto wake ateseke, asisome, awe chokoraa nk.
Lakini baadhi ya wazazi wanapitia changamoto wasizoweza kuzitatua mpaka wanaamua kukimbia familia.
 
Mkuu kuna watu wanamaisha magumu mnoo huezi soma tumbo likiwa halina uhakika wa chakula .hali ya maisha ndio inawafanya wawe mtaan
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…