Ongezeko la watoto wanaouza mifuko Sokoni ikiwamo Kariakoo linazidi kutia hofu

Ongezeko la watoto wanaouza mifuko Sokoni ikiwamo Kariakoo linazidi kutia hofu

Ndo maana Tanzani ina wananchi wa aina ya ajabu.

Watoto wengi sana wanaacha shule wako mitaani. Kuanzia garage za magari, mama lishe, boda boda, machinga.

Panya road, na wahalifu. Wengi sana Tanzania na ni watoto kabisa.
Bora hawa ambao wapo garage za magari wanapata ujuzi.
 
I see hii ni CHANGAMOTO kubwa sana kwa sasa,ukifika soko kuu Tabora,Soko kuu Arusha,Soko la Kilombero na hata Ngamiani Tanga ,hali ni hiyo hiyo

Baadhi niliobahatika kuwahoji walisema wanategemewa na familia zao..Nadhani ni wakati MUAFAKA sasa ,NGOs na Wanaharakati wa haki za watoto waangalie na huku
 
Nyie SI mnawatelekeza kwa madai kuwa watawatafuta ukubwani,Sasa madhara yake ndo haya inabdi waingie mtaani Ili waweze kujimudu. Muda ukifika wa wewe kumtafuta utakuta ni mraibu,shoga au kaathirika na mambo mengine
 
MAGUFULI aliposema ELIMU BURE watu walimuona chizi. ELIMU Bure ingesaidia kuondoa hizi vurugu.

Hawa CCM masalia wao wanataka wazazi wachangie gharama. Wazazi ni masikini hawana uhakika wa vipato. Unakuta mama ntilie kazalishwa na Bodaboda, au fundi ujenzi amabaye hana uhakika wa maisha yake mwenyewe, huyo mtoto ataenda shule gani.

Wanasiasa kwenye majukwaa wana sema ELIMU BURE, ukifika shuleni wanataka, michango ya chakula cha shule, sijui ukmatie mtoto bima ya afya, mara michango ya majengo, na madawati.

Wazazi wengu wanashindwa watoto wanarudi majumbani, na mwisho wa siku ndio hivyo wanaanza kujitafuta, na kujitafutia.
 
Back
Top Bottom