Kweli mkuu. Na dawa nyingi huharibika ktk hayo maduka hata kabla ya expiry date kwasabb ya poor storage.Hii inaenda sambamba na matumizi ya dawa. Uuzaji wa dawa kama biashara tena inayolipa ni changamoto. Siku zote mfanyabiashara anataka auze zaidi kupata faida kubwa.
Na FREMU nyingi zinaruhusu mwanga na joto jingi kuingia ndani ya duka. Mwanga na joto hubadilisha chemistry ya madawa mengi sana. By the time unaenda kununua ishaheuka kuwa sumu.
Kama unaweza kujisikilizia hata kwa siku 3 na ukapona kwa jitihada za Kinga ya mwili peke yake ni bema zaidi kuliko kununua dawa toka hivi viduka vya mitaani.
N.B. Mbali ya ukungwi pia mm ni mfamasia.