Onyango, Nyoni, Bocco na Mkude hawastahili kuichezea Simba. Muda umefika wa kuwaruhusu wakatafute maisha sehemu nyingine

Mi nafikiri uwezo wa simba ndio huo, kuokoteza sababu za kipuuzi kama hizi ni kujitekenya na kucheka mwenyewe tu, Simba amepigwa goli hizo hizo 3 kwa mkapa na Raja na wakiwepo wachezaji wote muhimu tena nyumbani inakuwaje muanze kuwalalamikia kina onyango? Kama mmepigwa kwenu kiroho safi mlitegemea kwenda na miujiza ya Musa kushinda ugenini? Kina onyango hao hao ndi mabeki wenu tegemeo wanaocheza kila siku leo hii mnawaangushia jumba bovu, wangefanya nini kipya mlichotegemea kule morocco? Acheni uzwazwa tengenezeni timu kule mnapoenda akuna kina horoya wala vipers tena ni ubora tu ndio utakufanya usonge mbele na sio kusonga ugali
 

Ukikutana na wanao jua ndio utaona madhaifu yako
 
Ndugu,
Maoni yako ni mazuri lakini hujayaleta katika wakati muafaka, hao wachezaji uliowataja ndiyo wameifikisha Simba hapa ilipo, Onyango kacheza mechi zote nguvu za Simba msimu hii sasa iweje leo tuanze kumkatisha tamaa wakati bado tunamuhitaji saana saana, kumbuka msimu ndiyo umefikia patamu
1. Robo fainali kombe la mabingwa Africa
2. Ligi bado hatujakata tamaa, tuna game na uto ambayo ndiyo itaamua hatma ijayo ya Simba
3. Bado tupo Azam federation

Haya mambo ni vizuri tukayaongea tukimaliza msimu, Kwangu mimi wachezaji wote wa Simba kwa sasa ni wazuri mno.
 
Wabakie hao wasiachwe.Simba ikileta wapya wanakua wabovu kuliko waliopo.
mfano:Kenedy Juma yupo vizuri wakaenda kumleta Oatara mbovu,una Mkude alafu wamemleta Sawa dogo mbovu nafuu ya Mkude.walimuacha Dunkan Nyoni na Chikwende wakaleta Okwa na Akpan😅😂
 
Hakuna kocha anaweza kupendekeza Nyoni aachwe! Hatuna local player wa kumzidi! Locally we have limited choices

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Wafuatao hawapaswi endelea
Bocco
Banda
Nyoni
Mkude
Okra
Okwa
Akpan
Mwenda
Sawadogo
Kibu

Utaona hapa tuna uwazi wa wachezaji wa Nje 5

Wafuatao wasiongezewe mikataba yao

Chama
Manura
Kapombe
Husein
Mzamiru
Onyango
Phiri


Simba isiwe sehemu ya kulea wachezaji, watu waje kucheza na kushinda

Madalali wanaiumiza Simba
 
Kwahiyo Sawadogo, Mwanuke, Gadiel, Mkude hawa wanastahili kuchezea Simba??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…