Onyo kwa mfumo wa kocha Masud Djuma wa Simba"

Onyo kwa mfumo wa kocha Masud Djuma wa Simba"

Hata striker nazo hazina makar ndugu ..kaz kukosa magoli ya waz tu
Ndemla anapiga mashuti huku amefumba macho
Ndemla angalia goli kwanza ndio upige.
Mpaka sasa umepiga mashuti zaidi ya kumi na tano na yote yamepita nje ya lango.
Ndemla angalia goli kwanza dogo wacha mapepe.

Kocha hebu mjaribu Gyani namba kumi au tisa, sasa ameonesha kiwango kizuri kwa kushambulia.
 
Yote kwa yote, timu ya Simba imeonesha uwezo mkubwa wa kiuchezaji chini ya Kocha mpya.

Tatizo lipo katika ushambuliaji na ufungaji magoli.
Wadau wa Simba tafadhali hebu tafuteni mfungaji wa kimataifa mwingine mwenye uwezo wa kucheza.

Ashike nafasi ya Bosi Emanueli Okwi.
Timu yetu ni nzuri, inamiliki mpira vizuri sana na imeanza kujenga pumzi.

Hebu mkiondoe Kirusi Kinachoitwa Okwi, na leteni mshambuliaji mwingine mwenye uwezo na shauku ya kuichezea Simba sc.

Mfukuzeni Okwi haraka sana hana maana hapo Clabuni.
Haiwezekana mnamsajiri mshambuliaji ambaye ndiye tumaini la kupachika magoli kwa bei kubwa halafu kila siku anashindia visingizio vya kukwepa kuchezea timu inayo mlipa.

Simba tunahitaji wafungaji na sio wazurulaji.
Simba kama munamuendekeza Okwi ataighalimu timu. Nafasi yake iko wazi haichezi hata kama amesajiriwa na Clabu sasa munamuweka wa nini ?

Si mutafute mshambuliaji mwingine mwenye muda wa kuichezea Simba..!

Au mnampenda Okwi kuliko mafanikio ya timu ?
Okwi huyu siyo yule tunaye mjua.

Okwi amekuwa tapeli wa kuihujumu timu ya Simba. Kama hamjui, basi huo ndio ukweli.
Naipenda Simba Daima.
 
Yule Gyan akicheza mbele ya goli anaonekana ana talent ila Kwasi ana kiwango cha Lipuli na Mbao kukamia mechi za Simba au Yanga ni mchezaji wa kawaida
 
tatizo la simba ni strike hata wangemleta gadiola atashindwa
 
Wee unadhani Azam ni timu ya kitoto? wewe unafikiri tu kila timu ikiingia uwanjani lazima ishinde? kwa taarifa yako kocha hana nafasi yoyote huwa ni symbol of unity kwenye timu tuu vingine ni longolongo tuu. Vipaji vya wachezaji ndio vina matter. Hakuna mchezaji aliyezalia kuwa striker, aliamua tuu siku moja kuwa awe striker lakini sii kwamba hawezi kucheza sehemu nyingine, ndio maana akina roberto carlos ni mabeki lakini kwenye list ya wafungaji bora walikuwepo. Brother mmewahiwa tuu na sii kwamba ni kocha , mbona wamekosa kosa nyinyi kwani na hizo kocha anahusika? mabao yote waliokosakosa hao mkia fc wangefunga ungeongea unachoongea sasa? Kati ya watu ambaop hula ujiko wa bure pale timu inaposhinda au lawama pale inaposhindwa ni kocha ila hawana lolote kwani hata timu ikienda bila kocha yoyote kama ina wachezaji wenye vipaji vya asili watashinda tuu.
Kocha hapimwi kwa kosakosa, hupimwa kwa ushindi. Kama ni kosakosa hata wakati wa Omog zilikuwapo. Lakini tatizo la Simba si kocha wala wachezaji. Tatizo la Simba ni Simba. Pale ni kama jikoni kwa Watanzania fulani wenye asili ya bara fulani. Kila mwanafamilia ana mkono wake kwenye chakula kinachopikwa. Mmoja akiongeza pilipili mwengine anaongeza kitunguu, mwengine kochimiri, mwengine giligilani ........! Fikiria ladha ya mwisho ya hicho chakula! Ndiyo Simba. Huyu anamwondoa Mayanja. Yule anamleta Masoud Juma. Huyu anasema Omog aondoke. Huyu anamkabidhi Masoud Juma ukocha Mkuu, unaomruhusu kuja na mfumo mpya katikati ya Ligi. Kwenye usajili ndiyo hivyohivyo. Huyu anadhani kunahitajika majina. Anayaleta. Yule anadhani kunahitajika wachezaji wa kigeni. Huyu anamleta Mavugo, yule anamleta Blagnon. Mwengine anasema wote hawafai. Analetwa Asamoah. Bado kuna mwengine a naona hafai. Mlete Kwasi. ....... Hao wote katika vipindi vifupivifupi. Kama chakula jikoni kwa ile jamii, timu hiyo itakuwaje?
 
Hivi okwi amecheza mechi ngapi na kila mwezi analipwa mshahara. Yuko wapi?
 
44f36104aaef2943ae8fd740de3361f2.jpg
 
Hivi okwi amecheza mechi ngapi na kila mwezi analipwa mshahara. Yuko wapi?
Mwache huyo sio mchezaji tu bali ana hisa pale Simba, na ni moja kati ya Wakurugenzi wa timu.
Kwa sasa anatimiza majukumu yake ya Ukurugenzi.
Akimaliza hizo kazi za Ukurugenzi atakuja kucheza ktk timu ya Simba.
Yeye ndiye anaye amua ni lini acheze na lini afanye kazi za kiofisi.
 
tatizo la simba wajuaji wengi. alikuwa anahitajika striker aneyejua kufunga na pesa ya mo ipo kamati ya usajili ikaleta ujuaji ikamleta beki kwasi halafu timu imefanya vibaya wa kwanza kutimuliwa ni omog. pamoja na mapungufu yake omog lakini hili kosa litawatafuna viongozi muda si mrefu kwa sababu sasa hivi jumba bovu linawaelemea golikipa mseja na kocha djuma. wakiisha hao itahamia kwa mabeki, baadae viungo mwisho wanachama watakuja kugundua shida ipo kwa uongozi hasa kamati ya usajili. kilichabki sasa viongozi wampange kwasi wao mshambuliaji wa kati ili afunge wao si walimsajili simba kwa sababu anajua kufunga.

timu inamiliki mpira kama barcelona lakini haina mshambuliaji makini wa kupasia nyavu sisi mashabiki wenye presha mtatuua mwaka huu.
 
Back
Top Bottom