ONYO LA USALAMA WA TAIFA: Bei ya Chakula ni Bomu Linalosubiri Kulipuka Tanzania

PESA ZIPO WAPI IN TANZANIA

Mkulima Paul Muema dunia imebadilika lazima tubadilike wakulima, pesa zipo ..

View: https://m.youtube.com/watch?v=4LGyhCgNQp8
Madalali wa mazao, soko, geopolitics, afya ya udongo, simu janja na taarifa za hali ya hewa, wateja wa mazao n.k
Dr. Kingori (Fe JSiaya)
 
U
Madalali ni Economic Insurgents(Waasi wa Kiuchumi). Hawa ni watu wanaovuruga usambazaji wa rasilimali na kudhoofisha utulivu wa nchi kwa makusudi ili kupata faida.

Katika lugha ya kijasusi tunaita mfumo huu "Value Chain Sabotage" Madalali nchini Tanzania wamejipenyeza katikati ya mzalishaji (mkulima) na mlaji na kutengeneza kizuizi ambacho kinanyonya damu ya pande zote mbili.

Tanzania ni nchi inayotegemea kilimo lakini madalali wanahakikisha kuwa kilimo hakitajirishi mkulima.

Mfumuko wa Bei wa Bandia. Dalali haongezi thamani yoyote kwenye bidhaa . Anachofanya ni kuhamisha gunia kutoka sehemu A kwenda B na kupandisha bei kwa 100%. Huu ni uporaji wa mchana kweupe unaopunguza nguvu ya ununuzi (purchasing power) ya mwananchi

Usalama wa Chakula (Food Security) ndio msingi wa amani yoyote.

Bei ya viazi, mahindi na maharage inapopaa kwa sababu ya magenge ya madalali, wananchi wanaanza kuichukia serikali yao. Wanaona serikali haina meno au inashirikiana na wanyonyaji. Hii ni kuni kavu inayoweza kuchochewa na maadui wa ndani au nje kuanzisha machafuko.

Uhalifu wa Mitaani.. Bei ya chakula inapopita uwezo wa masikini, vijana hukata tamaa na kujiingiza kwenye ujambazi na uporaji ili wale. Madalali wanatengeneza jeshi la watu wenye njaa ambao hawana cha kupoteza.

Udhoofishaji wa Sarafu na Mzunguko wa Fedha
Madalali wengi hufanya kazi kwenye (Shadow Economy). Hawalipi kodi stahiki, wanatumia Cash kukwepa mifumo ya kibenki na wanajilundikia utajiri ambao hautumiki kuzalisha viwanda. Badala yake wanatumia fedha hizo kuhonga maofisa wa serikali ili waendelee kulinda maslahi yao sokoni.

Kama nchi inataka kupona lazima madalali wapigwe vita kama magaidi wa kiuchumi. Haipaswi kuwa hiari ni lazima kwa usalama wa nchi

Digitization of Markets (Soko la Kidijitali).. Serikali ianzishe mfumo ambapo mkulima anaweza kuona bei ya soko ya Dar es Salaam akiwa Njombe na kuuza mazao yake moja kwa moja kwa wasambazaji wakuu bila kupitia madalali watano wa katikati.

Ujenzi wa Maghala na Miundombinu. Ikiwa mkulima ana sehemu salama ya kuhifadhi (Cold Storage)hatalazimika kuuza kwa bei ya hasara kwa dalali anayemvizia wakati mazao yanakaribia kuharibika.

Sheria ya Uhujumu Uchumi kwa Mapato ya Madalali. Mtu yeyote anayehodhi chakula au kupandisha bei kwa makusudi ili kutengeneza uhaba, anapaswa kushitakiwa kwa kosa la kuhujumu usalama wa taifa, si biashara tu.

Kuimarisha Vyama vya Ushirika (AMCOS). Wakulima wakiungana wanakuwa na nguvu ya pamoja dhidi ya madalali.

Taifa ambalo haliwezi kudhibiti bei ya chakula chake haliwezi kudhibiti mustakabali wake. Madalali ni maadui wa watu na ni jukumu la kila mdau wa usalama kuona kuwa mnyororo huu wa unyonyaji unakatwa.
Uko vzur sana!! Lakini nani atakusikiliza sasa? Kila mtu anatafuta upenyo wa kula ili ale vzur ashibe!! Sasahiv tunaishi kwa Law of the jungle!! Pia ni transition stage tuu, kwenda somewhere
 
Wakati korido za madaraka zikijaa mijadala ya kisiasa na miradi mikubwa, kuna adui wa kimyakimya anayesambaratisha amani ya nchi yetu… Njaa mitaani. Katika kipindi kifupi bidhaa za msingi kama viazi mbatata zimeshuhudia ongezeko la bei la hadi 200%.

Historia inatufundisha kuwa "Tumbo lenye njaa halina masikio." Serikali isipofumbua macho sasa tunatengeneza mazingira ya:

1. Mlipuko wa Uhalifu:

2. Hasira dhidi ya Mamlaka: Wananchi wanapohisi wamelelewa "peke yao" kwenye mateso, imani kwa serikali hupotea.

3. Machafuko ya Kiraia: Maandamano mengi duniani hayakuanza kwa kudai kura au Haki, yalianza kwa kudai MKATE.

Hatua za Haraka Zinazopaswa Kuchukuliwa

Serikali lazima iache kutazama siasa pekee na kuelekeza nguvu kwenye sahani ya mlaji:

• Uingiliaji wa NFRA: Hifadhi ya Chakula ya Taifa isihifadhi mahindi pekee. Lazima iingize sokoni akiba ya bidhaa mbadala kwa bei ya ruzuku ili kuvunja nguvu ya walanguzi.

• Kudhibiti Madalali: Ongezeko la bei mara nyingi halimfaidishi mkulima. Lazima kuwe na mfumo wa kudhibiti faidakwa bidhaa za msingi.(mi ningeshauri madalali wauliwe kwa mabomu maana wale sio binaadamu ni wanyama)

• Ruzuku ya Usafirishaji: Serikali itoe ruzuku ya mafuta kwa malori yanayosafirisha vyakula kutoka mikoani ili kupunguza gharama ya mwisho kwa mlaji.

• Kulinda Makundi Hatarishi: Kupitia TASAF kuanzisha mfumo wa "Voucher za Chakula" kwa familia maskini zaidi ili waweze kumudu viazi na unga.

Usalama wa Tanzania hauanzii mipakani na bunduki, unaanzia jikoni kwa mama lishe. Ni hatari sana kwa taifa kuendelea na "Business as Usual" wakati wananchi wanakosa mlo mmoja kwa siku. Serikali fanyeni kazi ya kulinda tumbo la mwananchi kabla hamjalazimika kulinda amani barabarani.

Ikiwa mapendekezo haya hayatatekelezwa serikali itajikuta ikitumia fedha nyingi zaidi kununua vifaa vya kuzuia ghasia (Riot Gear) kuliko ambavyo ingetumia kutoa ruzuku ya viazi. Chakula ni Haki si Anasa.
Prime minister yupo bize na chadema na guys guys
 
Mkuu mbona bado subilia mwakani kwani mwaka huu

Wakulima wameuziwa mbegu feki
Mbolea feki kwaiyo uzalishaji wa chakula utakuwa mdogo kupita mda wote yule waziri wa kilimo sijui alikuwa na lengo gani na nchi hii wakulima wanalia mbolea feki,.mbegu feki mkulima analima vizuri anapanda mazao yanaota ovyo ovyo tu anaweka mbolewa wiki moja mmea unaanza poteza nuru unaanza kuoza

Watu walikuwa wanajali maslahi yao si watanzania
 
Madalali ni Economic Insurgents(Waasi wa Kiuchumi). Hawa ni watu wanaovuruga usambazaji wa rasilimali na kudhoofisha utulivu wa nchi kwa makusudi ili kupata faida.

Katika lugha ya kijasusi tunaita mfumo huu "Value Chain Sabotage" Madalali nchini Tanzania wamejipenyeza katikati ya mzalishaji (mkulima) na mlaji na kutengeneza kizuizi ambacho kinanyonya damu ya pande zote mbili.

Tanzania ni nchi inayotegemea kilimo lakini madalali wanahakikisha kuwa kilimo hakitajirishi mkulima.

Mfumuko wa Bei wa Bandia. Dalali haongezi thamani yoyote kwenye bidhaa . Anachofanya ni kuhamisha gunia kutoka sehemu A kwenda B na kupandisha bei kwa 100%. Huu ni uporaji wa mchana kweupe unaopunguza nguvu ya ununuzi (purchasing power) ya mwananchi

Usalama wa Chakula (Food Security) ndio msingi wa amani yoyote.

Bei ya viazi, mahindi na maharage inapopaa kwa sababu ya magenge ya madalali, wananchi wanaanza kuichukia serikali yao. Wanaona serikali haina meno au inashirikiana na wanyonyaji. Hii ni kuni kavu inayoweza kuchochewa na maadui wa ndani au nje kuanzisha machafuko.

Uhalifu wa Mitaani.. Bei ya chakula inapopita uwezo wa masikini, vijana hukata tamaa na kujiingiza kwenye ujambazi na uporaji ili wale. Madalali wanatengeneza jeshi la watu wenye njaa ambao hawana cha kupoteza.

Udhoofishaji wa Sarafu na Mzunguko wa Fedha
Madalali wengi hufanya kazi kwenye (Shadow Economy). Hawalipi kodi stahiki, wanatumia Cash kukwepa mifumo ya kibenki na wanajilundikia utajiri ambao hautumiki kuzalisha viwanda. Badala yake wanatumia fedha hizo kuhonga maofisa wa serikali ili waendelee kulinda maslahi yao sokoni.

Kama nchi inataka kupona lazima madalali wapigwe vita kama magaidi wa kiuchumi. Haipaswi kuwa hiari ni lazima kwa usalama wa nchi

Digitization of Markets (Soko la Kidijitali).. Serikali ianzishe mfumo ambapo mkulima anaweza kuona bei ya soko ya Dar es Salaam akiwa Njombe na kuuza mazao yake moja kwa moja kwa wasambazaji wakuu bila kupitia madalali watano wa katikati.

Ujenzi wa Maghala na Miundombinu. Ikiwa mkulima ana sehemu salama ya kuhifadhi (Cold Storage)hatalazimika kuuza kwa bei ya hasara kwa dalali anayemvizia wakati mazao yanakaribia kuharibika.

Sheria ya Uhujumu Uchumi kwa Mapato ya Madalali. Mtu yeyote anayehodhi chakula au kupandisha bei kwa makusudi ili kutengeneza uhaba, anapaswa kushitakiwa kwa kosa la kuhujumu usalama wa taifa, si biashara tu.

Kuimarisha Vyama vya Ushirika (AMCOS). Wakulima wakiungana wanakuwa na nguvu ya pamoja dhidi ya madalali.

Taifa ambalo haliwezi kudhibiti bei ya chakula chake haliwezi kudhibiti mustakabali wake. Madalali ni maadui wa watu na ni jukumu la kila mdau wa usalama kuona kuwa mnyororo huu wa unyonyaji unakatwa.
Akili hizi ndio zinahitajika TISS kwenye idara ya uchumi sio uchawa tu.
 
Umeandika kwa akili kubwa na uzalendo wa hali ya juu sana.
 
Back
Top Bottom