Onyo: Udini ukifanikiwa, hata majeshi yatagawika na wanaotegemea majeshi, nao itakula kwao

Onyo: Udini ukifanikiwa, hata majeshi yatagawika na wanaotegemea majeshi, nao itakula kwao

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,828
Reaction score
165,667
Huu ndio ukweli mchungu kwa mtu yeyote mwenye kuona mbali.

Majeshi yakigawika kwa misingi ya imani za kidini, hayawezi kuwa loyal kwa mujibu wa viapo vyao na itawaathiri hata wale wanaotegemea dola iwaweka madarakani.

Mtatoa order, ila askari kabla hajatekeleza hio order, atajiuliza kwanza yeye ni wa dini gani na ni mtu wa dini gani ataethirika na utekelezaji wa hiyo order.

Mwisho wa siku, hata walinzi wa kuwalinda, mtataka wawe wa dini zenu.

Mpaka hapo, kutakuwa na nchi? Nani atakuwa usalama?

Endeleeni kuhubiri udini muone kama na nyie mtabaki salama

Kuna wakati unakuja tutawakumbusha huu msemo:
"Majuto ni mjukuu."
 
Udini,ukabila na umimi kwa wapenda madaraka walioshindwa kujua kama CCM wanaona ndio uwezo wa kisiasa kwao.
 
Huu ndio ukweli mchungu kwa mtu yeyote mwenye kuona mbali.

Majeshi yakigawika kwa misingi ya imani za kidini, hayawezi kuwa loyal kwa mujibu wa viapo vyao na itawaathiri hata wale wanaotegemea dola iwaweka madarakani.

Mtatoa order, ila askari kabla hajatekeleza hio order, atajiuliza kwanza yeye ni wa dini gani na ni mtu wa dini gani ataethirika na utekelezaji wa hiyo order.

Mwisho wa siku, hata walinzi wa kuwalinda, mtataka wawe wa dini zenu.

Mpaka hapo, kutakuwa na nchi? Nani atakuwa usalama?

Endeleeni kuhubiri udini muone kama na nyie mtabaki salama

Kuna wakati unakuja tutawakumbusha huu msemo:
"Majuto ni mjukuu."
Wanao mshauri Samia either sio wataalamu wa mipango ya kimkakati au ni Wajinga kabisa.

Akitaka Udini inabidi atoe vyeo vyote serikalini kwa misingi ya Udini kama yuko serious, and above all akifika hapo tateleta Silaha wasiotaka kuisikia ambayo ni "Muungano" tutamwambia arudi Zanzibar akawa Rais wao huko kwa waislamu wote
 
Hakuna jeshi linaloweza kugawanyika kwasababu ya udini usichokijua jeshi lenyewe pia ni dini

Nyumbu kweli ni chakula cha mamba.
 
Jana kwa masikio na macho yangu nilimsikia na pia kumuona kiongozi mkuu anayehamasisha huo udini. Ni aibu kuona mtu wa hadhi yake akiamini kwenye ujinga kama huu.
 
Yaani watu wanakuchalenge kwa hoja! Wanakuambia simama kwenye haki! Acha dhuluma, acha kuteka, kutesa na kuua wajosoaji wako! Acha kuwaweka wapinzani wako magerezani kwa makosa ya uongo, acha kuuza hovyo raslimali za nchi, nk.

Badala ya kuwasikiliza na kubadilika!! Eti unajitokeza hadharani na kuwafokea/ kuwachamba kwa kuwaambia wanakushambulia hivyo kwa sababu ya dini yako!! Kwa hiyo dini yako ndiyo inakutuma kukandamiza haki za raia!! Au ni matatizo ya uelewa wa mtu!
 
Serikali udini umeshamili balaa,kama sio wa dini yao unabaguliwa
 
CCM watajinyonga wenyewe. Ni suala la muda tu
 
Back
Top Bottom