Onyo:urembo unaposababisha upofu

Onyo:urembo unaposababisha upofu

Bishanga

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2008
Posts
15,321
Reaction score
10,075
yametokea kinondoni,mwanamke kenda kubandika nyusi,msusi kwa ubahili wake badala ya kutumia gundi yake maalum kambandikia superglue,mama kilio,kwenda ccbrt kafanyiwa operesheni ya kutoa gundi,kumbe gundi ilishaharibu macho,kawa kipofu.
Angalizo: kinamama chungeni sana mnapoamua kuongeza makalio,kutia mkorogo,kuongeza nyusi,kurefusha kucha.....na mengine sisemi ni ya siri......
 
halafu kuna wanawake wana ujasiri wa kipuuzi, kubandika nyusi na kuvaa contact lens kwa ajili ya urembo
 
Akabandike na macho ya spea sasa...
 
Mtu unajiuliza kinachowafanya dada zetu wajihangaishe kiasi hicho... Unakuta mtu ni mzuri tu lkn kajichakachua weee hadi kawa kama katuni.
 
halafu kuna wanawake wana ujasiri wa kipuuzi, kubandika nyusi na kuvaa contact lens kwa ajili ya urembo

kuvaa contact lens na kuvaa tampons ni vitu ambavyo naona ni majasiri ndio wanaweza kufanya hivyo,mie nawaheshimu sana mie siwezi walahi.....
 
Duh! Lazma watu wajikubali vile walivyo jameni! Mwee! Afu hata huyo alikuwa anamwekea hzo nyusi akamwone mzuri hatakaa amuone tena! Jamani wadada tujikubali vile tulivyo tusalimike!
 
akapandike macho ya mchina! nasikia yapo!

yametokea kinondoni,mwanamke kenda kubandika nyusi,msusi kwa ubahili wake badala ya kutumia gundi yake maalum kambandikia superglue,mama kilio,kwenda ccbrt kafanyiwa operesheni ya kutoa gundi,kumbe gundi ilishaharibu macho,kawa kipofu.
Angalizo: kinamama chungeni sana mnapoamua kuongeza makalio,kutia mkorogo,kuongeza nyusi,kurefusha kucha.....na mengine sisemi ni ya siri......
 
We bishanga unatulisha matango pori tu hapa!! Kabandika nyusi na superglue?? mmmhhh!!
 
Mtu unajiuliza kinachowafanya dada zetu wajihangaishe kiasi hicho... Unakuta mtu ni mzuri tu lkn kajichakachua weee hadi kawa kama katuni.
unajua wadada wanajikoki hivo kwa sababu ya wanaume, maana wanaume siku hiz kuwapata ni kwa manati
 
jamani wanawake wenzangu mbona tu wazuri kwa jinsi tulivoumbwa madude yote hayo ya nini!
 
kuvaa contact lens na kuvaa tampons ni vitu ambavyo naona ni majasiri ndio wanaweza kufanya hivyo,mie nawaheshimu sana mie siwezi walahi.....

hao wa tampons tuliwasahau. Kuna wanawake wana mioyo! Loh!
 
hapana dah naamini kila mwanamke ameumbwa na uzuri wake kwa jinsi ya ajabu kama maisha yangekuwa na njia moja tungeogopa wengine
urembo chauro. Sasa urembo unapogeuka urimbo na shughuli inapoanza!
 
Itakuwa alikuwa anabandika kope,ni urembo mzuri tu wanawake dunia nzima wanabandika tatizo ni sisi wabongo ni wataalam wa kuchakachua kila kitu,amekosa gundi yake special kaamua kutumia super glue kwenye jicho la mwanadamu,Mungu amsaidie tu aweze kupona.
 
Kitu ambacho akina dada kinatusumbua ni kushindwa jisoma... ni kweli kua wanawake wengine ni wazuri saana kuliko wengine, BUT ladies believe me you kila mwanamke ana uzuri wake... Kikubwa hata kama kweli siio mzuri cheza na Mvuto... Mwanamke makini na ukiamua huwezi kosa mvuto; na mvuto ule wakupendeza ni minimal artificiality.... Hebu fikiri mdada una nywele za bandia (which in most cases tunashindwa wengi kukwepa) haya basi kucha - bandia, Kope - bandia, macho - contacts, jamani..... Dah.

Kutafuta mvuto mtu atafute her best feature mwilini, dress the right clothes... Use the right make up, tafuta a perfect hair sytle inaendana na sura yako na inayokuongezea mvuto... Try as much as possible to be asilimia kubwa saana "YOU"
 
Kwa nini mshindwe nywele za bandia?

Anaeweka nywele za bandia hana authority ya kumwambia mtu asiweke kucha au kope za bandia. Vyote ni artificial
 
I do see nothing wrong with contact lenses. Hasa kwa sisi tunaovaa miwani 24/7 wakati mwingine mtu unachoka.

halafu kuna wanawake wana ujasiri wa kipuuzi, kubandika nyusi na kuvaa contact lens kwa ajili ya urembo
 
Back
Top Bottom