Oooh Gosh. kwa nini mnakuwa hivi jamani.....?

Oooh Gosh. kwa nini mnakuwa hivi jamani.....?

jamani kuna rafiki yangu ana boyfriend wake. huyu bf alikokua anakaa mwanzo alimuonyesha lakini baadae alikuja kuhama alipohamia hakumuonyesha. na kila wakikutana anasema hana pesa anataka yule mwanamke alipie vinywaji. kuhusu mawasiliano kila mara yeye ni hana credit akimpigie simu anapokea baada ya muda anamwambie nipigie baadae. na sababu ya kutomwonyesha kwake ni kuwa anadai huyo msichana hajakua kiakili so siku akikua atamwonyesha. kwake kutamka neno i luv u ni msamiati.
mi nachouliza je huyu kaka anampenda kweli huyu dada?
 
FirstLady1!!!hebu try to check out na upande wa pili wa shilingi!!usije kutoa lawama kabla hujajua mr anasemaje!!huenda ukimsikia mr. utamfukuza hata huyo friend wako,kuwa mvumilivu kidogo kabla ya kutumwagia lawama!!
my dear kwa lolote ambalo mke/mume kafanya, si haki wala si ustaarabu kumpiga mwenzako, kumfukuza kwenye nyumba yenu, tena si mke /mume tu hasa watoto ambao hata hawajui chanzo cha mzozo wenu, kwa ufupi huyo mwanamume anamatatizo makubwa, hayo ya kupekuliwa na mume kayafanya kama mwanzo wa sentensi tu ili apate pa kuanzia kumfukuza huyo mke, lakini laiti tungeingia moyoni mwake tungegundua kuwa mapenzi yalishaisha kitambo imebaki mazoea tu na yale mambo ya kiapo cha 'mpaka kifo kitutenganishe' I WISH NINGEKUWA NA UWEZO WA KUBADILI CLAUSE HII isomeke 'MPAKA MAPENZI YATAKAPOFIKA MWISHO"
 
FL1,

Hii issue ni inauma sana n a inakela mno! Ufikapo hm na kujaribu kulonga na mume wa huyo dada just kuwa makini sana maana huyo bwana akili zake ziko fyatu kimtindo, na ujaribu kuchunguza kama jamaa kaisha pata chupa zake mmoja mbili hivi just dont go asije kuharibia usingizi wako bureeeee!

Je huyo baba anafanya kazi?

kwanza topic lazi uianzishe na iwe ime base kwa watoto kwanza then issue ya yeye na mkewe ndio utaichomekea hapo kati kati ya maongezi.

Na ulisema muda flani ati rafikio huyo anataka kwenda Police? its oky lakini je ustawi wa jamii nako alisha kwendaaa kujieleza hayo matatizo? alafu kuna wakina mama wengine huenda hata kushitaki kwa mabosi wa waume zao kama wameleteana noma home.

thanks huo mstari wa juu imebidi nicheke kwanza
alikuwa amekunywa na ndio zake ulevi kwake ni sawa na chakula tatu mala tatu
ana elimu ya juu kabisa ni mfanyakazi wa serikalini sekta muhimu ..
Labda pia mama itabidi niongee nae juu ya ustawi wa jamii
thanks for the advice jethro
 
Thanks Bujibuji je nini cha kumsaidia huyu dada kafunga ndoa halali ua Kikristo

FL1,
Pole kwa yote.
Ndoa ni yake, je amejaribu kurekebisha na mumewe? Basi aende kwa msimazi wa ndoa yao...
 
...mid-life crisis,

Tatizo la jamii zetu za kiafrika mwanaume unatakiwa 24/7 upambane na matatizo yako mwenyewe kisaikolojia. Hakuna kulia lia, kushtaki wala kulalamika maisha yanapokukalia kooni...

Ukijumlisha hayo na manung'uniko na lawama za kila siku toka kwa mama watoto unajikuta siku unaripukwa kama hivyo.

Namlaumu huyo mheshimiwa kukosa busara kiasi cha kuwakurupusha wanafamilia wote usiku wa manane, lakini pia namlaumu mama mwenye nyumba kukosa busara ya kusubiria mzee mwenye nyumba apoe hasira ndipo aanze kuongea nae kiutu uzima.

Wakati umefika kuanzishwe vituo kwa wanandoa kwenda kupata counselling, maana kuna matatizo mengine yanachangiwa kwa kiwango kikubwa na umasikini tulionao + pressure za kazi na majukumu ya familia.

Kaka unayosema ni kweli kwa kiasi kikubwa.
 
First Lady,
Usikubali kukaa na mke wa mtu kwa siku mbili mfululuzo unaweza kushtakiwa kwa kuvuruga unyumba wa watu ohoo sauri yako.Tafadhali mpeleke kwa mjumbe ili mumewe aitwe ijulikana tatizo ni nini ? inawezekana kuna mambo mengine kakuficha labda kamyima mume unyumba.
 
baadhi ya kaka zetu wakimchoka mwanamke wanabadilika na kua vitu vya ajabu kabisa visivyo na chembe ya huruma.inasikitisha.
 
Ndoa ndoano.
Wanawake huwa wanakosea,
wanakuwa na haraka sana ya kuolewa na kusahau kumchunguza vyema mumewe mtarajiwa.
Hata akigundua tabia mbaya za huyo mwanamume husema moyoni mwake kuwa atamrekebisha, kitu ambacho hata wazazi wa mwanaume wameshindwa kuzirekebisha tabia mbaya hizo.
matokeo yake ni kwamba baada ya raha za muda mfupi wa ndoa mateso na dhuluma huanza.
Ila familia bora ni ile yenye hofu ya Mungu.
mkiwa mnatafuta watu wa kuwaoeni, tafuteni wale ambao wanamtegemea Mungu na kufuata neno lake.
........Bujibuji wanaume mnabadilika nyie kama kinyonga vile, hata ukimchunguza mwanaume miaka 10 eti ndio uolewe ni kazi bure. Miezi 6 tu inatosha kujua tabia ya mpenzi wako kama muda mwingi mpo pamoja.

.......FL1 pole kwa huyo rafiki yako, je huyo mdada anafanya kazi au? Kama mfanyakazi na kipato kinamtosheleza kuhudumia watoto wake ajiondokee tu hapo maana huyo mwanaume katili hana utu wa kibinadamu.
 
........Bujibuji wanaume mnabadilika nyie kama kinyonga vile, hata ukimchunguza mwanaume miaka 10 eti ndio uolewe ni kazi bure. Miezi 6 tu inatosha kujua tabia ya mpenzi wako kama muda mwingi mpo pamoja.

Sasa kama wanaume wanabadilika kama vinyonga mtajuaje tabia zao ktk muda wa miezi 6 tu achilia mbali kujua tabia zao hata ipite miaka?
 
Sasa kama wanaume wanabadilika kama vinyonga mtajuaje tabia zao ktk muda wa miezi 6 tu achilia mbali kujua tabia zao hata ipite miaka?

.......Kujua tabia ya mtu kazi sana, kama umeridhika na mtu jitose tu kwenye ndoa mkishindwana kila mtu kivyake.
 
.......Kujua tabia ya mtu kazi sana, kama umeridhika na mtu jitose tu kwenye ndoa mkishindwana kila mtu kivyake.

See, that's why I like you Pretty. You have good common sense. Na ulichosema ni kweli kabisa. Kujua tabia ya mtu ni kazi sana.
 
Yale yaleee...sijui kama yataisha anytime soon FL1! Pole mkaribishe mwanamke mwenzio mpe chakula na mavazi ili sipungukiwe kitu kwa sasa na Mungu atakuongezea apo ulipopunguza.
Do it with caution though maana hii ilisha wa cost wenzio sana.Kuna mama mmoja miaka mingi kidogo alimhifadhi shoga yake aliyekuwa na matatizo kama haya. Hifadhi hiyo ilidumu kipindi cha kutosha.Kumbe baada y muda chemistry baina ya mkimbizi na baba mwenye nyumba zikaendana..... you can guess the end of the story.....
 
......Da WoS hii kali maana hadi nimecheka, mhhhhhhhh!!Mbona ilikuwa kali mtu unapewa hifadhi na rafiki hadi unaamua kumchukulia mwenzio mumeo.
 
Do it with caution though maana hii ilisha wa cost wenzio sana.Kuna mama mmoja miaka mingi kidogo alimhifadhi shoga yake aliyekuwa na matatizo kama haya. Hifadhi hiyo ilidumu kipindi cha kutosha.Kumbe baada y muda chemistry baina ya mkimbizi na baba mwenye nyumba zikaendana..... you can guess the end of the story.....
Kwavile mama mwenye nyumba alionesha kumjali rafiki kwa chakula,mavazi na hifadhi basi hata baba mwenye nyumba huenda aliona si vema kumtenga mkewe ndo maana naye akaona ni vema akasaidia kwa kiasi flani ili kudumisha ushirikiano.
 
Do it with caution though maana hii ilisha wa cost wenzio sana.Kuna mama mmoja miaka mingi kidogo alimhifadhi shoga yake aliyekuwa na matatizo kama haya. Hifadhi hiyo ilidumu kipindi cha kutosha.Kumbe baada y muda chemistry baina ya mkimbizi na baba mwenye nyumba zikaendana..... you can guess the end of the story.....

hahaha WOS usinipe homa ya moyo faza house hayupo 😉
 
Hivi mapenzi huwa yanaisha kabisa ? yanapungua au yanakuwaje ??
Hivi pale mtu anapoamua kurudi na kukwambia sorry ni Ibilisi alinipitia naomba turudiane wife/husband ni shetani ndo anakuwa ameamua kuyaruddisha?😉
Nimetoa report kwa Mtendaji wa mtaa mama wa watu leo ataondoka kwangu lakini hatorudi kwa mme kwani jana alijaribu kwenda na watu wa church wote waliambulia kufukuzwa bila kusikilizwa ..maajabu ya duniani..
Nimeongea na Mme wa mama yule ..alichoniambia kamchoka mwanamama huyo aende anakojua na wanae..yeye ameamua kuoa na wanawake wako wengi..hajanipa chanzo hasa cha kumshushia wife ile kosovo na chechinia ..
Mshangao!!!
 
Ni mwanamama mwenye watoto watatu 10,yrs 7yrs and 3years
Jana husband wake kamshushia kipigo cha mbwa mwizi na kumfukuza kwake saa saba usiku na wanae na kukimbilia kwangu kisa eti mwanamke anamfata fata sana hataki mkewe aulizie maendeleo ya familia ,hataki mkewe aguse simu yake na pia hataki mkewe amuulize kama hakurudi home alikuwa wapi na kwa nini amechelewa .....Hii ndio maana ya ndoa?
Mie kama mwanamke kwanini machozi yasinitoke .nimewaza na ,nimeumia sana juu ya hili labda inaweza kutokea kwangu pia..
Wanaume kwa nini mnakuwa wakatili hivi??
Hamuoni huruma juu ya watotokwa watoto wadogo wanaohitaji mwongozo wa wazazi ?
kwa nini kuwatesa watoto usiku wa manane na kuwaamsha kama wakimbizi ndani ya nyumba yao ?
Hali hii ya manyanyaso itaisha lini ??

mi binafsi nilipomkataa mtu mapema niliambiwa maneno mengi sana humu tena na nyinyi wanawake. sina huruma, mbinafsi, n.k. so mnataka hadi yafikie hapo ndio mjue hakuna mapenzi kati yenu? wanawake ni wa ajabu sana. ukiulizia historia yao utakuta huyo mwanamke alikuwa analazimisha mapenzi. haiwezi kufikia hapo bila sababu yenye chimbuko. hiyo biashara ya kuolewa ili kutoa nuksi, hiyo biashara ya kuolewa ili kujisitiri itawatokea puani. ila pole zake huyo dada
 
Hivi mapenzi huwa yanaisha kabisa ? yanapungua au yanakuwaje ??
Hivi pale mtu anapoamua kurudi na kukwambia sorry ni Ibilisi alinipitia naomba turudiane wife/husband ni shetani ndo anakuwa ameamua kuyaruddisha?😉
Nimetoa report kwa Mtendaji wa mtaa mama wa watu leo ataondoka kwangu lakini hatorudi kwa mme kwani jana alijaribu kwenda na watu wa church wote waliambulia kufukuzwa bila kusikilizwa ..maajabu ya duniani..
Nimeongea na Mme wa mama yule ..alichoniambia kamchoka mwanamama huyo aende anakojua na wanae..yeye ameamua kuoa na wanawake wako wengi..hajanipa chanzo hasa cha kumshushia wife ile kosovo na chechinia ..
Mshangao!!!

Duuuuuh FL1,
Kwanza pole sana kwa kujitutumua na kumtokea huyo Dingi,

Swala la mapenzi kuisha au kuchoka kwakweli hapo huwa kuna jambo limewapelekea hao wapenzi na kusababisha hiyo hali ya kuchokana au kuisha lakini hivi hivi tu sidhani,

Mwaweza mkawa bado mnapendana tu ila tabia au vitimbi vikawa ni vigumu kwa mwenzio kuendelea nawe, iyo hali yakufanya tu wewe useme its oky let me stand aside and see,

Mwingien utakuta kila ukihitaji tendo la ndoa kachoka au hufanya game one hata 5mins hazijaisha kamaliza sasa hapo kweli kileleni hamjafika unategemea upande mmoja utaridhika kweli hapana lazima tu kutakuwa na maswali mengi tu hapo either huoni mvuto kwa mwenzio kwasababu fulani fulani, kwani mwenzio akija anakulukia tu jamani haya mambo yana hitaji uvumilivu sana kwa sie tulio kwa ndoa twayajua sana naniko makini sna na mke wangu kwa hili swala i dnt joke around at that Pitch na kingine msije fanya hii ndio maji ya kunywa au chai au soda eeeehhh.

Ivi hilo kundi la watu wa church wao hawakujipanga kwanza? walikuja as if wanenda kuhubiri pale jamani? obvious yule bwana angewatimu hamuwezi kwenda kuamua ugonvi au kupatanisha watu wa 5.

Ila huyo bwana atakapo kaaa na kutulia atakua juta sana, Pia jamani kuna jambo mmoja hapa napenda kuligusia, isije ikawa dada mmoja ya hao anotembea nao kamwendea huyo mzee kwa mtaalamu awe anajivinjari nae jamani kumbukeni huku mijini watu wanaishi kwa style ya ajabu sana. kuna nguvu za giza sana kwa wale wanaojua ni nini nakiongelea wananipata vyema.

Wanaume wenzangu jichunguzeni sana waweza ukawa unachezwa kumbukeni kusali sana japo hata mara mbili kwa week, maana izo shamba za njeee mmmhh zinajua kazi zao vyema hazi lazi damu, ukicheza kidogo nao kidogo tu ndoa yako iko matatani.

Back
Top Bottom