Kutokuwepo uelewa wa namna ya kufungua akaunti ya kufanya malipo mbalimbali ya Halmashauri nchini wa Tausi Portal ni chanzo cha maafisa mapato kujinufaisha. Huenda wizi huu unafanyika katika Halmashauri zote nchini. Katika oparesheni inayoendelea ya kukusanya madeni inayoendelea kwa wafanyabiashara Manispaa ya Morogoro. Maafisa mapato wakifika eneo la biashara wanakuomba leseni kama hauna au imeisha muda wake wanakutoa dukani nakufunga duka kwa utepe maalumu kama ule wa masanduku ya kura. Watakwambia lipia Kodi ya miezi husika na faini ya laki moja wakufungulie. Au kama huna Kwa muda huo wanakwambia nenda ofisi za mapato Manispaa. Ukiwapatia hapo dukani watakuandika jina na kuchukua pesa taslimu pamoja na hiyo faini na kuchukua particular zako kama TIN namba ili wakienda ofisini wakufingulie akaunti au watatuma taarifa zako hizo ofisini kwao. Kama utaenda ofisini watakuambia acha taarifa na pesa pamoja na hiyo laki moja ya faini. Kisingizio ili uache pesa ni mtandao wa Tausi unasumbua. Ukishaacha pesa baadae utafunguliwa akaunti na watakuomba OTP kukamilisha kufungua akaunti namba. Baadae utapokea msg ya GePG kukutaarifu kuwa malipo yako yamekamilika. Lakini kiasi cha malipo itakuwa ni malipo ya mwaka mmoja husika wa sasa. Malipo ya miaka ya nyuma hawataingiza wala Ile faini ya laki moja. Ukifuatilia watakujibu mtandao kwa ajili ya malipo ya nyuma au Ile faini ya laki moja unasumbua endelea kusubiria tu. Pamoja na uwepo wa mawakala wa pesa, pale ofisini kwao droo za meza zao utakuta zimejaa pesa zilizofungwa kwenye karatasi na majina ya wateja ikiwa ni malipo ya leseni na faini. Takukuru fikeni mjione hali hiyo.