Oparesheni agua leseni inayoendelea Manispaa ya Morogoro. Faini Sh 100,000 kwa wasio na leseni inaingia mifukoni mwa maafisa mapato. Uhakika huu hapa.

Oparesheni agua leseni inayoendelea Manispaa ya Morogoro. Faini Sh 100,000 kwa wasio na leseni inaingia mifukoni mwa maafisa mapato. Uhakika huu hapa.

Tozo

Senior Member
Joined
Aug 23, 2021
Posts
101
Reaction score
202
Kutokuwepo uelewa wa namna ya kufungua akaunti ya kufanya malipo mbalimbali ya Halmashauri nchini wa Tausi Portal ni chanzo cha maafisa mapato kujinufaisha. Huenda wizi huu unafanyika katika Halmashauri zote nchini. Katika oparesheni inayoendelea ya kukusanya madeni inayoendelea kwa wafanyabiashara Manispaa ya Morogoro. Maafisa mapato wakifika eneo la biashara wanakuomba leseni kama hauna au imeisha muda wake wanakutoa dukani nakufunga duka kwa utepe maalumu kama ule wa masanduku ya kura. Watakwambia lipia Kodi ya miezi husika na faini ya laki moja wakufungulie. Au kama huna Kwa muda huo wanakwambia nenda ofisi za mapato Manispaa. Ukiwapatia hapo dukani watakuandika jina na kuchukua pesa taslimu pamoja na hiyo faini na kuchukua particular zako kama TIN namba ili wakienda ofisini wakufingulie akaunti au watatuma taarifa zako hizo ofisini kwao. Kama utaenda ofisini watakuambia acha taarifa na pesa pamoja na hiyo laki moja ya faini. Kisingizio ili uache pesa ni mtandao wa Tausi unasumbua. Ukishaacha pesa baadae utafunguliwa akaunti na watakuomba OTP kukamilisha kufungua akaunti namba. Baadae utapokea msg ya GePG kukutaarifu kuwa malipo yako yamekamilika. Lakini kiasi cha malipo itakuwa ni malipo ya mwaka mmoja husika wa sasa. Malipo ya miaka ya nyuma hawataingiza wala Ile faini ya laki moja. Ukifuatilia watakujibu mtandao kwa ajili ya malipo ya nyuma au Ile faini ya laki moja unasumbua endelea kusubiria tu. Pamoja na uwepo wa mawakala wa pesa, pale ofisini kwao droo za meza zao utakuta zimejaa pesa zilizofungwa kwenye karatasi na majina ya wateja ikiwa ni malipo ya leseni na faini. Takukuru fikeni mjione hali hiyo.
 
Hakuna wa kumfunga paka kengele
 
Siyo Morogoro TU huu wizi upo halmadhauri zote nchini. Majuzi nikitaka kumkamatisha afisa mapato wa halmashauri moja. Baada ya kupigiwa simu kuwa wanataka kufunga duka langu la vifaa vya sinu. Binti aliambiwa natakiwa kulipia leseni elfu hamsini na fain laki moja. Nikamwambia mpatie afisa simu nilivyoongea nae nikamwambia anipe namba yake nirushe hiyo laki moja aende akanilipie akadai nitume kwenye namba ya Binti yangu. Nikaamua kwenda kulipa mwenyewe. Kufika ofisi zao za mapato. Wakaniambia mtandao unasumbua niache hiyo laki Moja na nusu. Meseji niliyopata ni ya malipo ya elfu 50 nasunbuana nao mpaka Leo juu ya malipo ya laki Moja. Mbaya zaidi huwa hawakusainishi popote ukiwaachia hiyo pesa. Na kwa kuwa unataka biashara isifungwe pesa inakulazimu uwape hivyohivyo pasipo ushahidi wowote.
 
Siyo kwa kumchukia wala nini. Mama angepumzika. Hii nchi kila ofisi ya umma ni rushwa na wizi. Kwa mwanamke tena aliyepata malezi mazuri ya kiislamu tena mzanzibar kupambana na maafisa wezi wa Tanganyika ni kumvika majukumu mazito. Urais una taka majike dume kama akina Anna Makinda kama ni mzanzibar basi awe type ya akina wakili Fatuma Karume. Wazee wakae nae akubali kupumzika kabla mambo hayajaharibika zaidi.
 
Hii nchi kila ofisi ya umma ni rushwa na wizi.
Ni kweli kila ofisi hivi Sasa ni rushwa tu.
1. Kuna halmashauri ilikuwa imepima viwanja na kiwauzia wananchi. Wananchi wakikamilisha malipo ili kuipata hati ya kiwanja, pesa unayotozwa ni kama unakinunua upya kiwanja hicho.

2. Wamama wajawazito wakishajifungua wanaambiwa baada ya miezi 3 njooni ofisi za RITA mchukue vyeti vya kuzaliwa vya watoto wenu. Ukifika unaambiwa lipia elfu 28. Hata ukilipa usumbufu wa njoo kesho unaanza kwa kisingizio cha mtandao kusumbua. Ukiongeza elfu 50 siku hiyo hiyo unapata.

Nchi ngumu sana hii.
 
Leta ushahidi sasa, tufanye kazi
Jim
Leta ushahidi sasa, tufanye kazi
  1. DED aombe orodha ya wafanya biashara waliopigwa faini Kwa kutokuwa na leseni au leseni zilizoisha ahusianishe na idadi waliolipia leseni mpya sambamba na faini.
  2. Aende site akaongea na wafanyabiashara wa moja ya Kata walizopita maafisa mapato.
  3. Afanye ziara za kushitukiza katika ofisi za mapato. Ajionee hiyo mifumo ya malipo kama kweli inasumbua Hadi wapokee fedha taslimu badala kufanya malipo moja Kwa moja.
  4. Afanye ukaguzi wa kushitukiza kwenye droo za meza za maafisa wanaoshughulikia kuingiza malipo yanayofanywa na wafanya biashara.
  5. Ashirki zoezi la kukagua leseni kwa wafanyabiashara walau siku moja.
Ukweli wa wizi huu ataubaini kama atakuwa hafikishiwi na sehemu ya fedha hizi.
 
Back
Top Bottom