Hussein J Mahenga
JF-Expert Member
- Mar 5, 2012
- 750
- 656
Na,
H. J. Mahenga, alias, Uncle Kaso
Usiku wa kuamkia tarehe 20 ya Januari ya mwaka 1964, yalitokea mauaji ya Mwarabu mmoja pale Magomeni aliyekuwa na duka, aliyepigwa risasi na wanaodaiwa 'waasi' wa JWT, kipindi hicho likijulikana kama Tanganyika Rifles, au kwa kifupi TR. Mwanya uleule, vibaka pia waliutumia kuiba mali za wafanyibiashara wengi Kariakoo na kwingineko, ambayo tathmini yake ilikuja kufanywa na serikali chini ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Job Lusinde, tarehe 22 Januari kwenye ziara ya Rais Nyerere katika maeneo mbalimbali ya Kariakoo.
Baada ya kurudi Ikulu, au kabla yake, tayari kulikuwa na ugeni Ikulu pale, wa wanajeshi wakiongozwa na Elisha Kavana, ambaye sasa alikuwa ameshapandishwa cheo na kuwa Brigedia akichukua nafasi ya Brg. Douglas, mzungu huyu. Ingawa presidental guard iliyokuwa chini ya Peter Bwimbo ilipata wasiwasi wa kutokea vurugu Ikulu pale, haikuwa hivyo; waliondoka salama salimini kabisa. Lakini baada ya hapo, tarehe 24 Januari, siku nne baada ya vurugu hiyo ya wanajeshi pale Colito na Ikulu ya Magogoni, ilitokea operation muhimu iliyopewa jina la Oparesheni Floodtide iliyoongozwa na wanajeshi wa majeshi kutoka Uingereza, wanamaji. Je, ilihusu nini hasa? Je, oparesheni Magogoni ilitokeaje? Kwa nini Special Branch haikuwa na taarifa za mipango ya maasi hayo? Je, Nyerere na Kawawa walijificha wapi?
Pantoni la MV Magogoni lilionekana upande wa Kigamboni badala ya upande wa Magogoni kama ilivyokuwa kawaida asubuhi ya tarehe 20 Januari 1964. Wafanyikazi wa pantoni lile walipohojiwa na Bhoke Munanka, akiwa waziri wa wakati huo wa Ofisi ya Rais, walieleza kuwa walikuwa wakimgojea Nyerere aliyekuwa ziarani na Waziri mkuu kwenye chuo cha Kivukoni.
Wakati yanatokea haya, Mwl. Nyerere na Waziri wake mkuu, Kawawa, walikuwa kwenye kijumba kidogo cha Sultan Kizwezwe, huko kwenye kijiji cha Salanga. Pamoja nao walikuwa askari wawili na mlinzi wake Peter Bwimbo, wakila mapapai na chakula walichokuwa wakipikiwa na msamaria mwema huyu, Kizwezwe.
Baada ya kufuatilia kwa kina, na mlinzi wa Nyerere kujiridhisha kuwa alikuwa mwanachama wa TANU mtiifu, Bhoke Munanka alifika kwenye nyumba ile na kuongea kinagaubaga na viongozi hawa wawili. Baadae alitoka na kuelekea Jijini, na kisha kuagiza Land rover la Ikulu liwapelekee matandiko viongozi hawa na chakula. Ingawa Nyerere alikataa wasipelekewe chakula, bali wangeendelea kula chakula cha familia ya Kizwezwe, kwani hawakuona ubaya wowote; na zaidi walijiridhisha kwamba Kizwezwe asingewasaliti.
***
Ilikuwa hivi. Maasi yalianza pale Colito (sasa Lugalo), kwa siri sana. Haikufahamika walikuwa wakipanga wapi mpaka pale kesi hii ilipopelekwa mahakama ya kijeshi kuwa walikuwa wakikutana Mbezi, nje kidogo ya Dar Es Salaam.
Kama nilivyotangulia kusema, ilikuwa ni mipango ya wachache sana, kwa sababu ambazo nitazieleza vyema.
Ilikuwa usiku, yapata saa 8:40 usiku ambapo Mlinzi wa Nyerere, Peter Bwimbo alipowatorosha viongozi hawa wawili na kuhepa nao Kigamboni, akilenga kuwapeleka Mjimwema ambako Nyerere alipendelea kupumzika wakati wa wikendi. Kuelekea huko ilishindikana kutokana na kwamba, tayari kulikuwa kumepambazuka, na hivyo wakakata shauri kuwa sasa waingie kwenye nyumba ya Raia, wakajikuta kwenye nyumba ya Kizwezwe, pale Salanga!!
Kutoroshwa kwa viongozi hawa kulikuwa na msafara wa watu watano tu ambao ndiyo walitumia pantoni lile; Nyerere, Kawawa, Bwimbo pamoja na askari wawili.
Ikulu waliachwa Bw. Mzena, aliyekuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, pamoja naye Kamishna wa Polisi (sawa na IGP sasa) Elangwa Shaidi, na walinzi waliokuwa na silaha kwenye geti kuu la kuingilia kwenye kasri la Ikulu. Walinzi hawa walikuwa ni wanajeshi wa Colito!
Kama nilivyosema awali, mipango hii haikufahamika na wanajeshi wengi kwa sababu, kama walikuwa wanafahamu wengi, basi Peter Bwimbo asingeruhusiwa kuingia Ikulu usiku ule, pamoja naye Mzena na Shahidi, kwa sababu waliokuwa wakilinda ni wanajeshi wa Colito, wenye maasi wenyewe. Pili, Nyerere na wengine wasingeweza kutoka, wangewekwa chini ya ulinzi.
Baada ya hali kutulia, na wakajiridhisha hivyo, Nyerere aliomba ndege ndogo ya Ikulu impeleke Mafia kwenda kufanya mawasiliano. Tarehe 22 Januari, akarudi rasmi Ikulu. Aliporudi Ikulu, tayari waasi walikuwa wamewapandisha vyeo Elisha Kavana ambaye alichukua nafasi ya Patrick Douglas kuwa Brigedia, na wengine wengi. Nyerere alizungumza nao Ikulu siku hiyohiyo.
Siku nne baadaye, tarehe 24 Januari, Nyerere alifanya Mawasiliano Uingereza ili iruhusu kikosi cha wanajeshi wa maji waliokuwa kwenye meli huko Aden (Yemen) ili wafike Colito kuwanyang'anya silaha waliojulikana kama waasi. Zoezi hilo ndilo lilijulikana kama Operation Floodtide, ambapo wanajeshi wale walichukua silaha za wote waliokuwa wamebainika kama waasi, ingawa baadhi yao walikimbia, na wakatangaziwa kujisalimisha, na wakafanya hivyo. Wanamaji hawa kutoka Uingereza walikaa mpaka September ya mwaka huo, mpaka pale nafasi yao ilipochukuliwa na wanajeshi wa Ghana.
Inaaminika Maasi hayo sababu yake ilikuwa ni kucheleweshwa kwa mipango wa Africanization jeshini, ambapo nafasi nyingi zilikuwa zikishikiliwa na wanazungu na ufinyu wa Mishahara. Hata hivyo, wapo wanaodhani kuwa yale yalikuwa ni mapinduzi yaliyoshindwa!