Huwa kila siku nawakumbusha humu, kupiga kinu cha nuclear Iran inabidi utumie bomber kama B2 ikapige na bunker buster, bunker buster ndio kombora limetengenezwa maalumu kupiga mahandaki ya kijeshi, sasa Iran sio tu wana mahandaki ya vinu vya nuclear, hayo mahandaki yapo chini kabisa ya mlima , huwezi kupiga kinu cha nuclear kipo chini ya mlima kwa kutumia kombora uchwara zinazobebwa na F35, na ili kusudi B2 ipige hilo eneo inabidi iende usawa wa hiko kinu, kitu ambacho hio B2 itapigwa tu... kingine bunker buster ya kupiga ku penetrate mlima, imalize iingie kusambaratisha concrete iliyo juu ya kinu cha nuclear si mchezo, hio bunker buster haipo.
Someni vitu mfuatilie, Iran ina vinu sehemu nyingi tofauti.
msidanganyane kwenye gahawa eti wamepiga kituo cha utafiti, vituo vya utafiti vipo chini ya ardhi, vimezungukwa na kila aina ya defenses systems pamoja na AAA, ndio maana myahudi kila mara anaua wanasayansi kwa kudhani ata stop projects zao.
Trump kwa Kiduku tu aliufyata alijitia kichaa, sasa atakuja kuanza kupambana kivita na Iran?, kule Iraq walipiga bases kipindi ni rais wa US, akatia mkwara atalipiza hadi kesho hakuwahi.
Iran ina uwezo wa kupiga bases za US zote hapo Middle East.