Ndio mkuu... Kihebrania ndiyo Hebrew language
Pia ndio kwa asilimia fulani ni kweli kuwa kila myahudi ni muisrael lakini sio kila muisrael ni myahudi... (Nimesema ina ukweli kwa asilimia fulani)
Asilimia za ukweli ni zipi?
Kwanza tuanze mwanzo kabisa kutambua kuwa uyahudi ni asili (na dini) wakati Uisrael ni uraia..
Wayahudi wote asili yao ni Israel ndio maana ya kusema kila myahudi ni muisrael.. Lakini sio kila muisrael ni myahudi kwa sababu mtu yeyote hata kama sio myahudi anaweza pata uraia wa Israel akikidhi vigezo vya kisheria...
Nimesema ina ukweli kwa asilimia fulani kwa kuwa pia wapo wayahudi ambao sio Waisrael... Yani ni watu ambao wayahudi wanaoishi nchi nyingine na kuwa na uraia wa nchi hizo...
Mfano rahisi; (tuchukilie mfano wasukuma ndio lingekuwa kabila pekee Tanzania)
Ni sawa na kusema, kila msukuma ni mtanzania lakini sio kila mtanzania ni msukuma..
Kwa maana ya kwamba wasukuma asili yao ni watanzania, hivyo kwa asilimia fulani tunaweza kusema "kila mtanzania ni msukuma"
Pia tunasema sio kila mtanzania ni msukuma kwa kuwa kuna watanzania ambao sio wasukuma wana uraia wa kuomba... Mfano wahindi, waarabu, wazulu, n.k
Lakini hii nayo ina ukweli kwa kiasi fulani tu kwa kuwa wapo wasukuma ambao sio watanzania... Yaani unaweza kwenda marekani na kukutana na msukuma mwenye uraia wa Marekani...
Lakini huku nimeeleza mbali kidogo.. Lakini kwa faida ya swali ulilouliza, ndio twaweza sema "kila myahudi ni muisrael lakini sio kila muisrael ni myahudi"