Oparesheni za Kijasusi zilizofanikiwa zaidi katika Historia

Oparesheni za Kijasusi zilizofanikiwa zaidi katika Historia

Akhsante sana The bold Tunasubiri hiyo operation ya pili!


Ila kwenye hii mission kifo cha Jonathan (Yoni) Netanyahu kilinisikitisha sana! Na alifariki akiwa mdogo sana huyu jamaa!
Kabisa... Hata Ehud Barak alikuwa Kenya anawasubiri yale madege yarudi... Anasema kuwa yalipotua Uwanja wa Jomo Kenyatta alishangaa makomando na waliokolewa wakiwa na huzuni tofauti na alivyotarajia kuwa wangetua wakishangilia kwa shangwe... Alipowauliza kwanini hawana furaha ndipo wakampa taarifa ya kifo cha Yonatan Netanyahu...
 
WENGI SANA HUNU JUKWAANI HUWA WALISEMA HII STORY ILISHAWEKWA... TUJARIBU KUPITIA KIPINDE HIKI...

Kwa bahati mbaya kulikuwa na mateka kadhaa ambao wwalikuwa hawajui kihebreania sawia na hii iliwagharimu sana. Kwa mfano kulikuwa na kijana wa mika 19 aliyeitwa Jean-Jacques Maimoni, huyu alikuwa amehamia Israel siku si nyingi sana kutokea nchini ufaransa. Lilipotolewa tangazo hilo la kila mtu kulala chini hakuelewa na alibakia akiwa amesimama na alitandikwa risasi na makomando wa Israel pamoja na wale watekaji. Kijana huyu hakuwa peke yake, lakini pia kulikuwa na mateka mwingine aliyeitwa Ida Borochovitch, ambaye alihamia Israel kutoka nchini Urusi.

Unaanzaje kusema mtu kama huyu amecopy na kupaste hii story... Tujaribu kupunguza chuki zisizo na maana vinginevyo mtajikuta mmeingia kwenye ushirikina pasina kujua... Hongera mkuu The bold honestly mi ndio nimejua leo kwamba kuna mateka waliuwawa kutokana na kutojua lugha.
Pamoja sana ndugu yangu magnifico

Nathamini sana sapoti yako..
 
Back
Top Bottom