Sijui nikoje nikishaona habari ya kitu fulani kutokea halafu sababu/muanzilishi ikatajwa NWO, Illuminati au Freemason hua si ipi uzito sana. Hua nachukulia kama hadithi za kina Shigongo au movie za Marvel's.. Uanzishe corona uue watu then? Unataka utawale dunia ambayo watu wake umewaua au wako kwenye mateso halafu iwe na faida gani katika sphere zote kiuchumi, kisiasa au kijamii? Kwamba corona imeanzishwa kuwamaliza wenye 5G ambao ni wachina, sasa mbona south Korea, japan, italia ambao ni washirika wa mpinzani mkuu wa China kwenye 5G tech nao corona inawaua! USA nako imeripotiwa kifo kutokana na huu ugonjwa so wameunda bioweapon ambayo hawawezi kuimanage! Ukiwaza kwa umakini hamna theory yoyote ya mlengo huu inaleta mantiki