Operation NORTHWOOD: CIA kufanya ugaidi ndani ya Marekani

Operation NORTHWOOD: CIA kufanya ugaidi ndani ya Marekani

DeepPond

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2017
Posts
41,728
Reaction score
103,997
Operation Northwood Ni false flag operation ya kijeshi iliyopangwa na wizara ya ulinzi ya marekani kwa kushirikiana na CIA mwaka 1962 kipindi cha Vita baridi ili kupata sababu ya kuivamia kijeshi nchi ya cuba.

Lengo kuu la operation Hii ilkua kutengeneza mfulurizo wa matukio ya mashambulizi ya kigaidi ndani ya ardhi ya marekani na Kisha kuilamu serikali ya CUBA.

Miongoni mwa matukio yaliyokua mezani yakisubiri utekelezaji ilkua ni
1. Magaidi Kuteka na kuua Watu kwenye Ndege ya kiraia ya kimarekani na kuilaumu serikali ya cuba

2. Kutega vilipuzi na kuua Watu kwenye kwenye baadhi ya miji ndani ya marekani Kisha kuilaumu serikali ya cuba.

3. Kuchukua wakimbizi wa ki-cuba na kuwaweka kwenye meli, kisha kuizamisha kusudi na lawama zote kuitupia serikali ya cuba.

mikakati na uchambuzi makini wa operation ile uliwekwa ktk maandishi ,kuwasilishwa na kupata sapoti kubwa kutoka kwa washauri mbalimbali wa usalama na kijeshi kutoka ndani ya PENTAGON.

Ila Katika hali isiyotarajiwa operesheni hii ilikataliwa Moja kwa Moja na raisi JOHN F. Kennedy pamoja na washauri wake wote bila kupepesa macho kwa kuambiwa "HAINA MASHIKO"

Raisi John f. Kennedy aliiandikia pentagon kwamba kwa jinsi asili ya shambulio zima lilivyopangwa, kwamba haiingii akilini kuwatoa sadaka wa mamia ya raia wasio na hatia ili tu kuhalalisha kuivamia kijeshi Cuba, ambayo kwa mtizamo wake hakuiona Kama tishio kubwa la usalama kwa marekani.

Na operation ile ikawa imekufa kibudu Moja kwa Moja, ila Makabrasha yote ya mipango yote ya
Operation Hii yalibaki kua siri (classified) ndani ya maktaba kuu ya VCIA Hadi hapo CIA wenyewe walipoamua kuiweka wazi kwa umma(declassified) mwaka 1997.

IMG_20240419_213205.jpg
IMG_20240419_213344.jpg
 
Back
Top Bottom