Operesheni "Gothic Serpent"!!!!!

Operesheni "Gothic Serpent"!!!!!

donlucchese

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2011
Posts
17,128
Reaction score
21,885
Mnamo mwezi December 1992, raisi wa Marekani wa wakati huo Georgw H.W Bush alitoa amri kwa majeshi ya marekani kuungana na umoja wa mataifa katika operation ya pamoja iliyoitwa 'operation rejesha tumaini (operation restore faith)' na dhumuni la msingi ilikua kurudisha amani na 'order' katika nchi ya Somalia.

Kipindi hiko nchi ya Somalia ilikua imeharibiwa kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe na njaa kali kutokana na kutawaliwa na faction leaders (nimekosa tafsiri iliyo rasmi) na kwa miezi mingi iliyofuata hali ilizidi kutetereka.

Mnamo tarehe 20 January 1993, rais aliefuata baada ya Bush, Bill Clinton alichukua ofisi.
Mwezi May 1993, vikundi vyote vilivyokua vikihusika na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe vilikubaliana kukaa kikao na kusitisha mapigano ambapo kikao hicho kiliongozwa na Mohamed Farrah Aidid.

Kikao jicho kilipelekea kuanzishwa kwa muungano wa kisiasa uliojulikana kama The Somali National Alliance (SNA) mwezi wa sita 1993.

Muunganiko huo ulihusisha vikundi mbali mbali ambavyo vyote vikawa chini ya utawala wa Aidid, baada ya Aidid kujitangaza kua raisi wa Somalia.

Wakati huo huo raia wengi wa Somalia walipinga shughuli za majeshi ya Marekani nchini mwao ambapo watu wengi hususan wanawake na watoto walijitokeza na kukamata silaha kupambana dhidi ya majeshi ya Marekani wakati wa mapambano katika mji wa Mogadishu.

Tarehe 5 June 1993, moja ya mashambulizi mabaya zaidi kutokea kwa vikundi vya majeshi ya umoja wa mataifa (UN) nchini somalia lilitokea na kupeleka vifo vya wanajeshi 24 wa Pakistan walifanyiwa 'ambush' na kuuawa katika eneo lililokua chini ya utawala wa Aidid.

Matumaini yeyote ya kumaliza mgogoro kwa njia ya amani yalitoweka rasmi na ndipo baraza la usalama la UN ( UN Security council) lika-issue kitu kilichoitwa "Resolution 837".

Hili lilikua ni tamko rasmi kuhusu kusakwa hadi kukamatwa na kuhukumiwa wale wote waliohusika na shambulizi lile.

Ndege za Marekani na majeshi ya UN yakaanza mashambulizi katika ngome za Aidid lakini bwana Aidid akabaki kua mkaidi na mashambulizi kati ya wasomali na vikundi vya majeshi ya umoja wa mataifa yakashamiri kwa hali ya juu.

Itaendelea.......
 
Hapo ndipo Hollywood wakaja na bonge la movie Black Hawk Down.
Kama vile haitoshi jamaa wakaongeza na game Delta Force; Black Hawk Down.
Kama sijakosea operation hii ina a.k.a The Battle of Mogadishu
Ni kweli kabisa mkuu, hiyo game nliicheza kitambo
 
TASK FORCE RANGER:

Tarehe 8 August 1993, vikundi vya wanamgambo vilivyoongozwa na Aidid vililipua bomu la kutumia rimoti gari la wanajeshi wa marekani na kuua polisi jeshi (military police) wanne wakimarekani. Wiki mbili baadae, bomu jingine lilipuliwa na kusababisha majeruhi zaidi. Katika kujibu mashambulizi hayo, rais Clinton aliainisha maombi ya kupeleka kikosi maalum kilichokua na askari 400 (US Army RANGERs) na maafisa viongozi wa Delta force. Kikosi hiki maalum kiliitwa 'Task Force Ranger' na pia kilihusisha askari wapatao 160 wenye weredi wa hali ya juu (elite troops).
Naam, shughuli ilikua imeanza kuiva. Askari hawa wakasafiri mpaka Mogadishu kuanza rasmi msako dhidi ya Mohamed Farrah Aidid. Tarehe 22 August, kikosi hiki maalum kikatumwa kwenda Somalia chini ya uongozi wa meja jenerali William F. Garrison, aliyekua kamanda kiongozi wa JSOC ( Joint Special operations command) kwa wakati huo. Rejea makala mbali mbali za nyuma kufahamu zaidi kuhusu JSOC.
Kikosi hiki maalum kilijumuisha:
B Company kutoka 3rd battalion 75th Ranger regiment,
C Squadron kutoka 1st Special Forces Operational Detachment-Delta (1st SFOD-D),
Helikopta 16 na marubani kutoka 160th Special operations Aviation regiment (160th SOAR) ambapo kulikua na helikopta aina ya MH-60 Black Hawks na AH/MH-6 little birds,
NAVY SEALS kutoka Naval Special Warfare Development Group ( DEVGRU),
Wataalam wa uokoaji kutoka jeshi la anga la marekani ( Airforce Pararescuemen) na wataalam wakivita kutoka katika kikundi cha mbinu maalum za kivita ( 24th Special Tactics Squadron). It was good to go......
 
Namkubali sana huyo Aidid...mwenye picha ya yule actor aliyemwigiza Aidid aweke picha yake hapa!
 
Back
Top Bottom