Hatimae taifa limepata "UHURU" kutoka kwa mkoloni mweusi.
Mama Samia mungu ampe umri mrefu na wenye afya, njia anayopita hakika inaleta faraja sana kwa wananchi. Watu wanamtolea maneno maswala ya kurudisha "IKULU" ndani ya Dar ila hawaoni sababu zinazomfanya awepo Dar, wamekaa kuishi maisha kwa kukariri na wala hawajui sababu ya kwanini "Nyerere alifanya Dodoma kuwa Mji Mkuu".
Kuwepo kwake Dar sasa hivi kuna rahisisha kuonana na;
1) Wafanyabiashara wa kubwa ulimwenguni, africa na tanzania (Mfano Alhaj Aliko Dangote) ili kuwashawishi warudishe biashara nchini na wafungue viwanda zaidi, ili watanzania wapate ajira.
2) Mabalozi wa mataifa mbali mbali ambao ofisi zao zipo Dar Es Salaam, kuwashawishi walete wafanyabiashara kutoka katika mataifa yao (Mfano Mabalozi Wa Saudia jana alipokutana nao).
3) Kuifufua Dar Es Salaam kuwa "BUSINESS HUB & BUSINESS CITY" baada ya kuuliwa kwa miaka 5.
4) Kuweka mazingira mazuri na wafanyabiashara waliowekeza Dar.