'Operesheni Haki' yafika Mkoa wa Kilimanjaro, mashambulizi yaongozwa na Salum Mwalimu

Kwa nini hawakutoa maneno makali ikulu ilipo hamia Chato. Tuache mambo ambayo hayana tija kwa nchi yetu. Ametumia busara kuzogeza huduma kwa mabolozi na wafanya biashara kuliko wao kufurika Dodoma. Hii ni busara na unyenyekevu kwa vitendo.
 
Kwa kuwa sasa tupo kwenye utawala wa kistaarabu, utawala wa mwenye hekima, Rais Samia, nawaomba viongozi wa CHADEMA na wanachama, kuwasilisha hoja zao kwa njia za hekima na busara, mpaka hapo itakapoonekana kuwa njia hizo zimeshindwa kuleta matokeo chanya.

Inakuwa ni ngumu sana kutumia lugha kali na iliyokosa staha dhidi ya kiongozi aliye na hekima kama Samia.

Pamoja na ukweli kuwa jukumu la cha cha upinzani, ni kuikosoa Serikali iliyopo madarakani pale inapokosea, lakini ni vema kumpongeza Mama Samia kwenye mazuri aliyoyafanya mpaka sasa.

Tufahamu kuwa Rais Samia amepokea uongozi kutoka kwenye utawala dhalimu ambao tayari ulikwishaotesha mizizi. Yupo kwenye chama cha mtangulizi wake, wasaidizi wake ni wale wale waliokuwa mikono ya kutekelezea uovu, na kuwapiga wote chini, siyo kitu kinachoweza kufanyika bila ya kuleta taharuki. Hivyo, aliyoyafanya tunaweza kuona ni madogo na machache lakini kwa mazingira aliyopo, tukubali kuwa amejitahidi sana. Tumpe moyo wa kufanya zaidi, hasa kwenye mambo ya msingi kwa Taifa (siyo vyama vya siasa).
 
Umechanganyikiwa Luna ccm vs Sukuma gang,ccm wanasema 10 kwa Samia Sukuma gang mapovu yanawatoka
Mkuu sasa mimi si nakuunga mkono? Yani ili kuwakomoa hawa sukuma gang inabidi ccm na Samia wapewe mi 10 tena na mr belgiji atasubiri sana hadi 2100,,

Au we uko upande gani wa sukuma gang au ccm?
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] daaah kipindi Cha jiwe katiba ilikuwa hii hii lakini Hali ilikuaje?
Katiba inamakosa mengi Sana!!
Lkn hii katiba mpya haisaidii chadema au cuf, hii ni katiba ya nchi na wananchi wake, kwanini CCM wanaigomea?
 
Unajuaje kwamba wananchi wanawachoka?
 
Kwani hii katiba iliyopo inambagua nani? au inabagua chama kipi?
 
Katiba ni Sheria..... Naam....

Je hizi Sheria zilizopo sasa zinafuatwa ?, Watu wanajua haki Zao ?, Wanakubali kuzidai na wakizidai wanapewa ?

Kuwepo kwa Kitabu kitachoitwa Katiba sio Mwarobaini kama Sheria mama hiyo haifuatwi na inavunjwa kila kukicha unless otherwise ni kuingia gharama ya kutengeneza kitabu kingine ambacho wala matakwa ya wananchi hayamo bali interests za wachache...
 
Wasisahau haki ya ukomo wa madaraka wa Mbowe ilikila mwanachama awe na haki kukiongoza chama.
Na haki ya kujua ruzuku zinaenda wapi wakati hakuna hata ofisi iliyojengwa makao makuu.
Haya ndo ya muhimu kuliko katiba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…