Nafikiri itakuwa si vibaya makamanda hao 19 walioko bungeni, wakiomba radhi tu kama inavyoweza tokea kwa binadamu yoyote, kwa mihemko waliyofanya ili maisha yaendelee.Manake wanachama nafikiri walisikitishwa na move yao kukimbilia bungeni bila ridhaa ,hivyo kuonekana kama kusaliti chama chao, maana watu kama akina Mdee,Bulaya,Matiko,Kishoa na wengine,ukweli ni kwamba walipitia vipindi vigumu vya kuswekwa ndani, lakini kwa sababu ya ukakamavu wao , wanachama wa CDM nafikiri walikuwa wamewaamini sana kiasi cha kwamba kila wakati walikuwa tayari kuwachangia na kuwalipia dhamana walipokuwa matatani na kesi zilipowaandama......sijui kitu gani kiliwapata aisee baadae na kufikia kuchemsha.... Wakiomba msamaha Wasameheni jamani nyie CDM......na nikitazama sura za hao wazee zinajieleza vizuri sana.....