Operesheni tokomezeza flash disk na mawaya, Nawezaje kutazama video za kwenye computer kwenye Tv kwa kutumia wifi ( wireless )

round kick

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2025
Posts
345
Reaction score
1,145


Nahitaji kuifanya Tv yangu iwe kama youtube au Netflix lakini niweze kustream video kutoka kwenye laptop yangu bila bando. Laptop nitakuwa naiacha chumbani, niweze kuchagua video moja kwa moja kwenye TV bila kugusa laptop.

Nimechoka kudownload videos kwenye pc kisha niiingieze kwenye flash baada ya hapo ndio nitumie kwenye TV, process inachosha pia sihitaji mawaya ya hdmi.

Vifaa nilivyonavyo

Laptop - processor yake ni core i5, hard disk ni 1 TB, nimechagua laptop badala ya desktop sababu ya matumizi madogo ya umeme.

Tv yangu ni smart tv inaingiza apps za playstore, pia inaweza kuconnect wifi

Cha kuongezea nina router ya tigo ambayo huwa siitumii, labda inaweza kuhitajika kuunganisha Tv na Pc kulingana na maelezo yenu wataalam
 
Simple sana, Kama TV yako ni smart na unayo smartphone & router, unganisha simu na TV kwenye router, kisha nenda kwenye simu washa video unganisha kwenye TV, au Ukiingia Youtube yenyewe itakuuliza kama unataka kuplay kwenye smart tv yako, press ok then enjoy!
 
Tv gani ina os gani, uzi wako wa Server kuna watu wamekushauri jellyfin na Plex hizo ndio wengi wanatumia.

Issue inakuja pale pale umetumia cpu gani kutengeneza server, kama server yako inakula Mamia ya watts hapo ndio utaanza kuona Dunia chungu.
 
Naomba uwe unasoma na maelezo ya post

Nahitaji kustream videos kutoka kwenye pc yangu,
 
Tv gani ina os gani, uzi wako wa Server kuna watu wamekushauri jellyfin na Plex hizo ndio wengi wanatumia.

Issue inakuja pale pale umetumia cpu gani kutengeneza server, kama server yako inakula Mamia ya watts hapo ndio utaanza kuona Dunia chungu.
Ni Tv ya samsung smart Tv, nimeona inaweza kuingiza hizo apps za jellyfin na plex

Ile computer niliyoifanya iwe file server sitaweza kuitumia kwasababu nahofia itakula sana umeme, ni special kwajili ya kuhamisha na kutunza files tu.

pc nitayotumia ni laptop yenye proceessor core i5 kizazi 6 th gen, ili kupunguza matumizi ya umeme pia urahisi wa kudownload videos
 
Hujaeleweka,unataka kutafuta movie mtandaoni kwa kutumia PC then zionekane kwenye TV,au unataka kutumia simu kusearch movies then uziangalie kwenye TV...?
 
tumi
Tumia HDMI Cable
 
Tv gani ina os gani, uzi wako wa Server kuna watu wamekushauri jellyfin na Plex hizo ndio wengi wanatumia.

Issue inakuja pale pale umetumia cpu gani kutengeneza server, kama server yako inakula Mamia ya watts hapo ndio utaanza kuona Dunia chungu.
Mkuu Hebu Ni0e Elimu Kuhusu kutengeneza Sever kwenye TV
 
Jifunze kuhusu DLNA software.

Mfano mmoja ni Plex Server.

Unaweza ku install Plex server kwenye laptop yako, uka install Plex client kwenye TV yako, kisha ukacheza movies zako zilizopo katika Plex server kwenye laptop yako kwa kuziangalia kwenye TV yako.

Nimekuwa nikifanya hivi kwa miaka mingi, ila mini natumia NAS (Network Attached Storage) kama server yangu ya Plex.

www.plex.tv

Mkuu Tebajanga anaweza kutuongezea kuhusu Jellyfin

 
Simple tumia casting, hii ipo kwenye chrome kama utastream online, ulizodownload play kwenye vlc,, feature hii kwenye vlc utaenda playback>renderer>chromecast/android tv

View attachment 3266063
Sihitaji ku cast au ku mirror, nataka kila kitu nimalizie kwenye TV, niwe nachagua videos kwenye tv
 
Mkuu Hebu Ni0e Elimu Kuhusu kutengeneza Sever kwenye TV
Ukiwa na router unaweza connect vifaa mbalimbali kwenye same network na hivyo vifaa vikaonana.

Mfano una router umetengeneza WiFi yako inaitwa Mambo jambo na simu na tv vyote vime connect kwenye hio network basi utaweza play video ambayo ipo kwenye simu kupitia tv.

Ili kufanya mambo yawe rahisi software kama Stremio, plex, kodi, jellyfin etc hutumika. Hizi software una install kwenye vifaa yako vyote, computer unaweka software mama, na vifaa kama simu ama TV unaweka client software.

Ukifungua ile client software kwenye tv utaona mafile yako ya computer kama vile movies, series etc.

Muonekano wa hizo software kama Plex.
Inakua kama Netflix sema this time inakua offline kwa Mafile yako mwenyewe.
 
Kwa plex kwenye computer eka server,. Download hapa


Fanya configuration maliza.

Nenda kwenye TV store download plex, then ziunganishe TV na laptop, utaweza play media za kwenye laptop.
 
Kwan ukitumia mirror cast unahitaji kuwa na waya?
Laptop nitakuwa naiacha chumbani, Tv ipo sebleni

Hata nikiwa sipo nahitaji watu wengine waweze kuchagua video za kutazama kwenye TV bila kugusa laptop
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…