round kick
JF-Expert Member
- Feb 3, 2025
- 345
- 1,145
Nahitaji kuifanya Tv yangu iwe kama youtube au Netflix lakini niweze kustream video kutoka kwenye laptop yangu bila bando. Laptop nitakuwa naiacha chumbani, niweze kuchagua video moja kwa moja kwenye TV bila kugusa laptop.
Nimechoka kudownload videos kwenye pc kisha niiingieze kwenye flash baada ya hapo ndio nitumie kwenye TV, process inachosha pia sihitaji mawaya ya hdmi.
Vifaa nilivyonavyo
Laptop - processor yake ni core i5, hard disk ni 1 TB, nimechagua laptop badala ya desktop sababu ya matumizi madogo ya umeme.
Tv yangu ni smart tv inaingiza apps za playstore, pia inaweza kuconnect wifi
Cha kuongezea nina router ya tigo ambayo huwa siitumii, labda inaweza kuhitajika kuunganisha Tv na Pc kulingana na maelezo yenu wataalam