moto wa kifuu
JF-Expert Member
- Sep 17, 2015
- 390
- 60
Afadhali Ebola kuliko ccm
Uzuri ni kwamba mungu anjua kuwa unatania tu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Afadhali Ebola kuliko ccm
Mi hua najiuliza, why not Lowasa? Sielewi, why nguvu nguvu kubwa hivi inatumika? Sielewi, hivi kama lowasa mwizi si wamkamate tu yaishe? Sielewi, kuna experiment kubwa sana ya kufanya, why not vote for him ili nigundue? Duh huyu lowasa ni binadamu wa aina yake. Mara fisadi, mara mgonjwa, mara mlutheri, mara mkaskazini duh, nimezindukaaaaa
NB: Video Inafuata
Operesheni Zinduka imeanza kama nilivyoahidi (jana haikuwezekana kwa sababu moja tu ya heshima ya Mch. Mtikila na haihusiani na mipango ya watu wengine). Nitajitahidi kuwa na onesho hili kila siku (ukiondoa mwisho wa Juma) na nitazungumzia mada mbalimbali. Wiki hii ya kwanza zaidi nitagusia hoja nyingi zilizoibuliwa kutushangaa tunaomkataa Lowassa kama mgombea Urais kwa tiketi ya upinzani.
La pili nitajitahidi hasa wiki ile inayokuja kutoa nafasi kwa wagombea wa CHADEMA kwenye Ubunge (ambao tutaweza kuwafikia) ili wajiuze kwani ninaamini Bunge lenye nguvu lililoundwa na watu waliolelewa na kukomaa katika upinzani na wenye kuelewa hasa ajenda ya upinzani ndio chachu ya kweli ya mabadiliko tuyatakayo. Hivyo, wiki ile inayokuja tutatoa nafasi hii kwa wote tutakaoweza kuwapata.
Tatu, kwa vile nina uhakika wapo wengi ambao hawajakubaliana na uamuzi wangu huu (ambao naamini ni sahihi) basi nitatoa nafasi pia kwa watu wengine kutoa hoja zao dhidi ya ninachosema (sikiliza onesha hili juu ya 'mashart kuzingatiwa'). Kwa barua pepe anuani yangu ipo chini na namna nyingine ya mawasiliano nitawajulisha siku chache zijazo.
Nitajitahidi kuweka shows zote kwenye uzi huu huu kila siku, na video zitafuata chini toka ya zamani zaidi hadi mpya zaidi.
Mwisho, ninaamini na nina uhakika kuwa kwa atakayeamua kunisikiliza kuanzia sasa hadi kuamkia Uchaguzi Mkuu hatoweza kumpigia Lowassa kura ya Urais. Ni kwa sababu hiyo wale ambao tayari wameshaamua kuwa haijalishi nini kitasemwa juu ya Lowassa nawaomba au kuwashauri wasisikilize mada hizi wasije kujikuta wanabadili mawazo. Mada hizi ni kwa wale tu ambao bado hawajaamua au wale ambao wameamua lakini bado wanajikuwa wanavuta na upepo wa 'nyomi' kiasi kwamba bado hawajathibitika katika msimamo wao.
"Uamuzi Makini, Uamuzi wa Lazima, Uamuzi Sahihi"
MMM
ONESHO 1. "Baada ya Kelele Sauti za Hoja Zitashinda"
ONESHO 2. "Makosa 2 ya Dr. Slaa na 1 la Mbowe - Jumatano Oktoba 7, 2015)
<strong>