Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
- Thread starter
-
- #161
Mzee Mwanakijiji usijiche kwenye keyboard. Anza kwa kujitambulisha jina lako halisi, kisha panda jukwaani. Kama una uwezo huo.
MWISHO: kwenye video zako zitakazofuata tafadhali tafuta mtaalamu akusaidie kwenye speech yako..punguza maneno yasiyo na mantiki. hizi ""eeh" "aaah"! Ninaamini ulijiandaa na uliiandaa speech kabla ya ku-rekodi. Inapoteza ladha kusikiliza! Inakaa kama unawaza kwa kadri unavyozidi kuongea. Go straight to YOUR point..!
Nashukuru.
Asante kwa ushauri wako na maoni yako; ila una uhakika gani ilikuwa ni "speech"? aah, eeeh na ooh.. ni sehemu ya mazungumzo eeh?
NB: Video Inafuata
Operesheni Zinduka imeanza kama nilivyoahidi (jana haikuwezekana kwa sababu moja tu ya heshima ya Mch. Mtikila na haihusiani na mipango ya watu wengine). Nitajitahidi kuwa na onesho hili kila siku (ukiondoa mwisho wa Juma) na nitazungumzia mada mbalimbali. Wiki hii ya kwanza zaidi nitagusia hoja nyingi zilizoibuliwa kutushangaa tunaomkataa Lowassa kama mgombea Urais kwa tiketi ya upinzani.
La pili nitajitahidi hasa wiki ile inayokuja kutoa nafasi kwa wagombea wa CHADEMA kwenye Ubunge (ambao tutaweza kuwafikia) ili wajiuze kwani ninaamini Bunge lenye nguvu lililoundwa na watu waliolelewa na kukomaa katika upinzani na wenye kuelewa hasa ajenda ya upinzani ndio chachu ya kweli ya mabadiliko tuyatakayo. Hivyo, wiki ile inayokuja tutatoa nafasi hii kwa wote tutakaoweza kuwapata.
Tatu, kwa vile nina uhakika wapo wengi ambao hawajakubaliana na uamuzi wangu huu (ambao naamini ni sahihi) basi nitatoa nafasi pia kwa watu wengine kutoa hoja zao dhidi ya ninachosema (sikiliza onesha hili juu ya 'mashart kuzingatiwa'). Kwa barua pepe anuani yangu ipo chini na namna nyingine ya mawasiliano nitawajulisha siku chache zijazo.
Nitajitahidi kuweka shows zote kwenye uzi huu huu kila siku, na video zitafuata chini toka ya zamani zaidi hadi mpya zaidi.
Mwisho, ninaamini na nina uhakika kuwa kwa atakayeamua kunisikiliza kuanzia sasa hadi kuamkia Uchaguzi Mkuu hatoweza kumpigia Lowassa kura ya Urais. Ni kwa sababu hiyo wale ambao tayari wameshaamua kuwa haijalishi nini kitasemwa juu ya Lowassa nawaomba au kuwashauri wasisikilize mada hizi wasije kujikuta wanabadili mawazo. Mada hizi ni kwa wale tu ambao bado hawajaamua au wale ambao wameamua lakini bado wanajikuwa wanavuta na upepo wa 'nyomi' kiasi kwamba bado hawajathibitika katika msimamo wao.
"Uamuzi Makini, Uamuzi wa Lazima, Uamuzi Sahihi"
MMM
ONESHO 1. "Baada ya Kelele Sauti za Hoja Zitashinda"
Sina hata guts za kurekodi sauti. Mwenzangu wewe na heshima uliyojipatia bado wajificha mkuu? Tena mtu wa system na bado wajificha?Watu wengine bana sasa wewe umejificha wapi? nyuma ya printer?
Hili ndilo swali ambalo Mzee Mwanakijiji anapaswa alijibu badala ya kuzungukazunguka?
Mimi nilifikiri kuna kitu cha maana kwenye the so called VIDEO, lakini ndani yake nimegundua kutokujiamini kwa the so called Mzee Mwanakijiji.
Ukisikia mtu anasema 'TUTA.....' hii ni dalili ya kutojiamini. Umetutangazia operesheni ukianza na 'NITA......' huku mbele tena unaanza 'TUTA....'. Kwa kifupi sijaambua jambo zaidi ya ngonjera.
Unaposema SISI unamaanisha wewe na nani?
Siyo lazima kulijibu swali hili; hatua kwa hatua kwanza. Ukisikiliza mada ya kesho nina uhakika utaona kuwa siyo mimi ninayepaswa kusema watu wamchague nani; Mbowe na waliomleta Lowassa ndio wamewapa Watanzania uamuzi wa nani wamchague. Miye nasema tu nani wasimchague. Kama hadi tunakaribia mwisho wa Uchaguzi watu hawajui bado nani wamchague basi itabidi sisi sote kuwasaidia hawa.
Mpakwa mafuta Mzee Mwanakijiji,
Teh teh teh!
Leo upo "kigango" gani? Naona unaendelea na kazi yako ya "Mchumia dini"
Nisalimie Vatcan!
Hivi unawachukuliaje Watanzania kwa mfano? Yani mimi shida yangu kwako ni kutudanganya tu! Nisigekuona muongo na mfitini kama ungeacha kutumia sifa hiyo ya 'mwandishi huru' useme tu wewe ni ccm na ndiyo sababu ya kutomtaka Lowassa! .
Heri Lowasa na Sumaye watuongoze, siyo hao wauza unga, ambao nina uhakika wanawalipa nyinyi waandishi wa habari. Tafadahari Mzee Mwanakijiji, heri Lowasa kuliko Magufuli anayeelea kwa mgongo wa wala rushwa, Mkapa na Kikwete! Heri Lowasa Mwizi tunayemfahamu anayejua anatka kufanya nini, kuliko mMagufuli ambaye hata vyombo vya dola havitamheshimu. .
Mzee Mwanakijiji Kaka leo unataka kutuaminisha kwamba Lowassa ndio the biggest evil na ndio hatari kubwa kuliko CCM.
Mbona hili rahisi; mimi na wale wengine wote ambao wamekataa kupanda treni lisiloenda popote ambalo tunaambiwa limeondoka Station. Unafikiri wote ni abiria?
Kwenye maelezo yako kuna sehemu umesema kwamba upinzani ulikuwa na nafasi kubwa ya kushinda safari hii (kama wasingemchukuwa Lowassa). Siwezi kukubalina na wewe kabisa. Kwanini? Tume ya uchaguzi ni kikwazo. Hivyo haijalishi nani anasimama kugombea upinzani, bila tume kubadilishwa hatashinda. PS. Mimi ni mshabiki wa mabadiliko na Lowassa ni chaguo langu na nina ukakika ATASHINDA kwa kura nyingi lakini hatatangazwa.
Miye nasema tu nani wasimchague.
CCM hata wangemsimamisha Amina Salum Ali wangetangazwa washindi tu.
Hivi watu wanadhani haya mabadiliko ya [uteuzi wa makamishna] ya tume ya uchaguzi yaliyofanywa na mwenyekiti wa CCM ni ya bure tu?
Nitalijibu hili swali vile vile... stay tuned. Hatari sasa hivi ni zaidi ya CCM!
Kwa nini husemi nani 'wasiwachague'?