SONGOKA
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 1,836
- 1,846
Kila kona DR shika, si wasomi wala serikali inayoonyesha kushtushwa na hizi shangwe ila nao wameingia humohumo katika mkumbo.
Dr shika anaposhangiliwa ndo kwanza naona matatizo yake yanakuwa makubwa, labda tuanze hivi
- Dr shika anaonekana kuwa na matatizo makubwa ya kisaikolojia, na hili linaonekana waziwazi. Kwanza anaamini kuwa yeye ni tajili mkubwa na mwenye mabilioni ya pesa, wakati hana hata senti tano.
- Pili anaamini kuwa kasoma degree nne, (bachelor, masters, PhD, mpaka degree of science in medicine), wakati balozi aliyemrudisha TANZANIA alinukuliwa na gazeti moja akisema Dr shika alirudishwa nchini wakati akiwa hajamaliza MASTERS yake.
Nilitegemea Baada ya ile sarakasi yake pale mnadani, serikali ingemsaidia matibabu ya kisaikolojia, lakini kinyume chake amegeuzwa kuwa maarufu na umaarufu huu unanizisha tatizo lake kwa kiasi kikubwa. Kwanini nasema hivi
- Juzi kanukuliwa akisema amechaguliwa kuwa balozi umoja wa mataifa na hivi karibuni ataenda newyok katika kituo chake cha KAZI. lakini mpaka sasa hakuna uteuzi wa namna hiyo uliofanyika kwa mujibu wa tovuti ya UN na hata serikali yetu ya TANZANIA
-Katoa ahadi ya Dora Milioni moja kwa chuo cha wauguzi, huu ni muendelezo uleule wa bilionea hewa. lakini pia katoa ahadi ya kutoa scholarship kwa watoto maskini, na ahadi hii inaweza kuleta usumbufu mkubwa katika jamii
Kimsingi huyu Dr anahitaji kupelekwa REHAB na si kushangiliwa, kila anaposhangiliwa tatizo lake linaongezeka, na sitashangaa siku moja akienda ikulu na kujitangazia uongozi wa nchi, ndo hapo mtakaposhtuka.
Huyu Dr. Akamatwe mara moja na kusaidiwa , REHAB ni mahala salama kwa Dr Shika na si VINGINEVYO