Opinion: Matokeo Mabaya ya Form IV, Jee?, Is It "Real?F" or there is a "Conspiracy Theory Behind?!.

Opinion: Matokeo Mabaya ya Form IV, Jee?, Is It "Real?F" or there is a "Conspiracy Theory Behind?!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Naomba kuanza kwa kudeclare interest, mimi ni mhanga wa matokeo haya mabaya ya Form IV, nilikuwa na vijana wangu wawili, ambao walichaguliwa kujiunga na shule za kata, wife akashauri tuwahamishie shule za maana, kwa vile mimi ni mtu wa Nyerere type, nikamgomea, kwa hoja kuwa maadam watoto wa wananchi wa kawaida, wanasoma shule hizo za kata kwa sababu hawana jinsi, lets watoto wetu wasoma shule hizo hizo za kawaida, "if they are bright, they are bright no matter wanasoma wapi!". Kiukweli kwa hili, tuligombana!.

Nikamhakikishia kuwa "the bright ones" from shule za Kayumba, are "the bright" in deed opposed to the "spoon fed brights" kutoka shule za Academy!. Nikawaeleza vijana wangu kwa nini siwahamishi, kwa kuzingatia nauelewa fika uthaufu wa shule za kata, hivyo niliwahakikishia "to make up!". Nikamshawishi wife kuwa hizi shule za Academy, ujanja ni lugha tuu na kutafuniwa kila kitu, wao kazi yao ni kumeza tuu, na mwisho wa kutafuniwa ni shule, wakifika chuo kikuu, huwa wanakimbizwa sana na watoto waliosoma Kayumba!. Mimi mwenyewe nimesoma shule za UPE enzi zile, nimeshuhudia wanafunzi wa academy wakiishia njiani baada ya kutinga pale UD!.

Baada ya kufanya mitihani, wote wawili walituhakikishia Div 1 zisizo na mawaa!, wakasema kwa jinsi walivyoiona mitihani hiyo na jinsi walivyoifanya, "there is no way, watakosa first class!, matokeo yametoka, "No first class!", na kwa shule zao, first class ni nil!, yaani hakuna!.

Nimekaa na vijana wangu kutathmini kilichotokea, vijana wangu, wamenigomea kata kata kuwa "there is something wrong!" kwenye usahihishaji, hayo sio matokeo yao!. Wa kwanza yeye ndiye aliyekuwa kipanga wa somo la hesabu shuleni kwao, siku ya mahafali, alitunukiwa cheti na zawadi za ubingwa wa somo la hesabu!. Kijana huyu amepata C ya hesabu!, akaniambia "Dady, hata kama ningepata F, masomo mengine yote, ningekubali, lakini sio C ya` hesabu!. Akanihakikishia kama kuna jinsi ya kuomba aonyeshwe mtihani wake, anaomba aonyeshwa kwa sababu haamini hata kidogo kwa sababu majibu ya hesabu ni majibu ya uhakika, ana uhakika alivyoujibu mtihani ule, yeye ana A ya Hesabu!.

Huyu mwingine, yeye alikuwa kipanga wa somo la Fizikia na ndiye aliyeongoza kwa kutwaa zawadi ya jumla ya Fizikia kwenye mahafali yake ya kidato cha nne. Yeye amepata D ya Fizikia, naye anadai, haamini!. Huyu wa Physics simwamini sana, ila kijana wangu wa Math, namuaminia, hivya nami naamini, "there was something wrong some where kwenye usahihishaji!".

Baada ya kuwaza haya ya yale, nikakumbuka lile sakata la kushinikiza Ndalichako ajiuzulu. Inawezekana usahihishaji ni ule ule ila matokea mazuri hupatikania kwenye standardization ili kuzinusuru baadhi ya shule, zisizungushe jumla!. In retaliation ya "kile cha mwaka jana", Bi. Joyce Ndalichako, akaamua kuhakikisha kuwa kumbe "hawa jamaa" walikuwa wakipata wanachokipa kwa kuhurumiwa tuu!, sasa hakuna huruma tena!, NECTA ikakaza mkanda mpaka tundu la mwisho ili kuwakomesha na kuwakomoa wale waliokuwa wakihurumiwa na mwisho wa siku kupiga kelele za kuonewa!.

Fanyeni utafiti wa shule zilizozungusha jumla ziko maeneo gani, na fanyeni utafiti wa wale wanafunzi asilimia 60 waliozungusha ni kina nani wanaosubiri kuingia mitaani na kuishia kuwa vibaka!. Fanyeni utafiti wahalifu wengi ni watu wa aina gani?, waliojaa magerezani ni kina nani, masikini wengi wa kutupwa ni kina nani? etc etc!.

Mtakuwa very much surprised kugundua kumbe wengi wa waliopata kuanzia DIV I-III ni watu fulani na wengi wa waliopata Div IV na kuzungusha ni watu fulani!. Sasa NECTA imefanya hivyo ili kuwakomoa, katika kuwakomoa, inadhani inamkomoa nani?!. Hao asilimia 60 waliozungusha unadhani shughuli yao kubwa sasa itakuwa nini?.

Serikali lazima iingilie kati hali hii, vinginevyo huko tuendako wengi wa wenye nacho, watakuwa ni watu fulani, na wengi wa wasionacho watakuwa kina fulani!, utafikia wakati, wasionacho watajiorganize na kuwanyanganya walionacho na ikibidi wanaweza kuamua kufanya chochote kwa walionacho ili wote tukose!.

Nazungumza haya kwa uchungu sana, kwa sababu nimeguswa!.

Nimemkumbuka sana Nyerere!.

Pasco.

Pasco wa jf ni baba wa watoto 6, watano kati yao wanasoma sekondari za kata!.
 
Ndugu shule ni muendelezo wa kila hatua mwanafunzi anayopitia, wote tunashuhudia usanii unaofanywa kwa darasa la saba na form 2 kuna wanafunzi wasio stahili kuendelea na shule wanapitishwa ili kufurahisha wananchi wakati wenzao wa NECTA wapo kazini kuhakikisha wanatoa stahili kwa kila mwanafunzi, miaka ya nyuma ilikuwa kila mwanafunzi alikuwa makini kwa kila hatua akijua kabisa akifanya masihara anabaki, huo wengi wa ziro ni matakoe ya mrundikanao wa wasio na sifa wanakuja kuchunjwa na NECTA, why baada ya wanafunzi kupita form 4 huko form 6huwa hakuna kufeli kwa wengi sana
Na hata kama kuna kitu kimefanywa na NECTA mwanafunzi wa A hawezi pata F angalau atapata C hata wewe umeshuhudia kwa vijana wako
 
Nyumba isiyo na msingi imara ni rahisi kuanguka. Kwanza tuangalie mfumo wetu toka shule za msingi. Hivi kweli hawa Watoto hadi wanapata 0 kidato Cha nne matokeo yao ya darasa la kwanza hadi la saba yalikuwaje? Matokeo ya kidato Cha kwanza hadi Cha tatu nayo yalikuwaje? Ama kulikuwa na udanganyifu wa maendeleo ya mwanafunzi huyu au kuna matatizo ya USIMAMIZI wa mfumo. Kifupi mfumo ulipaswa kumrekebisha mwanafunzi aliyepata ziro ama kurudia au mwanafunzi kuacha shule. Lazima kama taifa turudi kwenye mstari.
 
Tatizo hapa ni ufisadi. Watoto wa vigogo wanasoma shule binafsi na kwa hiyo waalimu wametelekezwa hawana masilahi wanauza vitumbua madarasani. Mwanafunzi hasahihishiwi daftari mpaka anunue biashara ya mwalimu. Hilo ni moja, lakini la pili ni utandawazi watoto kutwa kwenye tv, facebook, na kuchat kwenye simu, usiku wako clabu na starehe nyingine; Hasa Clouds wanaeneza sana uchafiu huu utasikia after school bash, sijui nini tena na nini yani wanalenga kuvuruga vitoto. Hebu iwe marufuku ya kiserikali wanafunzi kuangalia tv, kuwa na simu, kwenda klabu na maeneo ya starehe na vyombo vya usimamizi viundwe.
 
Ni ajabu kwa Mtanzania kushangaa Matokeo ya Mtihani wa kidato cha nne kama yalivyotoka.Mamabo yako wazi tangu Taifa hili lilipoamua kuendesha kila kitu kwa njia za Siasa.Kwa nini ushangae kufeli kwa wanafunzi wa Shule za Umma ili hali wale wote walioko Serikali ambao ndiyo wanaosimamia Shule hizo walishaona tatizo hilo na kuhakikisha Watoto wao hawaendi kusoma katika Shule hizo?.Hebu kaa chini na tumia muda wako kidogo ufikirie ukianzia Mwalimu anayemfundisha Mwanao katika Shule za Serikali kama je anavyovigezo kwa maana ya Elimu ya kutosha kuwa Mwalimu?,je Mazingira ya kazi zake yanampa fursa ya kuwa na muda mzuri kwa kujiandaa na Shughuli zake?.Je Serilikali inafanya juhudi za dhati kuboresha Elimu kama si tu za kulidhisha Wafadhili ili waendelee kuipa Misaada ambayo nayo inafisadiwa?.Kwangu Mimi tatizo la Matokeo haya naliona kama limechangiwa kwa kiwango kikubwa na Wazazi wa Taifa hili kwa kukwepa au kushindwa wajibu wao wa kusimamia haki za Watoto wa Taifa hili.Ni Wazazi hawa amabao inapofika nyakati za Uchaguzi wanauza Haki ya Watoto wao kupata Elimu bora kwa kupokea vizawadi kama Tshirt,Chumvi,viberiti,vibaragashia na Khanga na Kuchagua viongozi wanaoangamiza Taifa hili kama inavyojidhihilisha katika Matokeo haya.Aibu ya Matokeo haya ni ya nchi nzima wala haiishii tu kwa Wazazi wa Watoto bali ni kwa kila anaeamini kuwa ni Mtanzania kwani kwa hali hii hakuna Mtanzania anayeweza kusimama kwenye jumuiya ya Kimataifa akaaminika katika Masuala ya kitaaluma.Wapigieni makofi Maspika,Mawaziri ,Wabunge na Wakuu wa nchi huku Taifa likiangamia.
 
Tatizo lipo katika mfumo wote wa elimu,walimu wa shule za Serikali walishajikatia tamaa,wanafundisha ili muradi tu.Mtoto anayesoma shule ya kata kwa miezi sita unakuta ameandika notisi hata hazifiki kurasa kumi nenda kachukue daftari ya mtoto wa Private iliyo serious unakuta ameandika daftari zima.Hizi shule za kata unakuta hawana mwalimu wa biology mpaka aje mwanachuo wakati wa field awafundishe.Atakapofanya mtihani wa yale machache aliyofundishwa lazima yule aliye serious ataongoza wenzake.Kule Private schools wanaweka wastani wa kila mwanafunzi kuufikisha asipofikisha anarudishwa,Pia wanalazimishwa kujisomea kila jioni na alfajiri na unakuta masomo yote yana waalimu wa kutosha,darasa lina wanafunzi wachache(mara nyingi hawazidi 40) kiasi kwamba kila mwalimu anamtambua mwanafunzi wake,topics zote huwa zinafundishwa na kumalizwa na unakuta kila mwezi kuna mitihani ya kuwapima wanafunzi.
Sasa kama unampeleka mwanao shule ya kata itakubidi umpeleke tuition iliyo serious maana si kila tuition centre ni nzuri ili akahakikishe anaisoma sylabus yote,na pia kwenda kufanya majaribio ya kila jumamosi na hata watoto wengine huchukua na kukopi notisi za wenzao wakati wa likizo kwa kweli inahitaji nguvu za ziada zaidi kutafuta zaidi ya kile wanachokipata shuleni
Muhimu kwa Serikali kuyaboresha maslai ya walimu kwani wao ndio washika mpini.Waalimu wa Private schools wanalipwa vizuri kulinganisha na wenzao wa serikalini.
 
Pole Pasco yaani ningejua huja baadae kama majuto. Ungejua ungesikiliza ushauri wa mkeo. Shule za kata ni janga nyingi hazina mahitaji na mazingira mazuri ya watoto kujifunzia. Ingawaje watoto wachache wanachomoka na div. 1&11. Kama taifa yatupasa tutafakari, tujadili na kuchukua hatua. Kuhusu watoto wako kuwa walikuwa wanafanya vema shule tofauti na NECTA results yawezekana walikuwa wanaongoza watoto waliokuwa na uwezo duni kwa level ya hiyo shule.
 
Last edited by a moderator:
Wanabodi,

Naomba kuanza kwa kudeclare interest, mimi ni mhanga wa matokeo haya mabaya ya Form IV, nilikuwa na vijana wangu wawili, ambao walichaguliwa kujiunga na shule za kata, wife akashauri tuwahamishie shule za maana, kwa vile mimi ni mtu wa Nyerere type, nikamgomea, kwa hoja kuwa maadam watoto wa wananchi wa kawaida, wanasoma shule hizo za kata kwa sababu hawana jinsi, lets watoto wetu wasoma shule hizo hizo za kawaida, "if they are bright, they are bright no matter wanasoma w


wasaidie hao watoto wakate rufaa .paper zao zitasahishwa upya in their presence.
 
Pasco ungetutajia watoto wako wamepata div gani ingenogesha stori yako zaidi. Wacha na mimi ninukuu baadhi ya wanaphilosofia waliobobea. "Ex Africa aliquid novi" hii ni kauli ya phtolemy (tamka tolemi) ikimaanisha kila kukicha kitatokea kioja kingine barani Afrika, na hili la matokeo ni kioja kingine. Plato naye hakusita kuiasa jamii pale aliposisitiza hili " volenti non fiti enjuria" yaani la kujitakia halina madhara...kwa upande wa elimu hili suala ni la kujitakia. Aristotle alihamasisha tendo la kujifunza na kufunzwa miongoni mwa wanaojifunza kwa kuhimiza hivi " lipitison esti matel stadium" yaani kurudia rudia ndio mama wa kusoma....je vijana wetu wa leo (.com) wanalijua hili?. Hizo nukuu ni point of reference na zinaweza kutusaidia endapo kweli tunataka kuwa na jamii iliyoelimika na yenye kuleta changamoto za kimaendeleo nchini kwetu. Mungu ibariki Tanzania.
 
Last edited by a moderator:
haya umechangia wewe mzazi, mzazi serious hufanyi majaribio kwenye elimu. ukiona elimu ni ghali jaribu ujinga, watoto hao watakulaumu hadi kufa, usirudie tena siku nyingine. hata bado kuna nafasi wapeleke F 5 kasha warudie masomom waliyofeli.
 
pasco mimi ni professional mwalimu na nafundisha shule ya kata naelewa situation y shule zetu zilivyo. unaweza kulaumu baraza lakini nakuhakikikshia mwanafunzi wa shule ya kata hawezi kulinganishwa na mwanafunzi wa marian school. shule zetu hazina vifaa vya kumfanya mtoto awe creative na kwa kiasi kikubwa anamtegemea mwalimu kwa asilimia zaidi ya 99. so mwalimu akiamua kwenda kupiga stori class imekula kwa mwanafunzi na walimu sasa tumeamua kufanya kazi inayolingana na mshahara wetu bado inakula kwa mwanafunzi.
KAMA UNA UWEZO WA FEDHA PELEKA WATOTO SHULE NZURI ACHA KUCHEZEA FUTURE ZA WANAO.
 
Pole Pasco yaani ningejua huja baadae kama majuto. Ungejua ungesikiliza ushauri wa mkeo. Shule za kata ni janga nyingi hazina mahitaji na mazingira mazuri ya watoto kujifunzia. Ingawaje watoto wachache wanachomoka na div. 1&11. Kama taifa yatupasa tutafakari, tujadili na kuchukua hatua. Kuhusu watoto wako kuwa walikuwa wanafanya vema shule tofauti na NECTA results yawezekana walikuwa wanaongoza watoto waliokuwa na uwezo duni kwa level ya hiyo shule.
,
Mkuu Githe', hebu nisome in between the lines hapa
Wa kwanza yeye ndiye aliyekuwa kipanga wa somo la hesabu shuleni kwao, siku ya mahafali, alitunukiwa cheti na zawadi za ubingwa wa somo la hesabu!. Kijana huyu amepata C ya hesabu!, akaniambia "Dady, hata kama ningepata F, masomo mengine yote, ningekubali, lakini sio C ya` hesabu!. Akanihakikishia kama kuna jinsi ya kuomba aonyeshwe mtihani wake, anaomba aonyeshwa kwa sababu haamini hata kidogo kwa sababu majibu ya hesabu ni majibu ya uhakika, ana uhakika alivyoujibu mtihani ule, yeye ana A ya Hesabu!.
.

The subject in question is math. Kama 1+1=2 then that is it!, ukiandika hivyo ukaambiwa umekosea, then the best way is to see uliandikaje, unaweza kujidhania uliandika 1+1=2, kumbe what you actual did is 1+1=11!.

Kitu ambacho nakikubali, ni kweli vijana wangu niliwaona bright na ni kweli walikuwa wakiongoza madarasani kwao, lakini kumbe wao ndio waliokuwa vipanga wa vibonde!, lakini ukiwa kipanga wa hesabu, ni kipanga tuu wa hesabu, kwenye hesabu, hakuna kipanga wa vibonde wala wa vichwa!.
Pasco.
 
haya umechangia wewe mzazi, mzazi serious hufanyi majaribio kwenye elimu. ukiona elimu ni ghali jaribu ujinga, watoto hao watakulaumu hadi kufa, usirudie tena siku nyingine. hata bado kuna nafasi wapeleke F 5 kasha warudie masomom waliyofeli.
.
Mkuu Lidongo, mimi nimetoka familia ya watoto 8 na hakuna yoyote kati yetu aliyesoma shule ya kulipia!. Mimi I have six!, nami nikaweka msimamo, kuwa na mimi sitalipia mtoto yoyote shule ya kulipia!, asipopasi basi!, end of bussiness na baba, wangelipiwa na mama!. Vijana wangu walitaraji kupata DivI, hakuna aliyepata, sijasema wamefeli, wala hawana somo lolote la kurudia!, ugomvi ni kichwa wangu wa hesabu kapata C, haamini!.
Pasco.
 
pasco mimi ni professional mwalimu na nafundisha shule ya kata naelewa situation y shule zetu zilivyo. unaweza kulaumu baraza lakini nakuhakikikshia mwanafunzi wa shule ya kata hawezi kulinganishwa na mwanafunzi wa marian school. shule zetu hazina vifaa vya kumfanya mtoto awe creative na kwa kiasi kikubwa anamtegemea mwalimu kwa asilimia zaidi ya 99. so mwalimu akiamua kwenda kupiga stori class imekula kwa mwanafunzi na walimu sasa tumeamua kufanya kazi inayolingana na mshahara wetu bado inakula kwa mwanafunzi.
KAMA UNA UWEZO WA FEDHA PELEKA WATOTO SHULE NZURI ACHA KUCHEZEA FUTURE ZA WANAO.
Mkuu Mwalimu Fidelity, nimekuelewa lakini mimi ugomvi wangu ni somo moja tuu la hesabu!, nalo lilihitaji, vifaa, maabara au creativity?. Sisi wengine ni Nyerere type, watoto wetu watasoma shule wa Watanzania makabwela watakazosoma!. Mwaka nilioingia chuo, UD, shule fulani ya wasichana iliiongoza darasa zima walipiga div I na nusu yao tukaingia nao darasa moja!, walianza 18, waliomaliza ni 8!. Hivyo vijana wangu wote wawili watakwenda Form V tena shule hizo hizo za serikali!. Nashukuru japo Mungu amenipa uwezo wa kuwalipia private, lakini sitawalipia!. Kama mimi ni mwananchi, watoto wangu ni watoto wa mwananchi!.
Pasco.
 
,
Mkuu Githe', hebu nisome in between the lines hapa
.

The subject in question is math. Kama 1+1=2 then that is it!, ukiandika hivyo ukaambiwa umekosea, then the best way is to see uliandikaje, unaweza kujidhania uliandika 1+1=2, kumbe what you actual did is 1+1=11!.

Kitu ambacho nakikubali, ni kweli vijana wangu niliwaona bright na ni kweli walikuwa wakiongoza madarasani kwao, lakini kumbe wao ndio waliokuwa vipanga wa vibonde!, lakini ukiwa kipanga wa hesabu, ni kipanga tuu wa hesabu, kwenye hesabu, hakuna kipanga wa vibonde wala wa vichwa!.
Pasco.
Kukata rufaa na kusahihishwa upya inakubaliwa,hivyo ili kujiridhisha fanya hivyo.Lakini bado nadhani shuleni pale kuna baadhi ya topics hazikufundishwa hata kama ni maswali matatu,kitu ambacho kilipelekea huyu mtoto kuanguka.
 
Pasco,tatizo siyo hao vijana wako,tatizo walimu.Hata kama somo la hisabati halihitaji maabara,jiulize walikuwa na vitabu vya kiada vya hesabu vya kutosha?Mwalimu wa hesabu aliwafundisha vizuri?Na wa fizikia je?

Uzuri wa hesabu ni kujumlisha,kutoa,kuzidisha na kugawanya,tatizo formula walizijua zote?Au walifundishwa maswali na majibu kutoka mitihani iliyopita?

Umwandishi wa habari na sababu umekuwa mmoja wa waadhirika wa janga la elimu anza sasa kupiga kelele na kalmu yako wasaidie walimu kupiga kelele ili wapate mafao mazuri na wawafundishe watoto wa taifa hili vizuri,na iwe kama zamani shule za serikali zilikuwa zinang'ara leo zinatia aibu.
 
Back
Top Bottom