Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Naomba kuanza kwa kudeclare interest, mimi ni mhanga wa matokeo haya mabaya ya Form IV, nilikuwa na vijana wangu wawili, ambao walichaguliwa kujiunga na shule za kata, wife akashauri tuwahamishie shule za maana, kwa vile mimi ni mtu wa Nyerere type, nikamgomea, kwa hoja kuwa maadam watoto wa wananchi wa kawaida, wanasoma shule hizo za kata kwa sababu hawana jinsi, lets watoto wetu wasoma shule hizo hizo za kawaida, "if they are bright, they are bright no matter wanasoma wapi!". Kiukweli kwa hili, tuligombana!.
Nikamhakikishia kuwa "the bright ones" from shule za Kayumba, are "the bright" in deed opposed to the "spoon fed brights" kutoka shule za Academy!. Nikawaeleza vijana wangu kwa nini siwahamishi, kwa kuzingatia nauelewa fika uthaufu wa shule za kata, hivyo niliwahakikishia "to make up!". Nikamshawishi wife kuwa hizi shule za Academy, ujanja ni lugha tuu na kutafuniwa kila kitu, wao kazi yao ni kumeza tuu, na mwisho wa kutafuniwa ni shule, wakifika chuo kikuu, huwa wanakimbizwa sana na watoto waliosoma Kayumba!. Mimi mwenyewe nimesoma shule za UPE enzi zile, nimeshuhudia wanafunzi wa academy wakiishia njiani baada ya kutinga pale UD!.
Baada ya kufanya mitihani, wote wawili walituhakikishia Div 1 zisizo na mawaa!, wakasema kwa jinsi walivyoiona mitihani hiyo na jinsi walivyoifanya, "there is no way, watakosa first class!, matokeo yametoka, "No first class!", na kwa shule zao, first class ni nil!, yaani hakuna!.
Nimekaa na vijana wangu kutathmini kilichotokea, vijana wangu, wamenigomea kata kata kuwa "there is something wrong!" kwenye usahihishaji, hayo sio matokeo yao!. Wa kwanza yeye ndiye aliyekuwa kipanga wa somo la hesabu shuleni kwao, siku ya mahafali, alitunukiwa cheti na zawadi za ubingwa wa somo la hesabu!. Kijana huyu amepata C ya hesabu!, akaniambia "Dady, hata kama ningepata F, masomo mengine yote, ningekubali, lakini sio C ya` hesabu!. Akanihakikishia kama kuna jinsi ya kuomba aonyeshwe mtihani wake, anaomba aonyeshwa kwa sababu haamini hata kidogo kwa sababu majibu ya hesabu ni majibu ya uhakika, ana uhakika alivyoujibu mtihani ule, yeye ana A ya Hesabu!.
Huyu mwingine, yeye alikuwa kipanga wa somo la Fizikia na ndiye aliyeongoza kwa kutwaa zawadi ya jumla ya Fizikia kwenye mahafali yake ya kidato cha nne. Yeye amepata D ya Fizikia, naye anadai, haamini!. Huyu wa Physics simwamini sana, ila kijana wangu wa Math, namuaminia, hivya nami naamini, "there was something wrong some where kwenye usahihishaji!".
Baada ya kuwaza haya ya yale, nikakumbuka lile sakata la kushinikiza Ndalichako ajiuzulu. Inawezekana usahihishaji ni ule ule ila matokea mazuri hupatikania kwenye standardization ili kuzinusuru baadhi ya shule, zisizungushe jumla!. In retaliation ya "kile cha mwaka jana", Bi. Joyce Ndalichako, akaamua kuhakikisha kuwa kumbe "hawa jamaa" walikuwa wakipata wanachokipa kwa kuhurumiwa tuu!, sasa hakuna huruma tena!, NECTA ikakaza mkanda mpaka tundu la mwisho ili kuwakomesha na kuwakomoa wale waliokuwa wakihurumiwa na mwisho wa siku kupiga kelele za kuonewa!.
Fanyeni utafiti wa shule zilizozungusha jumla ziko maeneo gani, na fanyeni utafiti wa wale wanafunzi asilimia 60 waliozungusha ni kina nani wanaosubiri kuingia mitaani na kuishia kuwa vibaka!. Fanyeni utafiti wahalifu wengi ni watu wa aina gani?, waliojaa magerezani ni kina nani, masikini wengi wa kutupwa ni kina nani? etc etc!.
Mtakuwa very much surprised kugundua kumbe wengi wa waliopata kuanzia DIV I-III ni watu fulani na wengi wa waliopata Div IV na kuzungusha ni watu fulani!. Sasa NECTA imefanya hivyo ili kuwakomoa, katika kuwakomoa, inadhani inamkomoa nani?!. Hao asilimia 60 waliozungusha unadhani shughuli yao kubwa sasa itakuwa nini?.
Serikali lazima iingilie kati hali hii, vinginevyo huko tuendako wengi wa wenye nacho, watakuwa ni watu fulani, na wengi wa wasionacho watakuwa kina fulani!, utafikia wakati, wasionacho watajiorganize na kuwanyanganya walionacho na ikibidi wanaweza kuamua kufanya chochote kwa walionacho ili wote tukose!.
Nazungumza haya kwa uchungu sana, kwa sababu nimeguswa!.
Nimemkumbuka sana Nyerere!.
Pasco.
Pasco wa jf ni baba wa watoto 6, watano kati yao wanasoma sekondari za kata!.