Sungi
Senior Member
- Apr 29, 2009
- 149
- 47
- Thread starter
- #21
Sungi,
Mkuu wangu kidogo unakosea hapa.. Mambo mengi yaliyomo humu JF hayahusiani wala kutokana na NCHI yetu..Hakuna mtu anayetegemea tanzania imfikishe mahala ila sisi ndio tutaijenga Tanzania ya kesho!..
Kwa mfano maneno ya Kennedy kuhusiana na hotuba yake "Ask not what the Country can do for You' yana mapana zaidi ya policies. Na sidhani kama Mwanakijiji au mtu yeyote humu anauliza nchi yake itamfanyia kitu gani ila wanazungumzia empty promises za chama tawala. Hivyo Country na Policies za chama tawala ni vitu viwili tofauti kabisa.
Hotuba ya Kennedy ilikuwa kuhamasisha wananchi kwamba US ni nchi yenye Opportunity kibao na policies zake zilikuwa zikiwezesha sera na ahadi ambazo zilimpa kura (Kennedy) hivyo aliwataka wananchi kujiunga naye kuijenga nchi.. kwa maana nyingine wananchi wawe na imani na dira, policies na sera zake, kilichobakia ni nguvu zao wananchi wenyewe kuiendeleza nchi na masiha yao wenyewe.
Hivyo mkuu wangu tusichukulie hotuba kama hizi juu juu tu kwani huwezi kuitendea haki nchi yako ikiwa policies zake zinawafunga wananchi. Maneno kama ya Kennedy hata Mugabe au Kim wa North Korea anaweza kuyatumia kwa kutazama malengo yavyama vyao na ikaleta maana, lakini ukweli unabakia kuwa policies zilizopo nchi hizo haziwezi kabisa kutimiza malengo yanayokusudiwa vichwani mwa wananchi...ndipo majukwaa kama haya huingia kati kuchambua makosa ya Policies na sio mazingira ya nchi waliyomo.
Sijui kama umenipata!
You have a point ... maswala haya ni mapana kiasi, pengine majibu ya sentensi kadhaa haitoshi kuelezea. This is a good debate!