OR - TAMISEMI muondoeeni Dr. Fatuma Ramadhan Mganga Mke wa Spika Ndugai kuwa DED - BAHI DC

OR - TAMISEMI muondoeeni Dr. Fatuma Ramadhan Mganga Mke wa Spika Ndugai kuwa DED - BAHI DC

Wewe na spika nani jobless
Spika ana kazi gani kama siyo kuharibu nchi? Unaona wanavyomgeuka Magufuli kabla hata jogoo hajawika. Walimdanganya na upambe mpaka corona ikampaya na kumuua maskini na mara hii wameshamgeuka. Huyu hana kazi yoyote ni mharibifu ambaye alitakiwa asiwepo.
 
sanasana atapewa barua ya onyo kwa mdomo na next uteuzi watampooza kwazawadi ya u-RC
 
Uzuri mama anajua wanafiki wote hana haja kutajiwa majjna huoni Jobless anavyojikomba ?
 
Kwani ana wake wawili? Niliwahi kusikia mke wake anafanya kazi NIMRI huku Dar
 
Hii sasa ni personification...Kama Huyo Mkurugenzi kaharibu toeni mambo aliyoharibu ila kumhusisha Speaker na haya ni kuleta uonevu...Kwani mke wa speaker hana haki ya kufanya kazi? Yeye ni raia kama wengine haki zake kwanini anayng'anywe kwakua ni mke na akikosa kwanini asiadhibiwe kwa sheria na taratibu zilizopo?

Tuache hizi chuki na kuhusianisha watu na makosa ya mtu mwingine. Kila raia ana haki ya kupendwa, haki ya kulindwa na haki ya kufanya shughuli halali za kumpatia kipato ikiwapo kupata cheo...Ni haki ya msingi ya kila raia wa Tanzania. Akikosa aadhibiwe kwa kosa lake na siyo kwa hizi sweeping statements
 
Kwa wanaomfahamu huyo mama kwanza alitakiwa hata awe Katibu Mkuu siyo tu Mkurugenzi. She has records both in academics na hata practically...Kama kuna hasara ya pesa hilo ni kosa lingine na ahukumiwe kwa hilo, lakini kwa competence, she is very competent and intelligent
 
OR - TAMISEMI kwa heshima kubwa nawashauri mumuondoe mara moja Mke wa Spika Y. Ndugai kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya BAHI, MKOA WA DODOMA. Mama huyu, Dr. Fatuma Ramadhan Mganga anatumia uhusiano wake wa kifamilia na Job Ndugai kukwaza utendaji kazi wa Serikali. Mama huyu kwa sababu ya kuwa Mke wa Spika, anaharibu taswira nzima ya uwajibikaji kuanzia kwa mabosi wake kwa maana ya RC, RAS na hata DC.

Mwenendo wa Job Ndugai katika masuala ya TAMISEMI unategemea huyu mama anasema nini. Mama huyu amemshika kwelikweli Job kiasi cha kwamba JOB yupo tayari kuharibu kazi ya mtu ili kumtetea mkewe ambaye utendaji wake BAHI ni wa hovyo hovyo.

La mwisho niZITAKE mamlaka za Serikali kuhakikisha zinaondoa mgongano wa kimaslahi kwa viongozi wa juu wa Nchi na wana familia zao. Ni sharti muhimu na adhimu kabisa kwa viongozi wa mihimili ya Dola wenza wao wasipewe majkumu ambayo kwa namna moja au nyingine wakati wa kuchukua uamuzi kutakuwa na maslahi.

Msimuamini JOB hata kidogo, huyu anaongozwa na maslahi ya muda.
Mke wa Ndugai ni mkristo na anasali kwa askofu Gamanywa.

Niishie hapo!
 
Aisee ndiyomaana alikua hata akitaka kuunda kamati za bunge anaomba kwanza ushauri kwa Marehemu Pombe
 
Bro usiitumie JF kwa maslahi yako binafsi
Heshimu watu
Haikusaidii kuchafua watu namna hii
Mwogope Mungu usiumize familia za watu kumbuka unayemsakama hapa ni baba au mama mwenye watoto na ana ndugu pia
Mwenyezi Mungu akupe amani ya moyo wako
Pole kwa uliyokwazika nayo lakini hii si njia nzuri kuonesha hisia zako unawaumiza wasiostahili adhabu hii
Asante
 
Acha ushabiki. Job ndugai ni Spika, ni Kamati ipi ya Bunge itakuwa na uwezo wa kumchukulia hatua mkewe ambaye ni DED na Spika ndiye anayepanga Wabunge kwenye Kamati. Maadili ya kazi tu yangetosha kumtaka huyo mama akae pembeni. Naamini wenye Uamuzi wanajua nini cha kufanya na watakifanya soon kwa ufasaha.
 
Wala sina ushabiki bro nimekushauri tu
 
Back
Top Bottom