OR - TAMISEMI muondoeeni Dr. Fatuma Ramadhan Mganga Mke wa Spika Ndugai kuwa DED - BAHI DC

Wewe na spika nani jobless
Spika ana kazi gani kama siyo kuharibu nchi? Unaona wanavyomgeuka Magufuli kabla hata jogoo hajawika. Walimdanganya na upambe mpaka corona ikampaya na kumuua maskini na mara hii wameshamgeuka. Huyu hana kazi yoyote ni mharibifu ambaye alitakiwa asiwepo.
 
sanasana atapewa barua ya onyo kwa mdomo na next uteuzi watampooza kwazawadi ya u-RC
 
Uzuri mama anajua wanafiki wote hana haja kutajiwa majjna huoni Jobless anavyojikomba ?
 
Kwani ana wake wawili? Niliwahi kusikia mke wake anafanya kazi NIMRI huku Dar
 
Hii sasa ni personification...Kama Huyo Mkurugenzi kaharibu toeni mambo aliyoharibu ila kumhusisha Speaker na haya ni kuleta uonevu...Kwani mke wa speaker hana haki ya kufanya kazi? Yeye ni raia kama wengine haki zake kwanini anayng'anywe kwakua ni mke na akikosa kwanini asiadhibiwe kwa sheria na taratibu zilizopo?

Tuache hizi chuki na kuhusianisha watu na makosa ya mtu mwingine. Kila raia ana haki ya kupendwa, haki ya kulindwa na haki ya kufanya shughuli halali za kumpatia kipato ikiwapo kupata cheo...Ni haki ya msingi ya kila raia wa Tanzania. Akikosa aadhibiwe kwa kosa lake na siyo kwa hizi sweeping statements
 
Kwa wanaomfahamu huyo mama kwanza alitakiwa hata awe Katibu Mkuu siyo tu Mkurugenzi. She has records both in academics na hata practically...Kama kuna hasara ya pesa hilo ni kosa lingine na ahukumiwe kwa hilo, lakini kwa competence, she is very competent and intelligent
 
Mke wa Ndugai ni mkristo na anasali kwa askofu Gamanywa.

Niishie hapo!
 
Aisee ndiyomaana alikua hata akitaka kuunda kamati za bunge anaomba kwanza ushauri kwa Marehemu Pombe
 
Bro usiitumie JF kwa maslahi yako binafsi
Heshimu watu
Haikusaidii kuchafua watu namna hii
Mwogope Mungu usiumize familia za watu kumbuka unayemsakama hapa ni baba au mama mwenye watoto na ana ndugu pia
Mwenyezi Mungu akupe amani ya moyo wako
Pole kwa uliyokwazika nayo lakini hii si njia nzuri kuonesha hisia zako unawaumiza wasiostahili adhabu hii
Asante
 
Acha ushabiki. Job ndugai ni Spika, ni Kamati ipi ya Bunge itakuwa na uwezo wa kumchukulia hatua mkewe ambaye ni DED na Spika ndiye anayepanga Wabunge kwenye Kamati. Maadili ya kazi tu yangetosha kumtaka huyo mama akae pembeni. Naamini wenye Uamuzi wanajua nini cha kufanya na watakifanya soon kwa ufasaha.
 
Wala sina ushabiki bro nimekushauri tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…