Hapa si bure, kwanini watu wale wale waliokuwa na wataokuwa (milele) wakimuunga mkono Bwana Mengi ndo hao hao wanaoponda TBC1, sasa naanza kuamini ile thread ya walio kwenye payroll inaukweli wake. Hao ze comedy kwa taarifa yenu wamechoka wenyewe wala hakuna anayewagusa.
Kama mnakumbuka wakati wakifanya marejeo ya funga mwaka, waliwahi kuonyesha baadhi ya stori zilizopigwa stop mfano ile ya kijana aliyekunywa dawa ya Mkuyati baada kuahidiana na demu matokeo yake demu kaingia mitini na dawa ikawa imekolea...wenyewe walidai ilipigwa chini kutokana na maadili na kweli watu wengi walilalamika baada ya kwenda hewani. Mi naanza kuwatilia wasi wasi watu wanaoingiza mkono TBC si bure.....nani asiyejua TBC ya sasa tofuati ya miaka hiyo. Hawa madogo wa ze comedy wanaendekeza sana starehe badala ya kazi ndo maana hawana jipya.
Zamani walikuwa wakitumiwa visa na watu kupitia email na hata kupigiwa simu, sasa hivi hawana email wala mawasiliano ya moja kwa moja na wahusika, wanatakiwa kukaa chini na kuweka mikakati mipya ya kukupata visa maana sasa wamekuwa wakibudi na kusikilizia kutoka kwenye magazeti yetu ambayo mengi sasa yamegeuka kuwa mipasho kama ya udaku mkubwa. Mtazamo wangu mimi nafikiri wale vijana wako fit ila wameishiwa mbinu za kupata mikasa, pia ukumbuke kuwa wale sasa ni celebrity si silahi kujichanganya na watu ovyo, cha msingi waunde timu ya watafiti kufuatilia kinachoendelea katika jamii na wao wabaki na umaarufu wao wa kuuza sura.
Kuhusu hoja ya tamaa ya pesa, haina mashiko wale wako kwenye business bwana ile sio NGOs....Mi nashauri tuache kubuni mambo kwa vile tunavyo yaona kwa nje, look for evidences.