Orijino Comedi - Sasa Kwisha

Orijino Comedi - Sasa Kwisha

Kuna dada yangu anaishi Namibia ameniambia hata kule wameanza kupata impression kwamba wanatumiwa kwenye ujinga sasa. Ole wao!
 
Yahh ni kweli kabisa nadhani jamaaa wanakosa kitu fulani hivi ambacho nadhani ni ujinga wao ndo unawafanya wasikijue, wanatumiwa kimtindo na mafisadi.... hawakosoi kama ile zamani walivyokuwa EATV hata kuchekesha hawachekeshi tena bora hata ya Futuhi wa star tv. siku hizi nikitaka kucheka nasubiri mizengwe ya kina zembwela ITV...
Jamaa wanaboa labda kucheza muziki
 
Mathalan ukilinganisha kipindi chao cha Alhamisi iliyopita na kile cha FUTUHI utaona ni kwa jinsi gani wameshuka kiwango. Kwenye kipengele cha mabomu ya Mbagala FUTUHI walitumia bongo zaidi kuliko Orijino Comedi. Kinachowasaidia kwa sasa ni Goodwill ambayo walishaitengeneza vinginevyo ni kwisha kabisa kidhana japo Mkwanja wanaudaka vilivyo
Asavali umegundua FUTUHI wamesha wafunika Orijino Comedi, ukitaka Comedy na mafunzo FUTUHI Star TV Alhamisi saa 3 usiku yaani wale wako juu enzi ya Joti na kuweka ****** ishapitwa, watafute Creativity Manager
 
The so called Orijino Komedi ni chombo cha mafisadi!! Kilichukuliwa hususan, kufanya kazi kipindi cha kampeni!!!! Kinafadhiliwa na Manji et al.......Ni mbinu za kiuhakika zilifanyika na wakaweza kukutoa EATV. sikuwahi kukuangalia, ila siku chache baada ya Mengi kutaja yale Mapapa Matano basi katika kubadilisha channel nikawa nimebonyeza button ya TBC1 (huwa sina mazoea kabisa na hii channel) basi nikakutana nao ndiyo wanaanza kipindi. Yaani ile preamble ilikuwa ni habari ya Mafisadi Papa kuwa ............unataka mafisadi papa kwani wewe ni nani.......matatizo yako yamekushinda..... mwingine anataka kutaja .....akamnyamazisha akimwambia funga mdomo usitaje jina......kwani wewe ni nani na utaje majina ya watu....). Kwa hapa yaleyale ambayo alikuwa yanasemwa na Rostam na Manji!!!!!!!

Zote hizi ni njaa zao!! Nasema hao the so called orijino komedi si wazalendo, ni vibaraka wa mafisadi tu.
 
Tusitake kuleta ligi ya ubishani usiokuwa na maana Orijino Komedi ya sasa si ile tuliyozoea kuiona EATV.Kwa kweli jamaa wamekosa ubunifu katika kiwango cha kutisha,hawana jipya zaidi ya kuvaa mavazi ya kike.Sipendi kuamini Orijino Komedi wamekwisha eti kwasababu wamehamia TBC1,nadhani vijana wamelewa sifa wakadhani hata wakituonyesha madudu yao bado wataendelea kupeta.
 
hehehehehe

kwi kwi kwi kwi unajua kitu ukisha kuwa na -ve impact hata ufanyaje huwezi kukipenda hawa ze commedy toka wahama channel 5 watu walisha anza kuhukumu tena humu humu. Unategemea nini kwa watu hao na ndo walewale leo hii wanakuja wanasema hawana jipya.
Mtakoma na huyo chuuuuuuuuuuura wenu.
 
ITV ya regianld abraham mengi
Suala c TV ya nani, kwani walivyokuwa EATV hiyo TV ni ya Nani? Ndugu co unakurupuka tu.. issue ni kwamba Orijino komedi hawana jipya... au we unasemaje?
 
Kinachotokea Origino Comedy ni yale yaliyotokea na gazeti la "RAI". Lilikuwa gazeti la kumulika jamii na kufichua uchafu unaoendelea serikalini..ghafla likabadilika lilipochukuliwa..
Ze comedy enzi watu walipenda maana lilikuwa linaonyesha na kufichua mabaya mambo ambayo sawa kwa njia ya vichekesho..na hilo kidogo lilisaidia kuwaweka sawa baadhi ya watu..
ila sasa sio siri...ni ile last part tu ndio inavutia..ya "mziki"..Kwingine hawaonekani tena kama wako upande wa wananchi
 
Ningewashauri wajitegemee. Wafungue ka-kampuni, wajisajiri COSOTA, halafu wawe wanarekodi vipindi na kuuza kwenye TV na CD kwa watu wa kawaida. Kwa kufanya hivyo ni vigumu kutumiwa. Hata hivyo, muelekeo wa sasa si mzuri kwani wakipoteza wateja (watazamaji) basi wamekwisha. maana siku manji akikasirika kama anavyowafanyiaga yanga basi na wao watakuwa "WAMEFULIA".
 
Hawa jamaa siku hiz wanaboa sana. Mi tangu walipoingia TBC1 sijaona kitu cha maana wanachokifanya, wametekwa na mafisadi nao wamegeuka kuwa mafisadi.
Wanapotakiwa kukosoa wao wanasifia, na wanapotakiwa kusifia wao wanakosoa. Zaidi hutasikia wakimsema Fisadi yeyote, utasikia wanamsifia tu.

Walianza na Dr. Slaa sasa wamemgeukia Mengi, HAWANA JIPYA, KWISHA KABISAAAAA!
 
Suala c TV ya nani, kwani walivyokuwa EATV hiyo TV ni ya Nani? Ndugu co unakurupuka tu.. issue ni kwamba Orijino komedi hawana jipya... au we unasemaje?

Kukurupuka ndio kawaida yangu kama haujajua bado, ukiniuliza kama wanalo jipya nitakuuliza kama hata wanalo hilo la zamani.AAAH kumbe na EATV ni ya Mengi? habari mpya hiyo post kwenye breaking news....
 
Hawa jamaa wanajimaliza wenyewe kwa ujinga wao. Mimi binafsi nilikuwa napenda sana kuangalia kipindi chao siku za nyuma, lakini siku moja nikasikia wanajitangaza kuwa wao ni Yanga (sababu tu wanapewa fedha na fisadi Manji anayewafadhili Yanga). Kwa kuwa mimi ni mkereketwa wa Simba niliwachukia mara moja. Mbaya zaidi, of late wamekuwa wakionyesha wazi kuwa wanatumiwa na mafisadi. Lakini sishangai kwani hata TBC yenyewe imeshatekwa na mafisadi. Ni Aibu!
 
Haya ni maono au mtizamo wa watu mlio kuwa mnapenda Ze commedy wawe wanarusha EAT au chanel 5 mbona vijana wapo juu na wanakula maisha na kuchekesha kama kawa mtaani wanakamata sana vichwa...nyie endeleeni na hoja zenu zaifu.


Unajhua ndugu yangu kundi kaMA Commedy aliko kwa ajili ya kuchekesha tu, bali pia na kuikosoa serikali na jamii kwa ujumla. Lakini kwakuwa sasa hivi wako chini ya TBC na TBC ni chombo cha Serikali, hakiwezi tena kuikosoa serikali. Watabaki kuongelea watu wadogowadogo hasa ile taarifa yao ya UMEFULIA! kwakweli haka kataarifa kao mimi binafsi kana-niboa! Unazungumzia Mtu fulani kaishiwa sasa hivi hapo zamani alikuwa na pesa, sasa kwani mtu kuishiwa kuna ajabu gani!? Yanaishiwa makampuni makubwa na watu maarufu duniani itakuwa hao wachezaji wa mpira wa zamani na waandishi wa magazeti sijui wa vitabu wa hapa TZ!!!

KWAKWELI WAMEISHIWA SASA.
 
Wapiganapo mafahari ziumiazo ni NYASI...... POLENI ZE COMMEDY ugomvi huu sio wa kwenu ni Maslahi ya biashara na kasheshe za WAPAMBE.

Mtajuuuuta kwafahamu VYURA HAWA......

Sipati picha oooh toka waondoke EATV eeeh bora MIZENGWE....... TUTAWATAMBUA KWA POSTING ZAO........

pigeni mzigo vijana achana na vyura hawa...
 
Nafikiri Tatizo la TBC1 ni kukosa Management yenye uwezo mzuri kichwani,Tido hana uwezo mzuri kiasi cha kuaminiwa hivyo,ni bahati yake kuwa aliweza ajiriwa BBC si kwa sababu ya uwezo wake kichwani ila ni kwa sababu ya Utangazaji wa lugha ya Kiswahili...Fuatilia mahojiano ya Tido na Watu mbalimbali hana uwezo mzuri wa kufikiri haraka.
 
wewe unaowabeza comedi orijino ni FISADI NYANGUMI kwani vijana hawa bado wanaendelea kuelimisha,kufundisha,kuburudisha hata kuchekesha... inaonekana wewe mwenye mada unawachukia sana kwani umetumwa na FISADI mengi. hebu tuweke wazi ni mambo yapi yanayokukera na yamerushwa lini? ikumbukwe usiwe unalopoka lopoka hovyo kama mengi fisadi. kwanza inmaonekana wewe siyo mfuatiliaji wa hicho kipindi ndiyo maana unalaumu tu.kafe mbele kama fisadi mwenzio mmengi atakavyopelekwa mahakamani . usiwe unatumwa tumwa kama huna kazi ya kufanya ndani ya huu mtandao kuna sehemu unaweza ukatuma cv yako utapata kazi ya kufanya. TUZUNGUMZE MAMBO YA MSINGI UMESIKIA WEWE FISADI.
 
Hivi jamani hamna mtu ambae anaweza kuwashauri hawa original comedi kuwa wanakoelekea sio?Binafsi nilishaacha kuzngalia siku nyingi sana kwa sababu sioni la maana,Jamani kama yupo ambae anaweza kukaa nao na kuwaeleza kuwa viwango vyao vimeshuka na pia waangalie maana wanakoelekea siko na anguko lao mwisho wa siku litakuwa kubwa ili kama ni kujirekebisha wajirekebishe maana naona pia kama vile tayari wamelewa sifa,na siku zote sifa huwa zinaharibu hata yale mazuri ambayo mtu alikua anafanya.
 
Back
Top Bottom