Orijino Komedi kufungwa mwezi mmoja au faini ya shilingi mia mbili

barafu

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2013
Posts
6,739
Reaction score
32,880


Leo asubuhi kuna taarifa zimezagaa, kwamba wasanii wa kundi la sanaa za maigizo (Orijino komedi) wamekamatwa kwa kuvaa sare (rasmi) za jeshi la polisi katika harusi ya mwenzao, Emmanuel Mgaya (Masanja Mkandamizaji)..

.., ikanibidi nichimbue kwenye makabrasha yangu, na kugundua kwamba.., Sheria ya Adhabu (Penal Code) kifungu cha 178 (1) inaruhusu kuvaa sare za jeshi kwa matumizi ya sanaa za maonesho jukwaani au maonyesho ya muziki ndani ya ukumbi... Sheria hiyo iko kwenye ukurasa wa 71 na inaeleza ;

178 (1) - any person who, not being a person serving in the defense forces of the United republic or in any police force established by law, wears without the permission of the president the uniform of any of those forces or any attire having the appearance or bearing any of the regimental or other distinctive marks of such uniform or attire commits an offense and is liable to imprisonment to one month or to a fine of two hundred shillings;

Provided that nothing in this in section shall prevent any person from wearing any uniform or attire in the course of a stage play performed in any place in which stage plays may lawfully be publicly performed, or in the course of a music hall or circus performance, or in the course of any bona fide military representation.

(2) any person who unlawfully wears the uniform or attire of any of the forces referred to in subsection (1), or any dress having the appearance or bearing any of the regimental or other distinctive marks of......

....., hivyo sitashangaa kesi yao ikiwa kesi 'rahisi' kwa upande wa wasanii hao, na labda jamhuri inakwenda kuangukia pua kama wakithubutu kuipeleka hii kesi mahakamani kwa tafsiri hii ya sheria.. Section (178) na subsection (1)..,

Martin Maranja Masese
 
Itakuwa ni dollar 200 kwa sbb imeandikwa kwa kingereza
 
Itakuwa ni dollar 200 kwa sbb imeandikwa kwa kingereza
The rule of the law has no assumptions regardless of the language used provided that the used language is recognised by the United Republic as one of the nationally stipulated languages, i.e, English and Kiswahili.

Kwa vile haijaandikwa USD basi moja kwa moja inakuwa ni TSH kama ilivyoandikwa
the appearance or bearing any of the regimental or other distinctive marks of such uniform or attire commits an offense and is liable to imprisonment to one month or to a fine of two hundred shillings;
 
Wakishindwa kulipa fine waniombe niwasaidie
 
mia mbili ndio,unakuta hiyo sheria ilitungwa zamani sana kipindi sh 200 ilikuwa na thamani kubwa sana.imagine ili mtu awe declared banrupt/mufilis inabid asiwe na uwezo wa kushika hata sh50 kwa mwezi,so kama unamdai mtu na akiwa na uwezo wa kupata sh50 kwa mwezi,basi atakulipa hyohyo 50/= kwa mwezi.
 
Sheria inahitaji marekebisho....Hawa wabunge huko mjengoni huwa hawayaoni haya?
 
Hakuna fine kwasababu imeruhusiwa na sheria kufanyia maigizo Hawa polisi wetu sheria Hawajui ndo maana lissu anawanyoosha kila siku kwa kukurupuka
 
Kuna sheria nyingi sana zinahitaji marekekebisho, hicho kiwango ni cha zamani sana.
 
Sheria inahitaji marekebisho....Hawa wabunge huko mjengoni huwa hawayaoni haya?

Wabunge wenyewe uliowachagua maji marefu na godlluck wa daimond ndio wanaweza kweli kuchambua sheri na kuzibadili.
 
kama unapenda wafungwe hivi,acha wivu ile ni sanaa tu mkuu!
LUBEDE naona kama hujanielewa hivi,kwanini niwaonee wivu watu ambao fani yao na yangu hazichangamani?Wivu ili iweje?Mimi nimetaka tu kwa mustakhabali wa sheria hii,iwe ni kwako au kwa mtu yotote,faini ya shilingi mia mbili imepitwa na wakati.

Sheria hii ilitungwa zamani wakati faini hiyo ni kiwango kikubwa cha pesa,wazo langu ni kuwa Wabunge wabadili hizi sheria ili ziendane na wakati!
 
Sheria inahitaji marekebisho....Hawa wabunge huko mjengoni huwa hawayaoni haya?
hata mimi nashangaa kuna makosa mengine adhabu zake ni vichekesho lakin still hawazibadilishi sheria zake.
 
barafu acha kuandika taarifa za uwongo orijino komedi wameshaomba msamaha kupitia kwa mwenzao Masanja wameachiwa huru ila wapewa onyo wasirudie tena kuvaa zile nguo za polisi bila kuwa kibali maalumu
 
barafu acha kuandika taarifa za uwongo orijino komedi wameshaomba msamaha kupitia kwa mwenzao Masanja wameachiwa huru ila wapewa onyo wasirudie tena kuvaa zile nguo za polisi bila kuwa kibali maalumu
Emma soma kwa umakini,na jadili mambo kwa staha
Hakuna mahali niliposema hawa jamaa wamekamatwa au wamefungwa,kama umeelewa "thread" yangu,ililenga kuonyesha kuwa hata kama hawa jamaa watapatikana na hatia,basi kifungo chao ni mwezi mmoja au faini ya shilingi mia mbili.

Uwe unasoma vitu na kuvielewa!!
 
Huwa kuna amendments nyingi sana kwenye Penal Code sijajuwa kama umepitia amendments zote Na Kama bado fine ni hiyo
 
Waende tu jela mwezi mmoja kitu gani. Wakitoka huko watatuletea mambo mengi mazuri tusiyoyajua.

Msalimieni Babu Seya...mwana asiye na mtetezi!
 
Kesi imeshaisha tayari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…