Orijino Komedi: Kwa faida ya nani?

Orijino Komedi: Kwa faida ya nani?

Jamani vijana wamepata mlezi, hatujui motive yake mwacheni, acheni vijana watoke kimaisha!

FD
 
Jamani vijana wamepata mlezi, hatujui motive yake mwacheni, acheni vijana watoke kimaisha!

FD

FD, Habari? unaendeleaje? Nimefurahi kukuona umerudi ukumbini. Pole sana.
 
Thank you KKN! Unajua watu hawalioni hili. US kuna kipindi cha kuchekesha Satuday Night Live ambacho kiko huru na kinaweza kikaandaa vichekesho vya yeyote yule toka Republican au Democratic bila kuwa na wasi wasi wowote. Kwa sababu wachekeshaji hao wako huru katika kuamua waandae vichekesho vya aina gani.

Sasa hawa Ze comedy kwa kujihusisha na Manji basi wameshapoteza uhuru waliokuwa nao. Manji akiwaambia kwamba sitaki muandae vichekesho vya fulani na fulani basi hawatakuwa na ubavu wa kufurukuta na kufanya vinginevyo.

Kwangu, mtazamo wako uko SAHIHI 100%.
Wanaloweza kulifanya wakiwa TBC si jingine zaidi ya kumtusi R. Mengi
Na hilo natumaini ndilo litakuwa igizo lao la kwanza. Kwa hakika vijana wamewekewa AC kaburini wakafikiri wakifukiwa humo ndo hawafi wala kuoza.
 
hizi ni sh*tty news... kila kitu kinachanganywa na siasa.. humu sasa naona kumejaa walalahoi wa mawazo !
 
Hauko wrong hata kidogo, uko very right.

Kama tunataka quality katika kazi za hawa jamaa inabidi tuweke siasa pembeni na tuwaache wafanye maamuzi yao kibiashara. Si sahihi kuanza kuwaponda kabla hatujajua hata contents za mkataba wao na Manji, hii ni dalili ya skeptism tu!

Zemarcopolo,

Nadhani umejitahidi sana kumuelimisha Bubu, lakini ukweli anaujua kabisa kutoka moyoni mwake.

Suala la Manji kuwa mlezi wa Ze Comedy siyo issue hata kidogo, suala la msingi ni maslahi ya hao wachekeshaji.

Lakini kwa upeo wake mfupi wa kuangalia kila jambo kutokea katika angle ya siasa amefikia mahali anashindwa kupata mtazamo mpya wa kujadili mambo ya kijamii. Hayumkini hata mtaani kwake anapoishi anawatambua majirani zake kwa mitazamo ya kisiasa, huenda hata chakula anachagua, labda hali Green vegetables kwa kuhofia siasa. Inawezekana hula apple jekundu na hapendi kula apple la kijani kwa fikra za kisiasa.

Mimi ningependa kuwaona Ze Comedy wananufaika na kwa kazi za mikono yao kwa njia yeyote ile ambayo ni halali na wala siyo kuwahusishia maslahi yao na mambo ya kisiasa, uhuru nk. Kinacho hitajika ni maisha bora.
 
Wazalendo waliobaki ni wachache sana almost negligible, suala la njaa linagusa wengi sana,sina hakika kama kuna mtu anaweza kuacha kuchukua mshiko toka kwa fisadi ktk mazingira ya mashaka kimaisha tuliyo nayo.

siyajui maisha ya hawa vijana zaidi ya kuwaona ktk luninga.Nao wanatamani kujenga nyumba zao na pengine kusaidia jamaa zao huko porini,ikibidi wawasomeshe watoto/wadogo zao shule nzuri.

Mlezi awe Manji au nani sijui,kikubwa malipo yao yana tija? Mtumikie kafiri upate mradi wako.

Vita vya kibiashara kwa vijana hawa si muhimu,umri unakwenda na majukumu yanakuja.Ok huyu mwingine fisadi na je huyo mwingine unajua vitu vyake? Kimsingi napenda vijana wapate cho chote kitu wapunguze ukali wa maisha basi.

Kweli kabisa,

kama ccm na kikwete wanakwiba pesa ya nchi na kujinufaisha wao wenyewe, sioni kwa nini ze comedy wasifadhiliwe na mtu ambaye ana kashfa ya zaidi ya billion 40 za mifuko ya pensheni.

Kama ccm wanaiba kupitia kwa Manji na Patel, ngoja ze comedy nao wapate pesa ya wizi. yote ni maisha.
 
Jamani vijana wamepata mlezi, hatujui motive yake mwacheni, acheni vijana watoke kimaisha!

FD

FD a.k.a MTAZAMA PANDE ZOTE ZA SHILINGI karibu tena kilingeni na pole sana
 
Swala La Kusema Manji Atawatumia Hata Wao Wanamtumia Biashara Lazima Pande Zote Zinufaike,mengi Amewafikisha Hapo Atakuaja Mwingine, Kwenye Maswala Yote Music Na Michezo Pande Zote Lazima Zinufaike,sasa Mengi Ajipange Upya Yeye Alidhani Ze Comed Wa Nini, Manji Alikuwa Anasema Nitawapata Lini, Pili Nao Wanaakili Wamelenga Ameenda Kwa Adui Ya Mengi Hiyo Safi Pia, Wanajua Kuchagua Sides Pia Itakuwa Changamoto Kwa Manji,ukileta Za Kuleta Tutaludi,kwani Hadi Sasa Hatujui Lilojili Hadi Wakaondoka,
 
Vita ya kunguru....ops sorry..vita ya panzi.....
Anyway, hawa jamaa (hasa wa asili ya Asia) wanapenda kutafuta kinachopendwa na wengi na kujiingiza (hasa hizi klabu zetu za Simba/Yanga) ili kukamilisha malengo yao....then wakifikia malengo wanawapurura na kuwaacha porini.....
Ni vema hawa jamaa wakajua hilo wakawa nammalengo thabiti, hakuna cha bure hapo...Manji akifikia lengo lake tu basi atawaacha porini (kama watakua wamebweteka).
Kimsingi sio kwamba Manji kawapenda sana Ze Comedy ila ana malengo yake!
Lakini nadhini hili si la kipoliti.
 
ze comedy yenyewe hawachekeshi tena, tangu walivyonunuliwa na kina lowasa mi najisikiliziaga kichefu chefu tu kuwaangalia.
 
Wazalendo waliobaki ni wachache sana almost negligible, suala la njaa linagusa wengi sana,sina hakika kama kuna mtu anaweza kuacha kuchukua mshiko toka kwa fisadi ktk mazingira ya mashaka kimaisha tuliyo nayo.

siyajui maisha ya hawa vijana zaidi ya kuwaona ktk luninga.Nao wanatamani kujenga nyumba zao na pengine kusaidia jamaa zao huko porini,ikibidi wawasomeshe watoto/wadogo zao shule nzuri.

Mlezi awe Manji au nani sijui,kikubwa malipo yao yana tija? Mtumikie kafiri upate mradi wako.

Vita vya kibiashara kwa vijana hawa si muhimu,umri unakwenda na majukumu yanakuja.Ok huyu mwingine fisadi na je huyo mwingine unajua vitu vyake? Kimsingi napenda vijana wapate cho chote kitu wapunguze ukali wa maisha basi.

Mkuu!!!!

Umemaliza kila kitu hapo juu!!!, we should note that at the end of the day hawa jamaa wanataka maslahi for the betterment of their livelihoods, so far so good kwa kile walicholikuwa wakikifanya wakikiendeleza sioni kuondoka kwa manji kama kutawaathiri wao kama kundi as much as mkataba wao na TBC utabakia pale pale.

Labda tu cha msingi ambacho wadau wengi humu ndani wamekishauri ambacho naamini hata wao wenyewe their wise enough to note ni the way how hawa wenzetu waaasia wanavyopenda ''kukutumia then they damp you!'

Naomba ni-copy na ku-paste msemo wao hapo juu....mtumikie kafiri upate mradi wako!!
 
Jamani eh!! si tusubiri burudani hayo mambo ya Manji kuwa na maslahi binafsi kwa watu kama akina JOTI maslahi gani?? au mnadhani wakiigiza sauti ya Mengi itakuwa tabu??? kwa kuwa tu wametoka EATV??

Waacheni nao wahangaikie matumbo yao wanajua wanachofanya mbona wote wajanja kikundi cha watu 7 wote wakubali kulishwa ujinga????watakuwa wamerogwa basi....
 
Jamani hapa vijana wa ze comedy wanatafuta maisha nyinyi mnamaisha yenu, wengine nyie ni mafisadi wadogo, wengine mabosi wakubwa.
SASA vijana kutafuta GREEN PASTURES manaingiza siasa, ACHENI HIZOOOO! Hamna tofauti na watanzania wa JF waliokimbia TZ kutafuta maisha abroad.

Ugomvi wa Mengi na manji hauwahusu kabisa,after all, MENGI kwenye kulipa ni mgumu kama jiwe ingwa vijana wamememuingizia hela nyingi sana karibu na BINGO.

Manji ni mlezi tu katika kusaidia kuwaongoza na kuonyesha njia kama mengi alivyowanynyua kufika hapo licha ya kuwanyonya.

Mkataba na TBC ukiisha kama bado wako kwenye chart watapata mkataba mwingine mnono sehemu nyingine hivyo ni CHALENGE kwao ili waendeleee "kusavaivu"
 
Jamani, samahanini kwa yale nitakayoandika hapa leo. Kuna jambo fulani huwa linanikera sana. ni kuhusu hawa jamaa wa ze comedy. Hivi kwanini huwa wanajiexpress kama vile ni mashoga?kwanini wanaume wenye ndevu kama wale wanakuwa wanavaa nguo za kike, wanapaka wanja na kulembua mimacho kama mashoga fulani hivi? hivi kweli hawa sio mashoga hawa?, wamechafua jamii, hadi mtoto mdogo anawaiga kina joti. watu wengi wanaotoka nje, na wanaoangalia tv toka nje ya tz, wanatucheka sana, wengi wanafikiri ndo watz tulivyo.

Hivi wale jamaa huwa wanatoa ujumbe gani? Kwasababu hata wakitoa ujumbe, huwa unaonekana haupo kwasababu mambo wanayoyafanya ni ya kitoto sana, na wanakera kuwaangalia kwasababu ni kama mashoga. KWANINI WASIMSHIRIKISHE HATA MWANAMKE MMOJA TU wadada waliojaa hapa bongo kama nini hawa ndo awe anajiexpress kama mwanamke? unajua kuna siku tz watu kama kina joti watakuja kubadilishwa na kuwa....., Jamani, naomba mniambia, hivi ninyi na usomi wenu wote mnashabikia ze comedy, umekaa na mke wako unashabikia zecomedy, hivi wanaongeza nini kwenye akili yako? the way masanja anavyofanya, the way joti anavyofanya, na yule mwanamke wa kinyakyusa, hivi kweli wanatuongezea nini?

Nisemacho ni hikii, hivi hawa jamaa hawawezi ku express kitu fulani cha kiustaarabu kutuwakilisha watz kuwa ni watu wastaarabu sio wa kitotokitoto kama vile? nchi gani ulishawai kuona hadi viongozi wanashabikia utumbo kama huu?, mimi nawashari, waacha kujifanya mashoga, napenda wafanye kazi ili wapate ugali wao wa kila siku, lakini wanatakiwa waombe ushauri kwa ma intellectuals ili wafanye kwa ustaarabu wa kuifaidisha jamii sio kuishia kucheka tu na hakuna ujumbe wa maana. pia, wanatakiwa wawashirikishe walau wanawake kwenye kundi lile kwasababu wanavyojifanya mawanawake, wanajiaibisha na kuliaibisha hadi taifa zima. utumbo huu siupendi kishenzi. asante.
 
Ukisema they are unoriginal in that aspect nitakubali, ukisema wanaaibisha taifa nitakuona unataka kutupeleka kwenye sharia na mambo ya kina Ahmadinajad.

Utoto toto ndiyo style yao, kama hupendi flip channel au anzisha column ya performing art critique .Jamaa wana fan base kubwa na inaonekana watu wanapenda "ujinga" wao.

In short they are the "Shakespearean Fool" if you are acquinted with the idea, a fool who foolishly delivers a sensible message.Ndiyo maana watu wanawapenda.

Mimi napenda wanavyo expose pretentiousness kuanzia kwenye mimicking yao ya tone za watangazaji mpaka ku mock kauli na vitendo vya viongozi na vibosile.
 
ASPECTS OF COMEDY

The elements and techniques of comedy are diverse and differ from culture to culture. As much humour is derived from exaggeration, distortion, or inversion of cultural norms, what provokes laughter among one group of people may prove incomprehensible to another. In addition, more than tragedy or serious drama, comic entertainment is bound by social conventions that define the boundaries of acceptable humour and topics that are taboo or off-limits for humour. What is considered funny in one place and time may be forbidden or viewed as infantile or in poor taste in another. However, virtually every component of human behaviour is subject to comic treatment. This includes bodily functions, manners, fashion, eating, family quarrels, sexual desire, courtship, the procurement of money and social position, violence and punishment, religious piety, racial and social differences, vain presentations of self, physical shortcomings, cheating and lying, reversal of gender roles, and abnormal fear of ageing and death.
 
unafurahia nini kuona mwanaume mwenzio analembua majicho na kupakaa wanja kama vile, na wewe umekaa na mke wako mnaangalia litiviii. utumbo gani ule? wamekosa walau wanawake wawili tu kuwa nao mle ndani? kwasababu, kama ni utoto na utumbo, hiyo afadhali, kinachokera, ni kujifanya mawanawake, yanakera kishenzi. au ninyi mnashabikia ushoga?
 
Jamani, samahanini kwa yale nitakayoandika hapa leo. Kuna jambo fulani huwa linanikera sana. ni kuhusu hawa jamaa wa ze comedy. Hivi kwanini huwa wanajiexpress kama vile ni mashoga?kwanini wanaume wenye ndevu kama wale wanakuwa wanavaa nguo za kike, wanapaka wanja na kulembua mimacho kama mashoga fulani hivi? hivi kweli hawa sio mashoga hawa?, wamechafua jamii, hadi mtoto mdogo anawaiga kina joti. watu wengi wanaotoka nje, na wanaoangalia tv toka nje ya tz, wanatucheka sana, wengi wanafikiri ndo watz tulivyo.

hivi wale jamaa huwa wanatoa ujumbe gani?kwasababu hata wakitoa ujumbe, huwa unaonekana haupo kwasababu mambo wanayoyafanya ni ya kitoto sana, na wanakera kuwaangalia kwasababu ni kama mashoga. KWANINI WASIMSHIRIKISHE HATA MWANAMKE MMOJA TU wadada waliojaa hapa bongo kama nini hawa ndo awe anajiexpress kama mwanamke? unajua kuna siku tz watu kama kina joti watakuja kubadilishwa na kuwa....., Jamani, naomba mniambia, hivi ninyi na usomi wenu wote mnashabikia ze comedy, umekaa na mke wako unashabikia zecomedy, hivi wanaongeza nini kwenye akili yako? the way masanja anavyofanya, the way joti anavyofanya, na yule mwanamke wa kinyakyusa, hivi kweli wanatuongezea nini?

Nisemacho ni hikii, hivi hawa jamaa hawawezi ku express kitu fulani cha kiustaarabu kutuwakilisha watz kuwa ni watu wastaarabu sio wa kitotokitoto kama vile? nchi gani ulishawai kuona hadi viongozi wanashabikia utumbo kama huu?, mimi nawashari, waacha kujifanya mashoga, napenda wafanye kazi ili wapate ugali wao wa kila siku, lakini wanatakiwa waombe ushauri kwa ma intellectuals ili wafanye kwa ustaarabu wa kuifaidisha jamii sio kuishia kucheka tu na hakuna ujumbe wa maana. pia, wanatakiwa wawashirikishe walau wanawake kwenye kundi lile kwasababu wanavyojifanya mawanawake, wanajiaibisha na kuliaibisha hadi taifa zima. utumbo huu siupendi kishenzi. asante.

Funua kamsi kisha angalia Comedy maanake.
Hilo litakuwa jibu sawia kwako kwa maana unataka kutupeleka ndiko siko.
 
Back
Top Bottom