Orijino Komedi: Kwa faida ya nani?

Ndo usanii wenyewe huo mkuu,si ni waigizaji?Maana ya uigizaji ni kuwa wanaigiza/nakili kile kilichotokea kwenye hali halisi.
We mbona hoja yako imekua kama imelenga kuwaporomosha?we EATV nini?Af kwa taarifa yako Kenya nao wanakundi lao la REDKYULAS ambao nao wanatumia style hizohizo pia Uganda sema makundi ya wenzetu hawa majirani wameenda shule kidogo ukilinganisha na ze komedi.Hata hivyo hufungwi kutizama ukiona yakuboa then badilisha channel ila ukweli ni kuwa vijana hawa wamepata umaarufu mkubwa tokana na huo usanii wao
 

Si lazima uangalie, flip channel. Hii wala si cable service kusema unalipia na kwa hiyo uko entitled kuchagua content.Kuna watu wanaona hiyo "inversion of cultural norms" and laugh it of, kama wewe hupendi kuangalia si lazima uangalie, hujalazimishwa.
 
jamani wengine mna hoja hafifu nini maana ya Comedy?
Wa jiite comedy then wasichekeshe? maajabu
 
The comedy ndio jina lao so wanaweza kufanya lolote la kitotototo au lakizeezee mbona ujumbe na mafundisho yanapatika kama unaelewa hasa nini wanafanya wale vijana kuhusisha wasichana au wanawake sioni kama ni tatizo pia ilimradi ujumbe uwafikie watizamaji, mbona kina Martin Lawrence huwa wanavaa kama wanawake?
 
Funua kamsi kisha angalia Comedy maanake.
Hilo litakuwa jibu sawia kwako kwa maana unataka kutupeleka ndiko siko.

Kwa kumsaidia Mbeba Maono,

Comedy: A dramatic work that is light and often humorous or satirical in tone and that usually contains a happy resolution of the thematic conflict.

Wapo wangapi ambao hawana hata moja la kubuni mtaani? Kama inaaibisha taifa angejaribu kuchunguza kipindi ipo hewani siku ya Alhamisi kama aliweza kuona watu wanavyowahi majumbani kwa namna moja ama nyingine nikipindi muhimu sana kwa wana familia kurudi mapema nyumbani. Ingekuwaje kama siku Mbeba Maono unapita mtaani anakutanao wanakupiga roba kwa kukosa fedha ya kujikimu maisha. Acha zako wewe.
 
mbeba maono ana matatizo ya problem, yuko too stiff.
watu wanaopata picha ya watanzania kama tunafanana na kina joti basi wanamatatizo kama yako. wala hatuna haja ya kujisumbua nao.
 

Huyu jamaa ametumwa na EATV mbona tumegundua lasivyo anatoka IPP media hiyo hoja si hoja haelewi maana ya COMEDY....inaendana na ubunifu wa vichekesho.
 
... ndio wale wale wanaofikia hatua ya kutaka wawe na uwezo wa kuwachagulia watu ni mavazi ya aina gani wavae!
 

Kwani mashoga hawamo katika jamii? Ni wadogo zetu, ni ndugu zetu sasa ya nini kuwakana?

Kama ulivyoambiwa, kama yana kukera, si unayo remote?
 
Hiyo heading ... utadhani laashiria jambo kubwa na la ajabu !!
Mods wahamishe hii kenda kwenye vituko??
 
Umewahi kusikia wimbo wa "Mume wangu Jerry" wa DDC Mlimani Park?
 
kama wanakukera,best advice ni kuflip channel, kufanya comedy kwa kuvaa kama mwanamke its their style...thats called being creative!
 
Wewe mmbeba maono, me naona unayako tu yanayokusibu, wale wapo kazini na kwa njia ile ndo wanapata ugali/mbona. sioni cha ajabu pale. kama hupendi kuwaangalia hulazimishwi acha angalia chanel zingine.

Kwani huelewi maana ya Commedy??

mimi nawapenda sana huwa wananifurahisha na kila nichekapo naongezewa siku za kuishi hapa duniani. kwi kwi kwi
 
Mkuu mbeba maono picha nnayopata kutoka kwako ni kwamba ukiwa pale kwa living room remote huwa hagusi mtu!!!!!!!!! Enywayz nna kakwesheni kidogo, wanaliabisha taifa kwa nani??????????
 

Ametumwa na EATV huyu..si bure!
 
Ivi jamani humu watu wanaingia baada ya kuchambua wanayo taka kusema au basi tuuu,sasa wao washa jiita ze comedy what else tena wakajaribu kuweka hadi kwa swanglish still mtu unafikiri ni kweli basi kusiwe na hata maigizo!!!
 

You are very wrong my friend.Incase you didnt know what a comedy is?A real comedian has to be able to tune him/her self to any character.Hao watu unaosema wanaona wa tz ndivyo tulivyo siamini.mtu anaye jua what is comedy atakubaliana na mimi kwenye hili nadhani huja watch comedy za kutosha kufahamu hili.
 
Mkuu mbeba maono picha nnayopata kutoka kwako ni kwamba ukiwa pale kwa living room remote huwa hagusi mtu!!!!!!!!! Enywayz nna kakwesheni kidogo, wanaliabisha taifa kwa nani??????????

Hii point ya maana sana ni nani huyo anayeaibishwa?Kapteni Komba au wewe?ebu kajipange vizuri uje na thread nyingine.
 
Kabla ya wao kuhitimisha mkataba wao na EATV nilikuwa na zaidi ya miezi miwili sifuatilii maonesho yao. Si kwa sababu walikuwa wanvaa kama wanawake ama kurembua mimacho na kupaka hina na wanja, la hasha.
Kuna kauli walizokuwa wakizitoa mpaka nafikiri kama mtu umekaa na mama yako mzazi na anaelewa tukiswahili twa pwani inakuwa aibu kubwa sana. Na hasa kauli nyingi za joti awapo kwenye utangazaji zilikuwa hazinivutii kabisa kwani zilibeba ujumbe wa matusi ndani yake (sitaki hata kukumbuka). Shida ni kwamba walio wengi wanaangalia sanaa ya vichekesho kwa mtazamo mwingine, lakini ni kweli kabisa kuwa sanaa hiyo in kitu cha kufanya katika jamii yetu. Na kwa wale waliopitia fasihi kidogo (mimi si mtaalam) watakubaliana nami kuwa sanaa ya maigizo ni ngeni kwetu na tunafanya vitu vya kuiga na si halisi kwa upande wetu. Shida nionayo mimi ni pale tu tunaposhindwa kipi cha kuchukua na kipi cha kuacha (kwa wasanii). You conceive, you incode bofere you deliver.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…